Kikwete, Serikali ichunguzwe suala la Absalom Kibanda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, Serikali ichunguzwe suala la Absalom Kibanda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Filipo Lubua, Mar 6, 2013.

 1. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #1
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Watanzania wenzangu,

  Tumeshashughudia utekwaji wa watu kadhaa mara kwa mara. Tumeshashuhudia matukio mbalimbali ya ajabu, ambayo hata hivyo yalifanywa kwa namna ya kuwasingizia majambazi.

  Leo, tunamwona tena Mwanahabari mahiri, Absalom Kibanda, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, si ya ugonjwa, bali ya kipigo kutoka kwa watu wasiofahamika, watu waitwao majambazi.

  Hili linatokea muda wa miezi takribani minne baada ya Mnaku Mbani, Mhariri wa gazeti la Business Times kupigwa risasi mdomoni na kupoteza meno matatu.

  Hili linakuja baada ya Mwandishi mwingine wa Tanzania Daima, Shaaban Mtutu kupigwa risasi na Polisi eti akidhaniwa ni jambazi. Huyu alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake mnamo tarehe 4 Disemba, 2012, eti polisi walimdhania ni jambazi, AKIWA NYUMBANI KWAKE.

  Tukio la Kibanda, linatokea ikiwa ni miezi michache tangu Mwangosi Daudi, mwandishi wa Channel Ten kuuawa na jeshi la polisi tarehe 2 Septemba 2012.

  Hili linakuja miaka michache baada ya mapema mwaka 2008 Saed Kubenea, Mkurugenzi wa kampuni ichapayo gazeti la Mwanahalisi (ambalo nalo limefungiwa), kumwagiwa tindikali machoni pamoja na Mhariri Mshauri wa gazeti hilo Ndimara Tegambwage kucharangwa kwa mapanga.

  Linatokea miezi michache baada ya Dk. Ulimboka kutekwa na kupigwa nusu kifo, na kutupiwa msitu wa Mabwepande. Haya yote yanatokea Tanzania, na asilimia kubwa ya haya yote yamehusishwa na ujambazi.

  Huwa najiuliza, ujambazi ni nini? Kwa nini hao majambazi hawaibi chochote zaidi ya kuwajeruhi na kunuia kuwaua hawa makamanda? Kwa nini wawavamie tu watu wenye kuikosoa serikali?

  Hao majambazi kwa nini hawapatikani? Ikiwa juzi tu ameuawa kwa risasi Padre kule Zanzibar, na serikali imewaleta FBI kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo, kwa nini serikali isione haja ya kuwatumia FBI na taasisi nyingine za ukachero kutoka mataifa yaliyoendelea ili tuwapate hawa wahalifu wawavamiao wanahabari na wanaharakati wetu? Watanzania, tutanyamaza hadi lini ikiwa sauti zetu zinanyamazishwa?

  Bwana Kibanda, hadi sasa, ana kesi mahakamani. Kesi ya uchochezi baada ya gazeti la Tanzania Daima (Wakati Kibanda akiwa Mhariri) kuchapa makala iliyoandikwa na Mwandishi na Mwanaharakati Samson Mwigamba. Kesi hii ingali ikisikilizwa, leo tunasikia kuwa amevamiwa na majambazi! Kweli? Latuingia akilini kweli? Latushawishi hili kweli?

  Tanzania, serikali imetengeneza mtandao wa Kimafia (kama alivyoeleza Mh. Joseph Mbilinyi Bungeni Mwaka jana). Kumekuwa na mtandao wa kimafia unaowawinda makamanda, wanaharakati.

  Habari/tetesi zilishawekwa wazi kuwa kuna kundi la watu limeundwa, linalojishughulisha na utekaji, utesaji, na uuaji wa watu wenye ushawishi katika jamii, wanaoikosoa serikali kwa uwazi. Yamkini kundi hili ndilo lililoripotiwa kuwafuatilia Mh. John Myinka, Mh. Godbless Lema, na Mh. Dk. Wilbroad Slaa.

