Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
- Thread starter
- #41
Nadhani kila mwenye akili anajua tuna jeshi la Polisi lenye watu wahuni, wauaji, majambazi na waovu wa kila aina.Kuna uhuni gani zaidi ya kujua miamala husika ya watu waliolengwa?
Je miamala tajwa na makampuni husika,haikuwahi kufanyika?
Je namba tajwa,na shahidi wa kampuni haikuwa ya watuhumiwa wenyewe?
Je kuna uthibitisho kwa kauli yako kwamba jeshi la polisi Tanzania ni wahuni?
Acha kulazimisha watu tufuate emotions zenu,kisa tu kesi imemhusu Mbowe!
Polisi wetu wangekuwa wahuni kama unavyotamka wewe,wasingetumia weledi wao kumuokoa asipigwe na wananchi wenye hasira kali,kule Tarime alipojisahau na kuhudhuria mazishi ya aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa chadema,
Marehemu Chacha Wangwe.kwa tuhuma ambazo mpaka leo zina giza,ni kwamba imetumika funika kombe mwanaharamu apite.
Ni polisi hao hao ndio walifanya jitihada zao, na kutumia weledi wao hadi kumtorosha toka eneo la msiba na baadae kuhakikisha ameondoka kutoka Tarime kwa usalama wake.
Na tangia hapo Mbowe binafsi hajawahi kanyaga Tarime.
Tunasubiri tuone huo mshikamano wenu kugomea mtandao wa Airtel na mrudi hapa kutupatia mrejesho wenu.
Rais amekemea mara ngapi mambo ya hovyo yanayofanywa na jeshi la Polisi? Hakusema kuwa polisi wanaua mahabusu wakiwa mikononi mwao? Hakusema kuwa mara kadhaa raia wema wamepata ajali kutokana na kuwakimbia polisi waovu? Ulikuwa hujazaliwa wakati polisi walipomwua Mwangosi na binti mwanachuo? Hukuwahi kusikia polisi walipora fedha ya wafanyabiashara wa madini na kisha kuwaua wafanyabiashara? Unataka wafanye nini mpaka uweze kusema tuna polisi waovu?
Habari ya Wangwe, unazungumzia wale wahuni waliopandikizwa na CCM au kuna wengine? Hukushangaa kuwa huko huko Tarime, muda si mrefu baada ya tukio hilo, Mbowe alishiriki kwenye kampeni za uchaguzi kwaajili ya wagombea wa CHADEMA, hakuna aliyemrushia hata unyasi, na CHADEMA, pamoja na wizi wa kura uliofanywa na CCM, na matukio ya kuwashambulia wapenzi wa CHADEMA, bado CHADEMA ilishinda?
Kwani unafikiria tunagomea matumizi ya mitandao vibaraka wa uhalifu kwaajili ya kuja kutoa taarifa hapa kuwa wamepata hasara kiasi gani? Mapato yao yakipungua hata kwa milioni 50, inatosha sana kuwafikishia ujumbe, na watatafakari au kutoa huduma kwa kuzingatia ustaarabu na misingi ya biashara au kufanya biashara kwa kushikamana na watawala primitive.
Tunajua Airtel haitakufa kwa sababu tumepunguza kuitumia, lakini ujumbe utafika.