Watumishi wa Safina Radio (Arusha) acheni kumuiga Mwl. Mwakasege, mnaboa sana

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
20,025
2,000
Habarini Wadau,

Kama kawaida Mods, lengo si kukashifu ibada/huduma ya watu bali kuonya na kurekebisha

◆ SAFINA REDIO ni redio iliyopo jijini Arusha iliyoanzishwa miaka michache tu ya nyuma.

Niliwahi kuhudhuria ibada yao mara 2 na pia mara huwa naisikia kupitia redio za watu mbalimbali nikiwa Arusha.Muasisi ni Mzee Daniel Lema.

◆ Mwl. Christopher Mwakasege: Ni muumini halisi wa kawaida katika Kanisa Kiinjili la Kilutheri KKKT (Usharika wa kijenge) na mwalimu wa neno la Mungu kupitia huduma yake ya MANA.

Safina Redio Mnajiaibisha kwa tabia zifuatazo :

■ MNAIGA HUDUMA YA MWAKASEGE.

- Mfano wa kwanza:-

* Kuongea kama Mwasege:

baadhi ya Watumushi wa Safina Redio wanaongea kabisaa kama Mwakasege mpaka mtu unajiuliza iki iweje sasa? Mfano anavyosema

"Ooh halelujah haleluja" au

"Glory to God, glory to God"

Hasahasa "Otieno"

sasa mnaigaje huduma? Kweli mnaongozwa na Roho wa Mungu au na nafsi na maamuzi yenu ili mkubalike na waumini?

* Kutolea mifano kama ya Mwakasege pamoja na kutoa Shuhuda kwa namna ile ile anavyofanya Mwakasege katika huduma yake :

Pia hapa Mnaboa sanaa kuiga ule mtindo wa kuwaita watoa ushuhuda mmoja mmoja kisha utasikia

"Sifa kwa nani"

* Daah, Acheni kuiga iga, kuiga kutawafanya waliokomaa kiroho kugundua kuwa ninyi mnaongozwa na Maamuzi yenu au ya Daniel Lema na si na Roho wa Mungu.

■ MNASISITIZA MICHANGO NA SADAKA KULIKO KUOKOA ROHO ZA WATU:

Lengo la Yesu Kristo na Ukristo wenyewe ni Kuwaleta watu karibu na Mungu na kukuza uhusiano wao na Mungu

Safina Redio kila Jumanne, Alhamisi na Jumamosi sio siri huwa wanasisitiza zaidi utoaji wa Sadaka na Mchango wa Mnara/Minara kuliko kuwajenga watu kiroho.

Kwa anayebisha awasikilize hawa jamaa (Watumishi) ataamini hayo.

Msiige huduma, Mnakera...

Ongozweni na Roho wa kweli.
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
20,025
2,000
acha kutangatanga Mwamini Mungu peke yake shika amri zake fata maagizo yake enenda katika njia zake wachana na ministry za wafia tumbo
Wala mimi sintokaa nitange tange ila hawa wanaoanzishwa hizi huduma huduma mara sijui ministry wanashangaza sana.

Wanatafuta kiila mbinu ya kuwakamata watu na kuwafanya wawaamini.

Kama hawa Safina Redio sasa.
 
Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
23,985
2,000
Wala mimi sintokaa nitange tange ila hawa wanaoanzishwa hizi huduma huduma mara sijui ministry wanashangaza sana.

Wanatafuta kiila mbinu ya kuwakamata watu na kuwafanya wawaamini.

Kama hawa Safina Redio sasa.
MWAKASEGE ,RADIO SAFINA NA WENGINEO NI HAO HAO KWANGU MIMI NAMUAMINI MUNGU KUNA AMRI ZAKE PALE NA MAAGIZO YAKE BASI NIMEMALIZA
 
KARANJA 007

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
6,002
2,000
MWAKASEGE ,RADIO SAFINA NA WENGINEO NI HAO HAO KWANGU MIMI NAMUAMINI MUNGU KUNA AMRI ZAKE PALE NA MAAGIZO YAKE BASI NIMEMALIZA
Aaaaah bhana Ntafuta bhaaaanaaaaaaa usimalize tafadhali bhaaanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Pascal A

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
205
225
Habarini Wadau,

Kama kawaida Mods, lengo si kukashifu ibada/huduma ya watu bali kuonya na kurekebisha

◆ SAFINA REDIO ni redio iliyopo jijini Arusha iliyoanzishwa miaka michache tu ya nyuma.