  Yamkini hilo ndilo kundi lililomwekea sumu Mwanaharakati mwingine Dk. Harryson Mwakyembe. Hili ndilo kundi lililoripotiwa kufuatilia maisha ya Mh. Samwel Sitta. Hili ndilo kundi, ndilo hasa!

  Kundi hili la kimafia limeamua kuwanyamazisha Watanzania, na kuiacha serikali iendelee kutuibia, kutunyonya na kutufanya mafukara.

  Kundi hili limenuia kuifanya serikali iendelee kutawala na kujinawirisha. Vigogo wa serikali na watoto wao waendelee kufurahia nchi, kwa kodi zetu wananchi.

  Kundi hili limenuia kuhakikisha viongozi waovu na wabadhirifu wa mali za umma wanaendelea kututawala kwa mabavu, kwa matisho na kwa dhuluma.

  Kwa mtindo huu, lazima tuhoji waziwazi kuwa kwa nini watu hawa hawakamatwi na kutiwa nguvuni, iwapo kweli serikali haina uhusiano nao?

  Si ndio hawa wafanyao kazi kama Ramadhani Ighondu? Hapa tusidanganyane, serikali inawafahamu watu wote wa kundi hili... Serikali inafahamu A hadi Z ya kundi hili, na yamkini serikali ndiyo iliyowapa kazi hii maalum.

  Kufunika kombe ili mwanaharamu apite, tunaiona serikali ikienda kuwajulia hali wahanga wa uonevu huu. Serikali inamtuma Makamu wa Rais kwenda kumtazama Kibanda hospitalini, Rais Kikwete pia alikwenda kumjulia hali Saed Kubenea... Yote haya ni kujaribu kutudanganya (elude) kuwa hawajui kiendeleacho..

  Serikali inafahamu kundi lake hili la kimafia. Kundi la uovu, inalifahamu vyema..

  Sasa, kwa nini serikali ifanye hivi? Kwa nini wanaharakati wateswe, wakamatwe, wauawe? Ukweli wenyewe ndio huu:

  Lengo kuu la serikali, ni kunyamazisha sauti zote zinazoikosoa bila kujali sauti hizo zinatokea wapi. Serikali inahitaji kunyamazisha sauti za watu binafsi, inahitaji kunyamazisha sauti za vikundi, vyama au jumuiya zinazoikosoa.

  Sasa kwa sababu tasnia ya habari huwafikia wengi, na kwa sababu watu wengi huamini habari za vyombo vya habari, serikali imenuia kuinyamazisha kabisa tasnia ya habari kwa kushughulika na wakosoaji wakubwa katika vyombo vya habari.

  Ndio maana hata waandishi wa makala kama hizi wanatafutiwa visa hata vya kufungwa gerezani. Mfano mzuri wa hili ni kesi ambayo inaendelea mahakamani dhidi ya Kibanda mwenyewe, na Samson Mwigamba, eti kwa sababu ya makala iliyochapwa kwenye gazeti la Tanzania Daima.

  Pengine wengi wetu mnamkumbuka Sam Shollei. Huyu alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, kabla ya Tido Mhando wa sasa.

  Huyu si Mtanzania bali ni Mkenya. Shollei aliibadilisha taswira ya gaeti la Mwananchi na kulifikisha katika taswira lililokuwa nayo sasa.

  Alifanya kazi kubwa sana. Lakini, mwisho wake alinyimwa kibali cha kuendelea kufanya kazi nchini Tanzania baada ya kibali chake cha awali kwisha muda.

  Serikali, kupitia uhamiaji, ilimnyima Shollei kibali bila kuweka bayana sababu za kufanya hivyo. Zitto Kabwe alipiga kelele kidogo kuikosoa serikali kwa swala hilo lakini kelele zake hazikufua dafu.

  Shollei, aliyelipa gazeti la Mwananchi umaarufu mkubwa na maendeleo makubwa akalazimika kuacha kazi.

  Baada ya Shollei kulazimika kuondoka Tanzania, nafasi yake ikachukuliwa na Tido Mhando. Hapa tukumbuke kuwa, Tido Mhando alifuatwa na Rais Kikwete London mwaka 2007, akiwa Mkurugenzi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, na Kikwete akamwomba aje aiongoze TBC.

