Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,994
- 3,136
Najiuliza kidogo wana JF wenzangu kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa umwagiaji wa tindikali kwa mhariri wa MwanaHalisi Bw Kubenea na mapanga kwa Bw Ndimara Tegambwage walikamatwa lini maana mara aliporejea alitoa malalamiko yake na kushangaa kwa kwa kipindi cha siku zote hizo bado watuhumiwa wake hawajakamatwa. Pili najiuliza kutoakana na majibu ya Mzee wa Kanda Maalumu Afande Tibaigana alimjibu Bw Kubenea kwamba angependa kama anawajua aiambie polisi. Hii inamaanisha nini
1. Hao hapo juu Kubenea anauhakika siyo wenyewe?
2. Kama si wenyewe kuna msaada gani kisheria kuwaachia huru au mpaka majaaliwa ya kesi yenyewe?
3. Kama Kubenea anawajua kwanini asiwataje ili kuwanusuru hao anaoona si wenyewe?????
Nawasilisha