Watumishi wa Umma, Toshekeni na mishahara yenu

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,478
Wasalamu wana Jf,

Katika hizi siku mbili kumekua na mixed feelings kuhusu ongezeko la mshahara lililosubiriwa kwa takribani miezi mi-tatu.

Wapo wanaona ongezeko hilo ni dogo na ni mockery kwa "watumishi wa umma", pia wapo wanaodhani hao watumishi hawastahili, si tu ongezeko, bali hata hiyo mishahara wanayolipwa kwa uzembe, ubadhirifu na kukosa uweledi wanapofanya kazi zao, na pia wapo ambao hawaoni kwanini suala hili binafsi yaani kati ya mwajiri na mwajiriwa liwekwe wazi barazani lijadiliwe na ata wasiohusika.

Katika kuchakata hayo yote tajwa hapo juu, kwangu mimi nadhani mshahara haujawahi kumtosha mtu yoyote, haijalishi unalipwa shilingi moja au trillion. Serikali sikivu ya mama SSH imefanya gesture ya kuwaambia wafanyakazi inawajali, yaani pamoja na mapito magumu ya covid 19 na vita ya Ukraine, bado inaweza kufanya kitu kwa ajili yao. Ieleweke kwamba, nchi hii si ya wafanyakazi pekee, wapo wakulima, wavuvi, wafanyabiashara, wafugaji, na hata viongozi wa dini je hao wengine nani anawaongezea vipato vyao?

Aidha, ieleweke kwamba kila mtu ni mtumishi wa umma kwa nafasi yake. Wafugaji wanautumikia umma kwa kutupatia vitoweo halikadhalika wavuvi. Wakulima nao kwa kujitoa mashambani wanautumikia umma kwa kutupatia chakula pia na wafanya biashara kwa kutuletea bidhaa nyingi tunazozihitaji. Kimsingi, ata ma dada poa wanautumikia umma kwa nafasi yao. Hivyo basi, hawa waajiriwa wa serikali wakae kwa kutulia wajue kwamba utumishi wa umma siyo kuwepo kwenye ajira za serikali bali ni dhana pana na jumuishi.

Kwa kuhitimisha, wafanyakazi wa serikali lazima wajue kwa kukubali kwao kuutumikia umma, waliamua kuishi maisha ya kujitolea na waache tamaa za fedha na mali.

Umma wa wa Tanzania utawalipa kwa kadiri kipato cha nchi kinavyoendelea kukua. Ni rai yangu wafanyakazi wa serikali wataongeza bidii makazini ili kutoa huduma bora na kuongeza tija kwenye utendaji wao.

Nawasilisha.
 
Sifa mojawapo kwa wafanyakazi ni kupigania mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kila siku, mazingira bora ya kufanyia kazi, bima ya afya, pensheni ya kueleweka, nk.

Na siyo kutosheka na mishahara wanayopata! Maana siku zote huwa haitoshi kwa wafanyakazi walio wengi.
Hivyo jitahidi tu kukubaliana na ukweli.
 
Wazo lako zuri nimelichukua
 
Pia ukiona haikukidhi au kukutosha , pia unaweza acha hiyo kazi na kutafuta nyingine itakayokukidhi pia , maana usimlazimishe boss akulipe vizuri wakati huo uwezo wa kukulipa vizuri hana
 
Pia ukiona haikukidhi au kukutosha , pia unaweza acha hiyo kazi na kutafuta nyingine itakayokukidhi pia , maana usimlazimishe boss akulipe vizuri wakati huo uwezo wa kukulipa vizuri hana
Exactly
 
Back
Top Bottom