  Hata hivyo naye alipoiongoza TBC na kuwa chombo cha uwazi na ukweli, na pale aliporuhusu kuonyeshwa kwa mikutano ya kampezi ya vyama vyote vya siasa katika uchaguzi Mkuu wa 2010, bila upendeleo, Tido alinyimwa mkataba mpya mwaka 2011.

  Tido, akiwa amebadilisha taswira ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), akanyimwa mkataba wa kuendelea kuiongoza. Sasa ni nani asiyejua kuwa TBC imeshapoteza ule umahiri wake ambao Tido aliisaidia kuwa nao? TBC sasa imerejea ilipotoka, imeanza kulichungulia kaburi tena...

  Baada ya Tido kunyimwa mkataba na serikali, licha ya kwamba watu wengi walilaumu sana, Tido akachukuliwa na Mwananchi, kuziba nafasi ya Shollei.

  Sasa, pengine kwa weledi wa Absalom Kibanda, kwa kazi ambayo ameifanya tangu akiwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, naye ameanza kutafutwa roho yake na hao wanaoitwa "majambazi". Majambazi wasioiba chochote, majambazi watafutao roho za wanahabari mahiri na wanaharakati.

  Nirudie tena, lengo la serikali ni kuifunga mdomo tasnia ya habari Tanzania. Lengo lake ni kuwa na vyombo vya habari kama Radio Uhuru na Gazeti la Mzalendo ambayo kazi yao ni kuitukuza serikali ya CCM hata pale pasipostahili.

  Lengo la serikali, ni kuwanyamazisha makamanda wote waonekanao kuikosoa serikali kwa uwazi. Na hili linaonekana kufanikiwa kwa kiasi fulani.. Kwani gazeti la Mwanahalisi liko wapi leo? Mwangosi yuko wapi? Kubenea anasikika tena? Je ulimboka mmemsikia tena? Wote hawa wameshanyamazishwa kwa kiasi fualani, sauti zao zimefifia.

  Watanzania wenzangu, Tanzania ya sasa si mahala salama kwa Wanahabari makini, na wanaharakati. Nawaomba na kuwasihi tuwe macho na tuamke tuungane na wenzetu hawa waliojitoa mhanga.

  Tusimameni imara kuitetea nchi yetu, haijalishi watuue sote. Kwa hakika, tusiposimama imara, nchi hii tutaitumbukiza korongoni.

  Tupazeni sauti zetu pale tuwapo na nafasi. Kwa wale tusioweza kuchapa makala kwenye magazeti mbalimbali, mitandao ya kijamii ndio silaha yetu iliyosalia.

  Tusiandike jumbe za mapenzi kwenye kuta zetu za Facebook, Tiwitter, blogu zetu. Tuandikeni jumbe za kutafuta haki na usawa nchini.

  Tuandikeni jumbe za kuikosoa serikali na kuilalamikia kila uchwao uchao. Tusiishie hapo; tuwaamsheni Watanzia wenzetu; tuwaamsheni waliolala... Tuwaelezeni kumepambazuka.... Tusipofanya hivyo, tutakapoacha kazi hii mikononi mwa wenzetu wachache, kwa hakika tutashiriki kiliangamiza taifa letu. Mwisho tutalia na kusaga meno.


  mwandishi 1.JPG Mwandishi 2.jpg View attachment 85807 Mwandishi 4.jpg Mwandishi 5.jpg

  View attachment 85805 Mwandishi 7.jpg
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  Tumeshalalamika sana na hakuna kinachofanyika zaidi ya kulindana.Tabasamu la huyu jamaa huwa halitoki moyoni.Kilichobaki waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zenu muhamasishe umma tuandamane kudai mabadiliko ya kiutawala.

  Serikali hii ni chui alievaa ngozi ya kondoo!

  Yaliyotokea Misri,Tunisia na Libya ndio silahaa pekee iliyobaki!