Niliwahi kuhudhuria ibada yao mara 2 na pia mara huwa naisikia kupitia redio za watu mbalimbali nikiwa Arusha.Muasisi ni Mzee Daniel Lema.

◆ Mwl. Christopher Mwakasege: Ni muumini halisi wa kawaida katika Kanisa Kiinjili la Kilutheri KKKT (Usharika wa kijenge) na mwalimu wa neno la Mungu kupitia huduma yake ya MANA.

Safina Redio Mnajiaibisha kwa tabia zifuatazo :

■ MNAIGA HUDUMA YA MWAKASEGE.

- Mfano wa kwanza:-

* Kuongea kama Mwasege:

baadhi ya Watumushi wa Safina Redio wanaongea kabisaa kama Mwakasege mpaka mtu unajiuliza iki iweje sasa? Mfano anavyosema

"Ooh halelujah haleluja" au

"Glory to God, glory to God"

Hasahasa "Otieno"

sasa mnaigaje huduma? Kweli mnaongozwa na Roho wa Mungu au na nafsi na maamuzi yenu ili mkubalike na waumini?

* Kutolea mifano kama ya Mwakasege pamoja na kutoa Shuhuda kwa namna ile ile anavyofanya Mwakasege katika huduma yake :

Pia hapa Mnaboa sanaa kuiga ule mtindo wa kuwaita watoa ushuhuda mmoja mmoja kisha utasikia

"Sifa kwa nani"

* Daah, Acheni kuiga iga, kuiga kutawafanya waliokomaa kiroho kugundua kuwa ninyi mnaongozwa na Maamuzi yenu au ya Daniel Lema na si na Roho wa Mungu.

■ MNASISITIZA MICHANGO NA SADAKA KULIKO KUOKOA ROHO ZA WATU:

Lengo la Yesu Kristo na Ukristo wenyewe ni Kuwaleta watu karibu na Mungu na kukuza uhusiano wao na Mungu

Safina Redio kila Jumanne, Alhamisi na Jumamosi sio siri huwa wanasisitiza zaidi utoaji wa Sadaka na Mchango wa Mnara/Minara kuliko kuwajenga watu kiroho.

Kwa anayebisha awasikilize hawa jamaa (Watumishi) ataamini hayo.

Msiige huduma, Mnakera...

Ongozweni na Roho wa kweli.
Kama wanaiga kwa utukufu wa Mungu hamna shida. Ila kwangu sioni tatizo wala kuiga. Kwani glorly to God ni ya mwakasege au ni neno linalompa utukufu Mingu. Acha kazi ya Mungu isonge mbele
 
The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,895
2,000
MWAKASEGE ,RADIO SAFINA NA WENGINEO NI HAO HAO KWANGU MIMI NAMUAMINI MUNGU KUNA AMRI ZAKE PALE NA MAAGIZO YAKE BASI NIMEMALIZA
Mungu hayupo, kama yupo baai atakua amezeeka sana na hata hakumbuki kama kuna viumbe wake wanaitwa binadamu, achana na imani ambazo hazina maana.
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
20,025
2,000
Kama wanaiga kwa utukufu wa Mungu hamna shida. Ila kwangu sioni tatizo wala kuiga. Kwani glorly to God ni ya mwakasege au ni neno linalompa utukufu Mingu. Acha kazi ya Mungu isonge mbele
Hapana kutamka sio vibaya ila ukiwasikiliza vizuri ni kwamba target yao ni kuongeza idadi ya waumini na kuwazuia wasiende kwingine.

Kuna wakati wanasema kabisa "ooh wanakuambia utoke safina" waambie sitaki!!!

Ninachomaanisha utaelewa ukiwasikiliza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom