Kingunge Ngombale Mwiru: Nilitofautiana na kupata matatizo na viongozi wa kanisa Katoliki, Nikaacha kwenda Kanisani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Habari wakuu,

Nmebahatika kupitia mahojiano ya Kingunge aliyoyafanya na Jichojipya kwenye mitandao. Nmejifunza Mengi na kujua mengi kumuhusu tofauti na anavyoongelewa Mtaani. Nikaona ni vyema nikushirikishe wewe unayesoma ili japo utoke na hekima za Wazee. Mungu amlaze mahali pema Peponi Amina.
kingu.jpg
Mzee kingunge (wa kwanza kulia) na mkewe, mkewe amefariki siku za karibuni. Image Credit: Nsajigwa Nsa’sam.

KINGUNGE NGOMBALE MWIRU haitaji utambulisho Tanzania, ni Mkongwe jina lake kubwa. Ni mstaafu ambaye katika maisha yake toka ujana wake amelitumikia Taifa mpaka hata ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri. Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabithiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake. Kingunge alifanya harakati akiwa karibu na Mwalimu Nyerere, na waliendelea kuwa karibu hata baada ya uhuru kwa majukumu ya kujenga Taifa changa. Kingunge alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa na nafasi nyeti katika TANU na CCM mpaka pale alipoamua kuondoka CCM wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kwenda upande wa upinzani.

Ila kwanza kabla ya kusonga mbele nakuomba chonde chonde ndugu yangu msomaji, tafadhali uiangalie makala hii KIFALSAFA zaidi na si kisiasa, usije ukaipotosha maana.

Haya…Jina lenyewe tu “Kingunge” kwa Tanzania limekuwa “nickname” likimaanisha “Kiongozi Mkongwe”. Lakini kuna upande mwingine wa Mzee Kingunge ambao Jichojipya ilifanya udadisi wa kutaka kuujua na kuuweka bayana kwa jamii. Bahati mzuri na baada ya juhudi za muda mrefu (kwani Mzee ingawa kastaafu lakini bado yupo bize (busy) kweli na shughuli zake) Jichojipya walifanikiwa kufanya naye mahojiano yaliyogeuka majadiliano mwishoni mwa Februari 2017.

Mwaka jana Mtafiti Msaidizi wa ngazi ya PhD wa Jichojipya Mwl Lucas Isakwisa alipata nafasi fupi ya kukutana na Kingunge. Alimuuliza kwani Mzee wewe ni “Mmarxisti” au “Mcommunisti” au nani..? Kwa mshangao kabisa Mzee alimjibu mimi ni “independent thinker” and a “freethinker” Mwana fikra huru (ingawa hamna mtu aliyekuwa anaelewa hiyo yamaanisha nini wakati huo na pengine hata sasa!) Kwa hivyo ngazi za juu na za wasomi walikuwa wanamdhania ni “Mmarxisti” wakati ngazi za chini kwa watu wa kawaida alikuwa anajulikana kama “Mkomunisti”. Kwa kujua hilo kuwa Mzee ni Mwanafikra huru, tuliamua kumfuatilia kuomba appointmenti naye. Tuliweza kufanikisha baada ya mwaka. Alitukaribisha Nyumbani kwake na alitueleza haya kuhusu yeye kuwa Mwana fikra huru, kitu ambacho watu hawajui hivyo kubaki kumkisia tu:-

Jichojipya tulianza kwa kumuuliza Mzee, wewe uliwezaje kuwa mwana “fikra huru”..? lakini yeye akajibu kwa kurudisha pasi swali hilohilo kwetu…kwani nyinyi mliwezaje kuwa wana fikra huru..?

Lakini akasema ngoja kuna Profesa toka Kenya aliyekuja kwenye KAVAZI, ngoja naye awepo kwenye mazungumzo haya, kwa kweli mimi nami nimefurahi sana kukutana nanyi, aliongeza..!

Baada ya Prosesa “Taji” Ahmedi Mohiddin kuja tukaanza…Nsajigwa Nsa’sam alijibu swali, nilipokuwa nakua nilikuwa najiuliza hivi mbona kuna huyu mtu, kwanza ana majina yote matatu ya kienyeji (Kingunge Ngombale Mwiru) halafu wakati anakula kiapo cha kulitumikia Taifa (kama Mbunge au Waziri yeye ni tofauti, inatangazwa laivu (live) yeye hashiki Biblia au Kuran mkononi bali tu ananyoosha mkono…ikawasha hamasa ya udadisi kujua hivi kumbe waweza kuishi maisha kama hayo na bado ukachaguliwa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa, bila kuwa Mkristo au Muislamu au kuwa na dini yoyote kabisa!? hilo lilikuwa somo tosha la uraia kwangu kuhusu kanuni za “secularism”..!

Mwl (na Mwanasheria pia) Lucas Isakwisa naye alijibu ilitokana na kusoma vitabu, hasa vya Bw Okot P’Bitek wa Uganda — “Song of lawino and okol” na pia kingine “African religions in western scholarship” ambapo alizinduka kwa maswali kuhusu dini za kigeni dhidi ya zile za asili za Africa, na uwezekano wa kuishi maisha mazuri na kamilifu bila kuwa Mkristo au Muislamu kama ambavyo Bw Okot Pbitek alivyochambua kwenye vitabu vyake hivyo.

1*ITqNwNGye3ysK-CE6WUVDA.png

Mzee kingunge Ngombale Mwiru (wa pili kushoto), Mwl Lucas Isakwisa (wa kwanza kushoto), Nsajigwa Nsa’sam (wa kwanza kulia) na mgeni toka Kenya Profesa Taji (mwenye shati nyeupe). Image Credit: Nsajigwa Nsa’sam.

Na kwa swali yamaanisha nini kusema fulani ni Mwanafikra huru, nani ni Mwana fikra huru “freethinker”..? Nsajigwa Nsa’sam alisema ni mtu ambaye anaishi akiwaza na kujiuliza maswali nje ya upeo wa dini, utamaduni, mazoea na desturi bila kuogopa au kuogopeshwa na bila upendeleo akitafuta majibu kwa kimantiki urasini (rationalism).

Hapo sasa Mkongwe Kingunge akafunguka na kuanza simulizi ya maisha yake kwa kusema;- Kwangu mimi kuwa “Mwanafikra huru” ni “evolving of ideas” — “zamadamu” ya mawazo.

Kwamba alibatizwa Mkristo wa Roman Catholic na alifuata hatua zote za utaratibu wa kanisa isipokuwa tu zile za kuwa Padri, alituambia…

Ilikuwa ni wakati wa enzi za mkoloni, mkoloni Mwingereza, sikuwepo wakati wa mkoloni Mjerumani, aliendelea…

Nilivyozidi kukua nilijikuta najiuliza sana maswali mengi mengi…juu ya dini, dhehebu la RC, najiuliza toka darasa la kwanza mpaka la kumi…

Nilipochaguliwa kwenda sekondari Tabora, akili yangu juu ya kuendelea kujiuliza maswali makubwa ikapanuka…

Niliendelea kujiuliza maswali ya msingi kuhusu dini, utatu mtakatifu…niliuliza sana na nilipata matatizo nilipokuwa nauliza maswali kuhusu masuala hayo…

Nilijiuliza kuhusu imani yangu pia…

Nikaacha kwenda kanisani…

Lakini pia nilikuwa najiuliza kuhusu ukoloni…maana kwa wakati ule, “upande mmoja unakutawala, upande mwingine unakulazeni” alisema msemo wa enzi zao Mkongwe Kingunge.

Nilitofautiana na kupata matatizo na viongozi wa kanisa katoliki…

Niliambiwa kuwa mimi ni “Mkomunisti” (tukio hilo nikiwa darasa la 6)…ilitangazwa kabisa kanisani, nilitengwa (ex-communicated) kwa tangazo la Padri mmoja mzungu raia wa Switzerland kwa jina Padri Clement…

Baba yangu alikwenda kumuona Askofu Edger Malanja ambaye alikuwa anafanya kazi na kuishi Kigurunyembe TTC Morogoro…

Askofu Edgar Malanja hakuwa na taarifa, hakujua kuwa tayari Padri Clement aliisha nitenga na kanisa (ex communicated..!)

Ilitangazwa, ilisemwa kuwa mimi nilikuwa ni Mkomunisti, ingawa kwa wakati huo mimi mwenyewe sikujua “ukomunisti” ni nini.!?

Nilitangaziwa ubaya…kuwa mimi ni mtu muovu, Mkomunisti…ndivyo ilivyotangazwa…

Mkakati wa ushawishi (Lobbying) ukafanywa kwa Mkuu wa shule ili nifukuzwe shule, yote haya yalifanywa na yule Padri Mzungu Mromani katoliki raia wa Switzerland..!

Mkuu wa shule hakukubaliana na ushawishi huo, hakuona kwanini mambo ya kanisani yaje kushawishi mambo ya elimu ya shuleni?

Zaidi pia ilikuwa kwamba, shule yetu ilikuwa muda mrefu haijatoa mwanafunzi kuendelelea zaidi na masomo ya juu…ikaonekana ikiwa mimi nitafukuzwa pengine hilo halitatokea kwani nilikuwa mwanafunzi ambaye darasani nilikuwa naendelea vizuri sana na masomo yangu, hivyo nilikuwa na uwezekano mkubwa kufaulu na kuendelea mbele zaidi…

Na kweli nilifaulu shule ya kati (middle school), na kutoka Dar es salaam nilipokuwa nasoma (ni pale ambapo sasa ni shule ya msingi ya Uhuru), nilikwenda shule ya sekondari ya Tabora.

Baada ya hapo nikajiunga na chama cha TANU kwa harakati zake za kutafuta UHURU…

1*3R-etweFB2m2Q4WDDIHyDA.png

Mzee kingunge alielezea jambo kuhusu safari ya maisha yake kifikra. Image Credit: Nsajigwa Nsa’sam.

Nilipenda sana kusoma vitabu na nilisoma vingi…baadhi ya vitabu vilipigwa marufuku, lakini hata hivyo navyo nilikuwa mdadisi kutaka kuvipata na kuvisoma…

Ni katika kusoma vitabu ndipo nilipokutana na vitabu hivi vya Bw Thomas Paine: “The Age of reason”, “The rights of man” na “Common sense”…

Huyu Tom Paine alikuwa Mwana fikra huru (Freethinker).

Tom Paine aliuliza kuhusu imani za kidini, kuhusu pia tawala za kifalme na kimalkia (monarchy), pia alitetea mapinduzi ya Ufaransa, na aliunga mkono vita vya wamarekani kuwa taifa huru, kutoka utawala wa Mwingereza…

Maandishi ya huyu bwana (Thomas Paine) yalinipeleka hatua nyingine ya juu katika kuijua dunia na jamii, alisema Mkongwe Kingunge…

Yalinipaisha upeo wangu wa kuhoji mpaka ikafikia hatua ambapo kwa mambo ya imani za dini nikaanza kuwa na mtazamo tofauti..!

Nilijiuliza kuhusu imani yenyewe, kumbuka nilikuwa najiuliza toka enzi za shule, nilihoji imani ya Kikristo, halafu imani za dini kwa ujumla wake, imani ya maisha baada ya kifo- jee ni kweli kama dini zinavyodai..? hata hilo nilijiuliza pia (Mkongwe Kingunge alikuwa katika hali ya upole wa kutafakari sana wakati anayasimulia haya).

Chama cha TANU kilinipeleka Liberia mwaka 1958 kwenda kusoma. Kwa wakati huo upeo wangu katika kuhoji na kudadisi ulikuwa wa juu sana…

Tulikwenda Liberia watatu, kule tulikutana na Dr Gay. Tulifundishwa somo maalum, somo hilo ni FALSAFA (philosophy) yenyewe!

Sisi watatu tulikwenda Liberia tukiwa tumechelewa (wengine walikwisha anza). Kwanza tulipewa questionaires — maswali mengi kila mmoja kujibu, lengo likiwa ni kutaka kujua kiwango cha uelewa cha kila mmoja kimasomo na ki — imani (na pia kuchunguza kama kuna ushawishi wa siasa za mlango wa kushoto, ukommunisti).

Ninajihesabia kuwa mtu wa bahati sana kusoma somo la FALSAFA (Mkongwe Kingunge alisema), kupitia kusoma Falsafa tulisoma vitabu vingi vya wana fikra wakubwa na mawazo yao; — Marx, Lenin nk.

1*-HuBcQHML-pUxZBwJdLTaw.png

Mzee kingunge akifurahisha wanafikra huru wenzake kwa falsafa zake. Image Credit: Nsajigwa Nsa’sam.

Tulijifunza sana, Waalimu wetu wamarekani wakitaka kutusawishi tuone ya kuwa mfumo wa ukomunisti si mzuri hata kidogo..!

Ndio…nakili falsafa ya wanafunzi wa kuhoji wa Hegel (Young Hegelians) ya kina Karl Mark ilinivutia, aliendelea…

Yule mmoja nani yule aliyesema…“si kuwa Mungu kamuumba binadamu kwa mfano wake ila ni kuwa binadamu kamfikiria mungu kwa mawazo yake”…hiyo ilinifanya nielewe alaa kumbe Miungu imeumbwa na mawazo ya binadamu..! Nsajigwa aliongezea, nadhani unamzungumzia Ludwig Feuerbach — aliyeandika kitabu kwa kijerumani ambacho tafsiri yake kwa kimombo ni “Essence of christianity” sivyo? Ahaa sawa kabisa, Mzee Kingunge akamkumbuka, ni huyo haswa..!

Huyo Ludwig Feuerbach, nilimsoma sana, nilisoma sana kitabu chake hicho…

Yeye (Ludwig Feuerbach) alinifanya mimi niwe Mwana fikra huru — Freethinker, Mzee Kingunge aliendelea…

Ninaheshimu imani za dini lakini mimi sipo (sijaji identify na ) yoyote…

Kwa imani za asili yetu, Wamatumbi wa Kilwa kusini Tanzania wanaamini na kuomba kwa “Mungu wa chini”, na “Mungu wa juu”…

Kwangu mimi hulka hii ya kudadisi na kutafuta kutaka kujua inaendelea…siyo dogma (ng’ang’anizi), na wala si dini nyingine..!

Marafiki zangu “makomredi” wao ni wafuasi wa Marx…mimi ni “Marxian”, nakubaliana na kipengelele chake cha “Historical materialism” (mgongano wa nguvu za ukinzani — na za hoja pia) kama njia ya kuiangalia / kuichambua jamii..!

Waumini wa moja kwa moja wa falsafa ya Marx wao wanakataa uwepo wa Mungu kama vile wao wana ushaidi kwa hilo…itikadi yao inageuka kuwa dini nyingine..!

Kuna wakati fulani Balozi wa Urusi ya zamani (USSR) alitutembelea pale chuo cha Kivukoni — Dar es salaam, badala ya kujibu kisayansi kwa kushuku (scepticism), yeye alijibu kama vile wao tayari wana ushaidi, alisema:- sisi Warusi tumekwenda kwenye sayari ya Mwezi (kupitia mwana sayansi wetu Yuri Gagarin ) na kule hakumkuta Mungu…jibu hilo lilinikasirisha kwani mimi nilikuwa ndiye ninayejulikana pale chuoni kuwa nilikuwa naishi bila imani ya dini yoyote…kweli hilo ndio jibu toshelezi..?

Mimi siamini lakini sina uhakika, (Agnostic) Mkongwe Kingunge akasema msimamo wake..

Ndio…“Living without religion” kuishi bila dini, maadili bila dini hayo ndiyo maisha yangu (alikiri hivyo alipokiona kitabu kinachoitwa Euphraxsophy — living without religion)…mimi sina shida na hilo, mke wangu yeye ni Mkatoliki kabisaa kwa imani yake, hamna tatizo…akaongeza.

Nilipozaliwa mimi, Kipatimu huko kilwa, wengi ni Waislamu.

Nimekulia na kusoma Dar es salaam, Pwani, wenyeji ni Wazaramo na ni waislamu pia.

Kwamba pengine kulikuwa na dalili za ubaguzi wowote wa kidini..? hapana Mzee alinena!

Nilipokwenda Tabora sekondari (katikati ya Tanzania), kule wengi wakawa wakristo…

Akijibu swali kuwa kwa kuwa yupo peke yake akiishi kwa “maadili bila dini” jee anapata wapi msaada wa faraja (consolation) pale anapokumbana na matatizo ya kimaisha ambapo wenye dini wanakwenda kupata msaada msikitini au kanisani? alisema yeye ana marafiki kwa hilo…kwa huzuni kubwa (kufiwa, kilio na mazishi) anaungana na ndugu, jamaa na marafiki…

Katika ukoo wangu wengi wetu ni waislamu lakini hakuna ubaguzi…

Sihitaji consolation (faraja) ya dini, kwani unafikiri watu wengi wanategemea makanisa au misikiti kwa hilo..? aliuliza…

Sihitaji kumbadili mtu yoyote kwenye imani yake, kuishi kwangu bila dini ni msimamo wa kifalsafa, alimaliza.

Kuhusu yeye kuwa Mwanafikra huru na ukaribu wake na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye pia alikuwa mwana mawazo mkubwa na mashuhuri (great Thinker) na pia muumini Mkatoliki safi, Kingunge alijibu kuwa Mwalimu (Nyerere) alikuwa “hodari kweli”…kwamba alikuwa na imani yake (Mkatoliki) lakini kamwe hakuendesha nchi kwa misingi ya imani yake hiyo..!

1*j1dcIvAZizeAt7i1pssGoQ.png

Mzee kingunge katika tabasamu, ameishi maisha ya Maadili bila dini. Image Credit: Nsajigwa Nsa’sam.
Mimi na yeye (Mwalimu) tulikuwa timu moja kifalsafa ingawa yeye alikuwa Mkatoliki kwa imani wakati mimi sipo kwenye imani za dini, aliongezea…

Hawamtendei haki wale wanaosema kuwa alipendelea Ukristo…akiwa kiongozi wa dola alitaifisha hata shule za Wakatoliki — jua kuwa kanisa katoliki lina nguvu za ushawishi sana — ili kila anayeweza kupata elimu iwezekanavyo na aipate, asome, vinginevyo nafasi hizo zingekuwa kwa wakatoliki tu, alichanganua….

Kuhusu swali jee walikuwepo wengine kama yeye, waliokuwa wanaishi kwa “Maadili bila dini” lakini pengine hawakujitokeza au hawakujulikana kama yeye..? jee anawajua baadhi..? hapana Mkongwe alijibu…sidhani…

Na vipi kuhusu A M Babu? Kwa maandishi yake yaelekea alikuwa mwana fikra huru (freethinker open minded) aliuliza Lucas Isakwisa…

Mkongwe Kingunge alijibu kuwa A M Babu alikuwa mwana mawazo/fikra mkubwa na mashuhuri, Mmarxist wa kweli na msomi haswa, alikuwa mwana fikra huru (independent thinker) na pia Muislamu (ikikumbushia Kwame Nkrumah aliyewahi kuandika kuhusu yeye ni nani…“Mimi ni Mkristo nisiye na dhehebu lolote, Mmarxist, Msoshalisti na sioni kama kuna ukinzani kimantiki kuwa hivyo”..!)

Juu ya maoni yake kuhusu nadharia ya “uzamadamu” ya Charles Darwin? ( theory of evolution of species) Mkongwe Kingunge anaikubali na kuongeza…kama unaikataa hiyo mbadala wake ni kukubali dhana ya uumbaji (creationism)..!

Alichanganua zaidi na kusema dhana ya uumbaji katika kitabu cha mwanzo (genesis) inakwendana na hadithi (myth) ya Waisraeli katika historia yao, na pengine ni sahihi kwao kwa dini yao inayokwendana na utamaduni wao..!

Kuhusu kusoma na kujisomea vitabu, Mkongwe alisema hiyo ni tabia ya mtu (alituulizia ikiwa vitabu vya historia vya Basil Davidson vinapatikana kwani Lucas Isakwisa alivizungumzia kwenye mazungumzo yetu).

Mkongwe alichanganua kuwa jamii yetu haihamasishi watu kujisomea vitabu wenyewe kwa udadisi binafsi…

Elimu yetu ni “bookish education” (kusoma vitabu ili kufaulu mitihani tu), alisema…

Ni kikwazo…changamoto hasa, aliendelea…

Na simu za mkononi nazo zinaharibu tabia ya kujisomea…simu ni mzuri ila matumizi yake ni tatizo kwetu…

sisi ni Malimbukeni, tunapokea tu mambo ya watu wengine, haya mambo yanavuruga sana, alimalizia…

Katika majadiliano, Mkongwe Kingunge aliposikia Galileo katajwa akasema…kanisa lilimshurutisha Galileo aikane nadharia yake (ikionyesha jinsi Mkongwe alivyo na kumbukumbu nzuri ya yaliyomkuta Mwanasayansi Galileo alipohukumiwa mbele ya viongozi wa dini)…

Na kuhusu “Hero worship” kumpenda sana mtu fulani (hasa kiongozi au mtu mashuhuri) mfano Baba wa Taifa kiasi cha kwamba ni vigumu kumkosoa hata pale alipokosea, Mzee Kingunge alisema Mwalimu Nyerere hakuwa wa kawaida, kuna wanaomhusudu (adore him, revere him) lakini alikuwa ni binadamu. Kwa Watanzania, wengi wanamuheshimu na kumthamini sana.

Mwalimu (Nyerere) alisimama kidete / alisimamia kanuni ya secularism — kutochanganya imani za dini kwenye uendeshaji wa shughuli za dola / za nchi, Mkongwe alisema.

Kumpenda shujaa (Hero worship) kunaweza kukatokea kwa sababu yupo shujaa, Mkongwe alimalizia.

Jichojipya tulitoa shukrani zetu nyingi kwa Mzee wetu, tulikaa naye kwake masaa manne tukiendelea kuchambua na kuchanganua maisha yake KIFALSAFA bila ya yeye kuonyesha kuchoka. Yalikuwa mengi ya kuzungumza na Mzee alizungumza bila break (mapunziko) ya chai au kahawa. Tulifaidika sana, kifalsafa.

Mkongwe ni mwana fikra huru Freethinker wa hali ya juu sana, (Sceptic, Agnostic, Open ended Nonbeliever), ni mwenye kutia hamasa sana kwa kizazi kipya cha wana fikra na falsafa kama yeye. Alifikiriwa kuwa ni “Mkommunisti” kabla na kanisa, na alichukuliwa hivyo na Watanzania wengi, lakini kumbe hakuwa hivyo, bali tu ni Mwanafikra huru — a lonesome Freethinker na bahati mbaya hakuna aliyejua hiyo ni nini, akiishi kwa “Maadili ya UBINADAMU bila dini”

Tulikwenda kwake na vitabu, “Consciencism” — Philosophy and ideology for decolonisation cha Kwame Nkrumah, na “Euphraxsophy” — Living without religion cha Mwana falsafa Paul Kurtz. Mkongwe alipo ona dhana/nadharia ya kitabu cha Eupraxsophy — “Living without religion” aliikubali na kusema, haswa hayo ndiyo maisha yangu miaka yote hii mpaka sasa (ambapo ana miaka themanini na…)

Kwa upande wake Mkongwe Kingunge alifurahi sana (kwa maneno yake mwenye) kukutana nasi wenye fikra kama yeye, sisi wa kizazi kingine na kuongezea kuwa ni vema sana wana fikra huru wawe wanakutana. Alifurahi, appreciated kwamba Jichojipya yaelekea tumesoma sana vitabu kama yeye, na kwamba sisi ni watafiti zaidi sio waandishi wa habari (reporters), kwa hiyo hata majadiliano tuliyofanya naye yalikuwa ya kiwango cha juu sana. Hilo hata Mgeni Profesa Mkenya Ahmedi Mohiddin “Taji” naye alikiri akisema kafurahia sana kuwa kumbe hata kwenye jamii ya leo wapo wanafikra kama sisi, naye alituelezea nadharia yake ya aliyoiita “5-R s” (somo la siku nyingine).

