Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,505
- 41,013
Tangu kesi dhidi ya Mbowe, inayojulikana kama kesi ya mchongo au kesi kubambikia ianze, imedhihirika wazi pasipo shaka namna baadhi ya makampuni ya simu za mkononi yanavyoshirikiana na Polisi waovu dhidi ya wateja.
Mwanasheria wa kampuni ya Tigo na Airtel, wote kwa nyakati tofauti walieleza jinsi wanavyotoa taarifa za wateja hovyo, alimradi tu wameona barua yenye nembo ya jeshi la Polisi huku wakiacha kujishughulisha kabisa kulinda haki za wateja wao wala kutaka kujua taarifa za mteja zinaombwa kutokana na kosa gani. Kwao Polisi ndiyo kila kitu, wateja ni takataka.
Kutokana na ukweli huu, wateja ni lazima tulipinge hili kwa vitendo. Tufanye yafuatayo,na mengine uatakayoonekana yanafaa:
1) Sisi wenye line za Airtel, kwa vile wengi tuna lines zaidi ya moja, tusitumie line ya Airtel angalao kwa mwezi mmoja. Kama unalazimika, basi tumia pale tu ambapo huna namna nyingine.
2) Kwa uhakika mitandao karibia yote ya simu, ukiondoa Halotel na Zantel (hakuna ushahidi), siyo salama. Itumie kwa tahadhari kubwa hata kama mawasiliano yako hayana uovu wowote. Hawa jamaa hutengeneza uovu kisha wanausukumiza kwako alimradi mazingira yaruhusu. Tumia sms na calls za kawaida kwa mambo ambayo ni ya kawaida sana na yaliyo wazi. Mambo ambayo unadhani ni serious au confidential tumia whatsap, viber au skype.
Mawasiliano hata huko kwenye nchi zilizoendelea, yanakuwa monitored kwa sababu za kiusalama, lakini kwetu yanakuwa monitored kwaajili ya kuwakomoa au kuwabambikia watu kesi.