  Hivi kweli tuna serikali inayojali raia wake?
   
 3. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 3,134
  Likes Received: 1,608
  Trophy Points: 280
  Kwa utawala huu wa mr.dhaifu watanzania kila rangi tutaiona.
   
 4. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #4
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndiyo silaha pekee tuliyobakiwa nayo kaka. Tutumieni mitandao ya kijamii kuamshana. Tuwaamshe waliolala, nina uhakika tukiwa tumeungana, hawawezi kutushinda kamwe. The people, united, we never be defeated.
   
 5. lane

  lane JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2013
  Joined: Jan 17, 2013
  Messages: 896
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  thank you very much, its a good analytical piece of work. Kwa kweli nchi yangu pendwa ya Tanzania iko na ombwe kubwa la uongozi this time more ever.

  Kwa kifupi udhaifu wa JK.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndiyo approach ya serikali yoyote dhaifu duniani. Serikali isiyokuwa na uwezo wa kuongoza nchi hutumia jeshi na vyombo vya usalama kuwatisha wananchi ili wasiikosoe wala kuhoji utendaji wake.

  Fuatilia nchi kama vile Ethiopia na nyingine nyingi ambazo utawala umeshindwa kuongoza. Njia pekee wanayotumia ni hiyo ya kunyamazisha. Na wanaamua kutumia njia ya kuwanyamazisha na kuwatisha waandishi wa habari, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, wananchi wa kawaida watakosa mahali pa kupitishia habari zao za kuikosoa serikali, kwa kuwa wahariri wataogopa kuchapisha hizo habari.
   
 7. Crocozilla

  Crocozilla JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2013
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Thanks Lubua. Watu kama wewe wapo wachache. Nakutunuku award ya Jf best analyst wa mwezi wa 3!
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mitandao ya kijamii inaweza isisaidie sana, tunatakiwa tuende kuhamasisha wale watu waliopo vijiweni wasio na kazi na wale wananchi wa vijijini wasiokuwa na uhakika hata wa chakula. Hawa wa kwenye mitandao ya jamii wengi wao wanaandika humu wakiwa wameshiba na hata ukiwaambia kesho kuna maanandamano ni wachache sana watakaoshiriki, maana wengi wao wana kazi zao, au biashara zao ambazo zinawakeep busy.

  Na hapa ndipo ambapo hata CHADEMA inakengeuka. Utakuta viongozi wao wamejaa tele kwenye facebook wakibadilisha status zao kila kuchapo, badala ya kwenda vijijini kuwaelewesha wale wananchi wenye njaa kwamba njaa yao inatokana na CCM, na kwamba njia ya kuiepuka ni kuikataa CCM. Vivyo hivyo, tunatakiwa tuchukue hatua kama hizo iwapo tunataka kuikataa serikali.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,977
  Likes Received: 6,672
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama tunaelewa ilikofikia hii nchi!
   
 10. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2013
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  umeandika vizuri sana Lubua.
  kwa kweli nchi yetu ina viongozi wahuni! mkasa uliomfika ndugu Kibanda, jeshi la polisi haliwezi kutoa taarifa ambayo wapenda haki tutaiamini! ila haya yote yana mwisho!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. f

  frakitosho JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 13, 2012
  Messages: 802
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  You have impressed me a lot. It is such a beautful analysis. Keep it up!
   
 12. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #12
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante sana mdau. Tuko pamoja katika kulitetea taifa letu
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  @Lubua Mkuu umeongea vizuri, lakini pia ukweli utabaki pale pale kuwa Mazingira ya matukio yote uliyoyataja yamekuwa yakigubikwa na hisia mbalimbali. Nikianza na tukio la MWANGOSI, ikumbukwe kwamba huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana na mwanahabari ambaye ni mnazi mkubwa wa chama cha CHADEMA, sina sababu ya kutomtaja huyu si mwingine bali ni TUMAINI MAKENE, kama utaliangalia tukio hili kwa undani utapata picha kuwa mbali na kuaminishwa kuwa Mwangozi alikuwa katika shughuli za habari, lakini mazingira yanaonesha kuwa yawezekana alikuwa akitekeleza shughuli za chama chake cha CHADEMA, nasema hivyo kwa sababu hakuwepo yeye peke yake mwanahabari, kwa nini yeye tu ndo akumbwe na mkasa huo?

