Hapo kwenye kukomoa hujaeleweka!
Fafanua vizuri.
Polisi walitaka kupewa taarifa ya miamala ya mteja husika, polisi walitaka pia kujiridhisha na mtiririko wa mawasiliano kati ya watuhumiwa, ambao pia ni wateja wa Airtel.
Huu ni utaratibu wa kawaida katika nyanja ya upelelezi wa makosa ya jinai Duniani kote.
Nini kosa la Airtel hapo?
Kumbuka kwamba kwao Airtel, wateja wote ni fair treated, hakuna mwenyekiti au katibu. Kwao wanafuata vigezo na masharti yaliyoko kwenye mikataba na leseni zao.
Mleta mada nakuomba utafute Documentary za "Discover ID's" zinapatikana kwenye king'amuzi cha Azam bundle la 35,000/=.
Huko utajifunza mengi kuhusu namna wenzetu hao tunaowaiga wanavyoshirikiana na makampuni ya mawasiliano kuwa trace watuhumiwa kwa kutumia mitandao ya simu na minara ya mawasiliano.
Tena wao wanakwenda mbali zaidi,saa ingine wanarekodi mawasiliano yoote ya mfuatiliwaji na kwa muda mrefu, mpaka wanapojiridhisha.
Chadema mnataka kila kila kitu muwe wajuaji.sheria nyinyi,siasa nyinyi,akifariki mwandishi habari Polisi,tayari mmerukia.
Yaani hamna agenda rasmi ambayo mnaitumia kama dira. Bali mnabaki kudandia matukio na kuongoza kamati za fitna na visasi.
Yaani team ^roho mbaya "
Mmeweka wanasheria nguli kwenye hiyo kesi ya Mwenyekiti Mbowe.
Vema muwaache wafanye kazi yao kwa uhuru mpaka mwisho wa kesi.
Hizi harakati zenu za kujifanya kupambana na huduma za kijamii huwa mnafeli kila wakati, ila sababu hamtunzi kumbukumbu ndio maana mnarudia mihemko yenu kila mara.
Nchi inao wananchi milioni sitini, chadema mnao wanachama wangapi nchi nzima ambao wako radhi kuitikia wito huu wa kijinga?
Hata kama wakiitikia kwa 15% au 100%,still haitaweza kubadili mwenendo wa kesi iliyoko mahakamani.
Lakini pia haitawadhuru Airtel kwa lolote.hii kampuni ina operate almost Afrika kote.na mmoja wa wana hisa wake ndie huwa anatoa tuzo ya mwanasiasa bora Afrika kila baada ya kipindi fulani.
Huyo ni Mo Ibrahim.
Watu mnaweza kuwa na imani ya itikadi moja ya kisiasa ndio.
Lakini hamuwezi kulingana linapokuja suala la mahitaji binafsi.
Kila mmoja anazo mbinu na shughuli zake mahsusi za kujitafutia kipato kwa kuendesha familia yake.
Hata Mbowe ni mwanasisa lakini pia ni mfanyabiashara.na kuna namna amekuwa mnufaika wa huduma za Airtel kwa kipindi kirefu.
Ndio maana alikuwa mteja wao.
Wengine mawasiliano ndio kila kitu, ukizingatia maendeleo ya teknolojia ya sasa.
Ikiwemo suala la miamala ya simu pia.
Halafu wewe mkereketwa wa siasa umwambie afunge ujasiliamali wake .
Kisa mawasiliano ya mwenyekiti yametolewa na kampuni kwa serkali kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi?
Je baadae chadema itamsaidiaje huyu mnayemshauri kususia huduma kwa maslahi ya chama chenu,kwa maslahi ya mwenyekiti Mbowe?
Mtamsaidia kujikimu kimaisha wakati akiwa ameitikia wito wenu na amesitisha uwakala wa miamala ya Airtel?
Mlifeli huko nyuma, kampeni kama hii kwa Vodacom.
Pia mkafeli kwa kampeni kama hii kwa kampuni ya kuzalisha maji ya kunywa, mkiihusisha na mheshimiwa Aeshi,kama sikosei.
Hamjifunzi kuanzia hapo?
Acheni kamati za Roho Mbaya!
#Hatutakiwahuni