Jichojipya tunaona ni muhimu sana ku document — kuweka kumbukumbu sahihi za wanafikra huru wa kizazi kilichotangulia ili maisha yao yawe hamasa kwa wanafikra huru wa kizazi kipya, na hasa kwa Afrika ambapo kuishi kwa “Maadili bila dini” au nje ya dini ni Zeitgeist — upepo unaokuja na hauepukiki tena. Ulitabiriwa na waandishi kama John Mbiti, Okot PBitek, Shaaban Robert, Odera Oruka, Ali A Mazrui na pia usimamizi kidete wa kanuni ya secularism ya Mwalimu Nyerere hapa Tanzania. Wakati ukuta. Kuna watu sasa, wa umri wa uhuru na vijana wa kizazi cha sasa, wanao-hoji kila kitu, mpaka hata imani za dini. Jamii imepevuka na kufikia hapo pa Mkongwe Kingunge kifikra. Wasalaam Dar es salaam…

Credit kwa jichojipya@gmail.com
 
Asante kwa Makala hii na mahojiano haya. Viongozi wetu wengi, huondoka duniani bila kuacha maandishi yoyote. Mpaka sasa, mashuhuda wa Muungano wetu adhimu waliobaki hai ni wawili tuu, Balozi Job Luside na Hassan Nasor Moyo wa Zanzibar. Wakichomoka hawa, bila kuhojiwa kuhusu muungano na kuachwa maandishi, hakuna atakayeijua siri ya Muungano kati ya Nyerere na Karume.

Kwa sasa rais Mwinyi yu hai, Mkapa yu hai, Kikwete yu hai, natamani watokee waandishi mahiri, wafanye mahojiano ya kina na viongozi hawa kwa lengo la hifadhi ya historia kwa ajili ya Vizazi vijavyo.

Mpaka sasa, sijui ni waasisi wangapi wa Tanu bado wako hai?. Mawaziri wa baraza letu la kwanza la mawaziri, amebaki mmoja tuu, Job Lusinde. Sijui ni wangapi wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi, wangalipo hai Zaidi ya Moyo.

Wazee hawa ni hazina adimu, kima chao chapita marijani!, tuwatafute, tuzungumze nao, tutunze kumbukumbu hizi adhimu na adimu.

RIP Kingunge Ngombale Mwiru.

Paskali
 
KINGUNGE NGOMBALE MWIRU haitaji utambulisho Tanzania, ni Mkongwe jina lake kubwa. Ni mstaafu ambaye katika maisha yake toka ujana wake amelitumikia Taifa mpaka hata ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri. Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabithiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake. Kingunge alifanya harakati akiwa karibu na Mwalimu Nyerere, na waliendelea kuwa karibu hata baada ya uhuru kwa majukumu ya kujenga Taifa changa. Kingunge alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa na nafasi nyeti katika TANU na CCM mpaka pale alipoamua kuondoka CCM wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kwenda upande wa upinzani.

REKEBISHA KIDOGO HAPA MKUU, ALIPOONDOKA CCM HAKUJIUNGA NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA
 
Asante kwa Makala hii na mahojiano haya. Viongozi wetu wengi, huondoka duniani bila kuacha maandishi yoyote. Mpaka sasa, mashuhuda wa Muungano wetu adhimu waliobaki hai ni wawili tuu, Balozi Job Luside na Hassan Nasor Moyo wa Zanzibar. Wakichomoka hawa, bila kuhojiwa kuhusu muungano na kuachwa maandishi, hakuna atakayeijua siri ya Muungano kati ya Nyerere na Karume.

Kwa sasa rais Mwinyi yu hai, Mkapa yu hai, Kikwete yu hai, natamani watokee waandishi mahiri, wafanye mahojiano ya kina na viongozi hawa kwa lengo la hifadhi ya historia kwa ajili ya Vizazi vijavyo.

Mpaka sasa, sijui ni waasisi wangapi wa Tanu bado wako hai?. Mawaziri wa baraza letu la kwanza la mawaziri, amebaki mmoja tuu, Job Lusinde. Sijui ni wangapi wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi, wangalipo hai Zaidi ya Moyo.

Wazee hawa ni hazina adimu, kima chao chapita marijani!, tuwatafute, tuzungumze nao, tutunze kumbukumbu hizi adimu.

RIP Kingunge Ngombale Mwiru.

Paskali

Paskal naomba nikurekebishe!