  Katika tukio la kutekwa, kuteswa na hatimaye kutelekezwa kwa ULIMBOKA, wewe unaangalia upande mmoja kuwa ni serikali ndiyo iliyolaumiwa, unasahau kuwa mengi yalisemwa katika tukio hili, wapo waliosema alitekwa na ndugu wa wagonjwa waliokuwa wakiathirika kutokana na mgomo ule, wengine wakasema aliwasaliti wenzake ambao alikuwa akifuatana nao kutafuta suluhu dhidi ya serikali, kuna waliokwenda mbali na kusema alikuwa na mahusiano na mke wa kigogo mmoja, mazingira yote haya huwezi kkuyabeza na kuusuta upande mmoja ambao ni serikali eti kwa sababu tu mnatetea chama fulani, wananchi wanaona na wanaujua ukweli. Katika tukio la ABSOM KIBANDA, hata mtoto mdogo anajua kuwa huyu bwana hakutoka Tanzania DAIMA kwa amani, na kwa maana hiyo lazima aliondoka huku akiwa anajua siri nyingi hasa ukizingatia kuwa alikuwa akiandikia gazeti la chama, unafikiri wanaimani naye na uwezo wake wa kutotoa siri zao?

  Tuache kuchonganisha serikali na wananchi katika mambo ya kudhania, wanahabari ni watu wanaoheshimika duniani kote , kuanza kukurupuka na maneno ambayo yanaweza kulitumbukiza taifa katika korongo kama ambavyo umesema siyo vizuri hata kidogo. Tuache Polisi wafanye kazi zao, Suala la kusema majambazi gani hawachukui kitu ni mawazo potofu, utambue ujambazi siyo lazima utumie nguvu hata mhanga mwenyewe anaweza kuwa jambazi na kuzulumu wenzake hata kwa njia ya kalamu na hivyo wenzake wakahitaji roho yake tu na siyo pesa kama tunavyodhania.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kama sababu ni kuchoka tu bila kuwa hoja ya msingi, maandamano ni kazi bure, tazama hao mnaowasema kuwa wameandamana wanavyojutia kufanya hivyo.

  Kama kweli kuna ushahi kuwa serikali inahusika katika haya matukio kwa nini usijitokeze hadharani na kuutoa ushahidi wako hata tunapokwenda kundamana tunajua tunachokifanya, MAJUNGU, vurugu na maandamano kwa ushahidi wa hisia na msukumo wa itikadi ni upuuzi mkubwa. Mnapotezea muda wao wa kujiletea maendeleo ili baadaye mseme maisha ya wananchi ni magumu na chanzo ni serilkali.
   
 15. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtiririko wa matukio kabla ya kutekwa na kupigwa vibaya kwa Absalom Kibanda mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri unatia shaka sana! Kwa msiokumbuka, alianza kwa kuandika makala za kuwatahadharisha vyama vya upinzani hasa wanaounda kambi rasmi ya upinzani bungeni juu ya ujio wa Abdrahaman Kinana Katibu Mkuu wa CCM,tena akayawakilisha mawazo yake hayo kupotia gazeti lao la TanzaniaDaima!
  Ikaleta maneno sana na vitisho kutoka kwa wenye chama na gazeti! Akaandika makala ya mwisho "namuogopa kinana"nayo wamiliki wa gazeti wakaja juu sana...

  Akaamua kuhama gazeti na kujiunga na magazeti ya Habari Coperation,leo sio vitisho tena bali wamemng'oa jicho na majeraha kibao!

  Nyie mmemfanya nini Kibanda wetu?
   
 16. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #16
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kamanda, hoja ya Kibanda kuondoka Tanzania Daima inahusianaje na kuvamiwa kwake? Je, nani kasema Gazeti la Tanzania Daima ni la CHADEMA? Kwa hiyo kampuni ichapayo magazeti ya Mtanzania, Dimba na Rai kwa sababu yanamilikiwa Rostam Aziz, basi magazeti haya ni ya CCM?

