Watumishi wa JWTZ wakatiwe Bima ya Afya

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,465
Andiko hili limechochewa na habari ya kujinyonga kwa mwanajeshi William Chacha Giriago huko Dodoma, na malalamiko ya wastaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambayo yako kila siku, kuhusu wao kukosa Bima ya Afya.

JWTZ linajinyumbulisha kuwa lina hospitali pande zote, kuweza kutoa huduma kwa watumishi wao, hivyo kwao kuwa na Bima ya Afya si muhimu. Halafu kuna tishio la kiusalama.

Ukweli, ukiacha Lugalo, vituo vyao vya afya ni duni sana. Vina wataalamu wachache wenye sifa, pia vinapungukiwa na vifaa tiba.

Ikiwa waajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania, watajiunga na Bima ya Afya, hapa ifanyayo vizuri ni NHIF, itawapa uhuru wa kutibiwa hospitali yeyote nchini Tanzania inayotoa huduma hizo. Kuwapa unafuu watumishi walioko kazini kutibu wategemezi wao kama baba na mama kwa kuwakatia bima za wategemezi ambao huwa hawapati huduma za hospitali ya jeshi bure.

Kupunguza gharama za bajeti ya matibabu zinazotengwa kwa ajili ya jeshi kila mwaka gharama ambazo zinaweza zikatumika katika maeneo mengine ndani ya jeshi (tetesi zinasema hili fungu ni moja ya sababu inayowafanya wakubwa kule jeshini wasiruhusu jeshi kujiunga na NHIF, maana hili ni fungu tamu).

Jeshi likijiunga na NHIF, hospitali ziendelee kupokea kadi za NHIF, ila uchakataji wa madai yao upewe dawati maalumu, kama lile la NHIF za TISS.

Wastaafu wengi wa NHIF wanateseka mitaani kwa kukosa matibabu bora. Hii ni hatari. Wanajeshi walioko kazini wanapata sonono ya kutibu familia zao (zilizo mbali na maeneo ya jeshi), katika hospitali bora zilizo karibu na wategemezi, na pia wanahangaika kutoa pesa za matibabu kwa wazazi wao, kwa sababu hawana Bima ya Afya, ambayo ingetibu na tegemezi.

Angalia wastaafu wa TISS, Polisi, Magereza na Uhamiaji wanavyotesa kwa kutumia kadi zao za Bima.

Serikali ilitazame hili kwa jicho makini.
 
Boss askari mdudu binadamu siyo raia usalama wake vizuri kulindwa ndio maana askari Jeshi anatakiwa kuishi kambini siyo uraiani kwaiyo ni vizuri wakaboreshewa hospital zao na waondoke uraiani wakaishi kwenye kambi ili iwe vizuri kuwa hudumia

Sasa hivi uhuru umewazidi sana wanajisahau wananaza kudai haki za kiraia kisa tunaishi nao mitazani uku wamejenga nk
 
Kuna mahali mtoa maada ameongelea kuhusu wategemezi wao hasa wazazi wanapokuwa wanaishi nao mikoa tofauti.

Hilo la kudai haki kama za raia usilizingatie Sana Mkuu. Maisha yanapokuwa magumu yanamuumiza kila mtu hivyo unakuta wanaelemewa na lawama toka Kwa ndugu mwisho wa siku mtu anajiona hafai Bora achukue maamuzi magumu Tu.
 
Una hoja nzuri. Sikuwahi kujua kua ndugu zetu wa Jeshi hawana bima ya afya.

Kiukweli bila bima kwa mtumishi ni kumuongezea stress.

Wapewe bima jamaa wawe na uhakika wa matibabu popote.
 
Mnauziwa bia nusu bei ila bima ya afya Hamna??

Anyway, kateni CHF ni elfu 30 kwa mwaka na ina-cover watu 6.
 
Wao huwa naona wana JWTZ claiming form,ndizo wanazotumia,sijajua kwa wategemezi wao.
Kiukweli yawezekana kuna ulaji flani kwa baadhi ya wakubwa,ndiyo maana hawaingizwi kwenye NHIF kama hizo claiming form zao zina mapungufu kwa wategemezi wao.Wakae chini waliangalie kwakweli.
 
Nimesha sema mara nyingi JWTZ ndiyo watawakomboa WATANZANIA na madudu ya serikali ya CCM na siyo harakati za kupiga kura maana huko tayari kuna utatu mtakatifu Kati ya Polisi,NEC na Serikali ya CCM.
Sasa Kama mpaka Askari wa JWTZ anaishi maisha ya kuungaunga baada ya kuitumikia nchi yake,hao wastaafu watarajiwa wanasubiri nini!!
 
Mchakato huo ushaanza mda sana, nadhani kwenye mwezi November up December Kila askari atakua na Bima ya afya
 
Kuna mahali mtoa maada ameongelea kuhusu wategemezi wao hasa wazazi wanapokuwa wanaishi nao mikoa tofauti.

Hilo la kudai haki kama za raia usilizingatie Sana Mkuu. Maisha yanapokuwa magumu yanamuumiza kila mtu hivyo unakuta wanaelemewa na lawama toka Kwa ndugu mwisho wa siku mtu anajiona hafai Bora achukue maamuzi magumu Tu.
Askari na familia yake wanatibiwa hospital za Jeshi kwa vitambulisho kwaiyo hata wazazi pia wanatibiwa wakowa na vitambulisho kwaiyo Jeshi liboreshe huduma zake
 
Nimesha sema mara nyingi JWTZ ndiyo watawakomboa WATANZANIA na madudu ya serikali ya CCM na siyo harakati za kupiga kura maana huko tayari kuna utatu mtakatifu Kati ya Polisi,NEC na Serikali ya CCM.
Sasa Kama mpaka Askari wa JWTZ anaishi maisha ya kuungaunga baada ya kuitumikia nchi yake,hao wastaafu watarajiwa wanasubiri nini!!
Hakuna askari wa jwtz ambaye anaishii maisha ya kuungaunga kiukweli wale jamaa wanaishi maisha mazuri mnoo kwasababu wanamishahara mikubwa na posho za kufa mtu
 
Back
Top Bottom