Mwl. Mwakasege: Vijana epukeni kujibizana kwenye Social Media

MzeeKipusa

JF-Expert Member
Feb 10, 2023
2,706
4,923
Shalom Aleichem!

Ndugu zangu Watanzania,

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwà kudra zake , lakini pia namshukuru kwà kuendelea kumlinda na kumuongoza Rais wetu mpendwa Mhe. Rais . Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN.

Ndugu zangu, jana nilipost humu Jamii forum thread ambayo ilikua ikimhusu Mwl. Mwakasege akisema aliwahi kufika Mbinguni ambako aliweza kukutana na Nabii Musa pamoja na Bwana Wetu Yesu Kristo wa Nazareth. Itoshe kusema thread hiyo ilikua na mjadala mrefu sana ambao mpaka sasa hivi bado unaendelea.

Leo hii pia nimepata nafasi ya kumtizama Mwalimu huyo via Upendo TV,...na nilichokigundua ni kwamba ,..kumbe hata na yeye pia ni miongoni mwa watu waliopata nafasi ya kuipitia thread niliyoiandika kumhusu yeye.



Sasa Ndugu zangu, (yeye Mwl. Mwakasege) katika kujibu hoja za thread niliyoiandika....amewahimiza kondoo wake ( hasa vijana) kutokufanya najibizano katika Social Media. Na tena kasisitiza kuwa , kuna roho za udanganyifu ambazo zinaweza kuwatoa kwenye reli.

Sasa Mimi naomba niseme yafuatayo kwakua najua kwanini kawaambia hivyo kondoo wake.

1. Ni jukumu letu sote kama Watanzania kuhakikisha Taifa letu linakua salama wakati wote.

Ili Taifa liwe salama , linahitaji vitu viwili

1. Silaha ( Hii ni Sawa na nuru na ni kwà ajili ya kulilinda TAIFA)

2. Maarifa ( Haya ni Sawa na Mwanga na ni kwà ajili ya kuliongoza Taifa)

Ndugu zangu, vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kama vikijikita katika kuinvest kwenye silaha peke yake na likasahau kuinvest kwenye maarifa, au likawaachia watu waspreed maarifa ya hovyo yasiyokua na tija, ni dhahiri Taifa letu litaangamia , na tena kutakua na mmomonyoko wa maadili uliothikiri.


Nakumbuka , Hayati Mahatma Gandhi kuna siku aliwahi kutembea na nuru yenye Chemli , kwà lengo la kuwawashia Mwanga Wananchi wa India ili MWANGA huo uwaongoze kwenye Amani ya kweli. Lakini jambo hilo lilikua la Muda tu kutokana na uhalisia wa Nuru hiyo ( fake light) ambayo haikua na Mwanga wa kutosha.


2. Ni vyema viongozi wa dini katika Taifa letu wakubali kukosolewa. Wasijione wao ni malaika na wasipende kuwakumbatia watu ili wapate fedha nyingi wanazowaomba kwà njia ya Sadaka.

Social Medias, hasa Jamii forum, ni app nzuri sana hasa katika mambo ya kutoa Maoni au kurekebisha kasoro za watu hasa viongozi wetu. Kwasababu hii App inakufanya unakua Anonymous..usijulikane...unakua free kuairout your views / opinions kwà lengo zuri tu la kuwafanya wahusika wacorrect errors zao + mistakes zao.


Baada ya kusema hayo, itoshe tu kusema...Mimi ni Mtanzania ambaye ni Mzalendo, Muaminifu, Mtiifu na Mnyenyekevu. Hakuna mtu aliyenituma kuandika haya...ni Maamuzi yangu mwenyewe , ambayo yamenipa uthubutu na utayari wa kusema ukweli huo.


"MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA"
View attachment 2594507
 

Attachments

  • 1284edb5c084dd3c53f58d378eab4c89.mp4
    2.2 MB
kasema kuna nuru ya kweli na nuru feki. Hii nuru feki inaigiza nuru ya kweli ili ifanye uharibifu. Sawa, yeye kama mfuasi wa nuru ya kweli na anaihubiri, vipi kuhusu ubatizo wa maji mengi mbona hajawahi kufundisha hilo kama ni hitaji la kutimiza haki yote ya maisha ya wokovu?
 
kasema kuna nuru ya kweli na nuru feki. Hii nuru feki inaigiza nuru ya kweli ili ifanye uharibifu. Sawa, yeye kama mfuasi wa nuru ya kweli na anaihubiri, vipi kuhusu ubatizo wa maji mengi mbona hajawahi kufundisha hilo kama ni hitaji la kutimiza haki yote ya maisha ya wokovu?
Nuru na Mwanga ni vitu viwili ambayo ni muhimu kusemwa au kufundishwa kwà pamoja. Akifundisha kimoja na akaacha kingine maana yake inakua ni Half truth.

Kwasababu kinacho waangamiza watu sio Kukosa nuru ( silaha)... bali ni Kukosa Mwanga ( Maarifa) .

Ukigombana na mtu, silaha anaweza kuipata sehemu yeyote ile...anaweza kuchukua hata kiti au kitu chochote kilicho karibu yake na akakupiga nacho...., Issue ni Maarifa!!!
 
kasema kuna nuru ya kweli na nuru feki. Hii nuru feki inaigiza nuru ya kweli ili ifanye uharibifu. Sawa, yeye kama mfuasi wa nuru ya kweli na anaihubiri, vipi kuhusu ubatizo wa maji mengi mbona hajawahi kufundisha hilo kama ni hitaji la kutimiza haki yote ya maisha ya wokovu?
Hili la maji mengi au machache natafuta kwenye biblia ila sijawahi kupaona kwakweli..Ila naonaga tu ubatizo ni agizo ni sawa na kushiriki chakula cha Bwana.Yesu alimega mkate halisi na kikombe kikubwa cha divai.lakini tunashiriki kidogo na hapa hatugombani.
 
Nimeishia hapo kwenye M. Gandhi mkuu.... Ni siyo Gandhi ni SOCRATES mkuu hapo umetupiga
Soma Historia yake vizuri...., Concept hiyo aliicopy kwà SOCRATES
quote-even-a-single-lamp-dispels-the-deepest-darkness-mahatma-gandhi-65-72-20.jpg
 
kasema kuna nuru ya kweli na nuru feki. Hii nuru feki inaigiza nuru ya kweli ili ifanye uharibifu. Sawa, yeye kama mfuasi wa nuru ya kweli na anaihubiri, vipi kuhusu ubatizo wa maji mengi mbona hajawahi kufundisha hilo kama ni hitaji la kutimiza haki yote ya maisha ya wokovu?
Yani ukibatizwa na maji mengi ndio unakuwa umeokoka?
 
Ile ni kazi kama kazi zingine, mwisho wa siku kipato kipatikane maisha yaendelee
Ile ni Kazi ya Mungu Ndugu yangu sio Kazi ya watu. Kazi ya Mungu hainaga makosa! You must be sure na unachokiongea au kukisema, otherwise ni Sawa na mtu aliyejituma tu mwenyewe kuifanya.
 
Mimi huwa nashangaa sana pale ambapo anasema anaombea watu wajazwe na Nguvu za Roho Mtakatifu na kisha wanaanza kunena kwà lugha.


Lugha yenyewe sasa;-


"Yendorobo katapaka teka kebosndoro....."

Yani kila mtu ni " Yendorobo..."

Kwamba, ilitakiwa wanene kiyunani ama ki-igbo ndiyo ukubaliane nao, ama?.
 
Back
Top Bottom