Watumishi wa maofisini na vijimambo vyao!

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
244
Reaction score
166
Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusiana na upotezaji muda unaofanywa na waajiriwa ni kwamba, wafanyakazi maofisini huwa wanapoteza saa tatu kila siku katika kufanya mambo ambayo hayana maana kwa mwajiri au kwa kazi zao.

Kwa wale ambao wan mitandao ya intenet maofisini mwao na wanaweza kuiangalia kwa kadiri wanavyopenda hutumia dakika 54 kwa siku kuangalia mitandao hiyo.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 18 kila siku kuchungulia madirishani. Hata wale ambao viti na meza zao katikati ya ofisi, huwa wanasimama na kwenda kuchungulia madirishani mara kwa mara. Kwa wastani hutumia dakika 18 kutwa.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 14 kwa kwenda kujisaidia au kwa wanawake kwenda kujipamba au kujipodoa upya bafuni au vyooni. Ile nenda rudi ya kujisaidia au kujipodoa upya huchukua wastani wa dakika 14 kila siku. Kumbuka, kuna watu hujisaidia haja kubwa hata kwa dakika kumi.

Watumishi wa maofisini yaani wale ambao hukaa ofisini, hutumia dakika 35 kila siku kupiga soga zisizohusiana na kazi na pengine zisizo na maana sana. Soga zinazohusu mpira, siasa, ufuska, majungu na umbeya mwingine hutawala.
Halafu hutumia dakika 17 katika kunywa kahawa au chai na pengine soda. Inaweza kuwa wananywea kwenye mighahawa ya kazini au pale ofisini walipo. Wengine wakati wakiwa wanakunywa kahawa au chai hawagusi kazi kabisa.

Siku hizi maofisini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuteka mawazo au akili ya watumishi. Vitu kama mitandao viriba vya chai na kahawa vya kujichotea na mengine mengi yanafanya kujikuta mtumishi ameacha kazi na kuingia katika kitu kingine.

Lakini watumishi wengi wa maofisini hasa wale ambao wanatumia muda mwingi ofisini,inadaiwa kwamba, hawafanyi mazoezi. Hii inasababisha watumishi wengi wa kazi za aina hiyo kufa au kustaafu mapema kutokana na ubovu wa afya.
 
Kuna ukweli hapa ofisi moja nlienda bosi anapiga story 1hour na ukimgöngea anasema subiri ,ukisikilza wanayoongea ni upuuzi mtupu.
 
Du hili ni bonge la reseach, wewe kweli ni great thinker..................
 
niko natafuta thread moja hapa JF ambayo imewekwa na member mmoja na inahusu Kaburu Botha alivyosema juu ya Waafrika. Niliingalia haraka na ikavuta hisia zangu sasa nataka niisome vizuri ili kujua juu ya ukweli huu unaoumiza alafu nitarudi huku kutoa maoni yangu.
na ndo wa kwanza kudai nyongeza ya mshahara!!
 
..hapo hujataja ofisi zenye tv. Kipindi cha bunge hakuna kazi yoyote inayofanyika. Pia muda mwingi unapotea kwn kuchat kwa sms, kusoma magazeti,
 
Hapo kati pia kuna muda wa kwenda kungonoka kwani wale wana ndoa inabidi baada tu ya kazi wawahi kwa wake/waume zao.
 
True that. Very True. Hapo hujaweka kuomba Ruhusa za mara kwa mara, sijui mtoto anaumwa naenda hospitali, sijui nimefiwa naenda mazishi, sijui leo naenda kuchezwa Ngoma mwali anatolewa nje. blah blah......
Kuna rafiki yangu mmoja Mkenya,amewekeza hapa TZ,na ametajirika akiwa hapa hapa TZ, anasema Watanzania tupo usingizi, hatufanyi kazi, ni kulalamika na porojo kutwa kucha.
 
Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusiana na upotezaji muda unaofanywa na waajiriwa ni kwamba, wafanyakazi maofisini huwa wanapoteza saa tatu kila siku katika kufanya mambo ambayo hayana maana kwa mwajiri au kwa kazi zao.

Kwa wale ambao wan mitandao ya intenet maofisini mwao na wanaweza kuiangalia kwa kadiri wanavyopenda hutumia dakika 54 kwa siku kuangalia mitandao hiyo.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 18 kila siku kuchungulia madirishani. Hata wale ambao viti na meza zao katikati ya ofisi, huwa wanasimama na kwenda kuchungulia madirishani mara kwa mara. Kwa wastani hutumia dakika 18 kutwa.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 14 kwa kwenda kujisaidia au kwa wanawake kwenda kujipamba au kujipodoa upya bafuni au vyooni. Ile nenda rudi ya kujisaidia au kujipodoa upya huchukua wastani wa dakika 14 kila siku. Kumbuka, kuna watu hujisaidia haja kubwa hata kwa dakika kumi.

Watumishi wa maofisini yaani wale ambao hukaa ofisini, hutumia dakika 35 kila siku kupiga soga zisizohusiana na kazi na pengine zisizo na maana sana. Soga zinazohusu mpira, siasa, ufuska, majungu na umbeya mwingine hutawala.
Halafu hutumia dakika 17 katika kunywa kahawa au chai na pengine soda. Inaweza kuwa wananywea kwenye mighahawa ya kazini au pale ofisini walipo. Wengine wakati wakiwa wanakunywa kahawa au chai hawagusi kazi kabisa.

Siku hizi maofisini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuteka mawazo au akili ya watumishi. Vitu kama mitandao viriba vya chai na kahawa vya kujichotea na mengine mengi yanafanya kujikuta mtumishi ameacha kazi na kuingia katika kitu kingine.

Lakini watumishi wengi wa maofisini hasa wale ambao wanatumia muda mwingi ofisini,inadaiwa kwamba, hawafanyi mazoezi. Hii inasababisha watumishi wengi wa kazi za aina hiyo kufa au kustaafu mapema kutokana na ubovu wa afya.

ninampango wa kuacha kazi nifanye biashara kwani sioni kama nazitekeleza vilivyo mission zilizonileta hapa duniani nikiwa naendelea kumfanyia kazi boss wangu.
so i think now it is time for me to chase my destiny(ego) and employ my self.
 
Back
Top Bottom