  Mbona wewe unatafuta mahali pa kujificha na kuitetea serikali katika maswala haya? Mwangosi akiwa na urafiki na Tumaini Makene ndo auawe? Au Tumaini Makene ni jambazi? Hata kama mwandishi akiandika habari yenye mrengo wa kusapoti chama fulani, je hilo ndu humfanya auawe au hilo lafanya mauaji yake yahalalishwe?

  Nikirejea katika hoja yako kuhusu Dk. Ulimboka, hayo mengine uliyoyasema yana uthibitisho gani zaidi ya ule wa Ramadhani Ighondu? Je namba za simu za Ighondu na mawasiliano aliyoyafanya hayathibitishi uhusika wake? Na kama kuna hoja za namna hiyo, kwa nini jeshi la polisi limekataa kumhoji Dk. Ulimboka? Kwa nini serikali imegoma kuunda tume ya kulichunguza? Daktari aliyekuwa na Dk. Ulimboka wakati anatekwa, alimtambua Ramadhani Ighondu kama mtu aliyekuwa maeneo hayo wakati huo, je huo ushahidi nao hauko wazi?

  Ndio maana nimeongelea hilo katika makala yangu kuwa, endapo kuna mambo ya namna hiyo, kwa nini serikali isitafute wataalamu kutoka FBI na CIA kuchunguza matukio haya?

  Tunapokuwa na Watanzania wa aina yako, wanaotumia mwamvuli wa wavu kujikinga na mvua, kamwe hatufiki popote!! Huwezi kujikinga na mvua kwa kutumia mwamvuli wa wavu, kamwe!
   
 17. n

  nguvukazi mikono JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2013
  Joined: Jan 1, 2013
  Messages: 490
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni UGAID,ni UKATILI uliofanywa na AL-QAIDA na washirika wao AL-SHABABU.Lazima CIA na FBI waje kuchunguza na kuwatia hatiana hawa MAGAIDI maana serikali yetu ni DHAIFU sana.DR.MCHIMBI njoo na MATAMKO yako yale ya ZANZIBAR.Chezea BUKU HARAMU wewe!
   
 18. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lubua umejitahidi sana kuandika,umenikumbusha machungu katika maisha yangu kwa kuweka picha ya mabaki ya Mwangosi! Maiti hiyo ilinifanya nimchukie Kikwete maisha yangu yote mpaka nakwenda kaburini!........!
   
 19. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2013
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana nawe kwa asilimia mia kuhusu kuhamasishana na kuchukua hatua... Kinachonisikitisha saana sio ukatili ambao serikali inaufanya bali ni jinsi watanzania tunavyo-respond hata kama tumepata taarifa zinazoonyesha kiasi cha kuridhisha kua serikali imehusika, tutaishia kuandika na kulaani...ni miaka kadhaa sasa hii mbinu inaonyesha haiwastui. tunakua kama mbu anaepiga kelele nje ya chandarua.

  Kulaani sasa basi, no more MUNGU atawahukumu, Mungu ametupa uwezo na utashi wa kujua nini kinatakiwa kufanywa na kwa wakati gani,, Wakati wa kuwazuia hawa ni sasa.. lets take a step further. Kila mmoja kwa nafasi na mahali pake a-recruit watanzania tayar kwa mapambano.. tumaini la 2015 liko mbali sana na zaid wanaweza kutuchakachua af tukawa na miaka mingine mitano au kumi ya upuuzi kama huu..

  Tangu lini tnasema MUNGU atawahukumu?imeshawah kusaidia? MUNGU katupa mti tupande tuepukane na simba mla watu tuache uvivu wa kumuomba amuue simba na badala yake tukwee mti.
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kibanda ndio yule aliyekuwa anashutumiwa na wana CHADEMA kwa kukisaliti chama chao?

  Kwani Kibanda alikuwa na kadi ya CHADEMA? Just asking
   
Loading...