Mzee Pius Msekwa ni mtu muhimu sana kwenye Muungano japo huwa hatajwi tajwi na bado yupo hai.
Lusinde na Nassoro Moyo walikuwa tu mawaziri wakati wa Muungano 1964 lakini huyu Msekwa Pius alikuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika na ndie kuna sahihi yake yeye na Nyerere upande wa Tanganyika!

Hata Mchakato wa kuipa Nchi yetu ya Tanganyika na Zanzibar jina la Tanzania yeye Msekwa ndio alisimamia Mchakato huo wa kuchagua jina toka kwa washindani kadhaa waliokuja na majina Pendekezwa.

Mzee Kingunge nitamkumbuka kwa mengi lakini kubwa zaid ni kuwa na msimamo katika anachokiamini kiwe sahihi au laa japo pia kuna upotoshaji kusema ana kadi namba 8.

Kwenye orodha ya wanachama wa awali 17 wa TANU wa 1954 July,7 Mzee Kingunge hayupo japo alijunga mwaka huo huo!
 
Hivi Pascal kila siku unaota kuhusu muungano. Ulishaambiwa na gavana kuwa huo ni uvamizi uliopewa jina la muungano. Tanganyika chini ya Nyerere iliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte aliyechaguliwa na wananchi na kumfunga katika magereza ya Tanganyika pamoja na mawaziri wake kabla hata huo uitwao Muungano haujafikiriwa.
 
siku hizi wanakimbilia kupata Phd lakin wanazidiwa na diploma za kina Mzee Mwinyi za 1940 kwa maarifa, busara na ujasiri na hekma!
Ni kweli mkuu..Tatizo kizazi hichi hakitaki fikra za kina na maamuzi sahihi..kwenye muda sahihi..na misimamo isiyoyumbishwa...maana fikra zilikua za muda na za kina
 
Paskal naomba nikurekebishe!

Mzee Pius Msekwa ni mtu muhimu sana kwenye Muungano japo huwa hatajwi tajwi na bado yupo hai.
Lusinde na Nassoro Moyo walikuwa tu mawaziri wakati wa Muungano 1964 lakini huyu Msekwa Pius alikuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika na ndie kuna sahihi yake yeye na Nyerere upande wa Tanganyika!

Hata Mchakato wa kuipa Nchi yetu ya Tanganyika na Zanzibar jina la Tanzania yeye Msekwa ndio alisimamia Mchakato huo wa kuchagua jina toka kwa washindani kadhaa waliokuja na majina Pendekezwa.

Mzee Kingunge nitamkumbuka kwa mengi lakini kubwa zaid ni kuwa na msimamo katika anachokiamini kiwe sahihi au laa japo pia kuna upotoshaji kusema ana kadi namba 8.

Kwenye orodha ya wanachama wa awali 17 wa TANU wa 1954 July,7 Mzee Kingunge hayupo japo alijunga mwaka huo huo!
Asante, kunikumbusha kuhusu Msekwa, huyu pia ni mtu muhimu.

Kwenye Muungano, kuna mambo mawili. Muungano ulifikiwa kwa hati za muungano, articles of union, ndipo kisha bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano.

Hii ndio picha ya kusainiwa hati za muungano, watu walioshuhudia tukio hili, walio hai mpaka sasa ni wawili tuu, Job Lusinde na Hassan Nassor Moyo.

Msekwa alihusika kwenye sharia ya muungano, acts of union.

Paskali
 
Hivi Pascal kila siku unaota kuhusu muungano. Ulishaambiwa na gavana kuwa huo ni uvamizi uliopewa jina la muungano. Tanganyika chini ya Nyerere iliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte aliyechaguliwa na wananchi na kumfunga katika magereza ya Tanganyika pamoja na mawaziri wake kabla hata huo uitwao Muungano haujafikiriwa.
Anayeota ni yule anaye kanusha kitu ambacho kipo, kina exist na kujifanya hakipo ili tuu kuji please!.

Muungano upo na una exist, uwe ni uvamizi, uliingiwa kwa halali, au kwa shinikizo, it doesn't matter much, kitu muhimu ni muungano upo na una exist!.

Muungano huu ni kama ndoa, ndoa ikiishafungwa, na kuwa consummated, ndoa hiyo ni ndoa halali na wanandoa wapo wakitimiza majukumbu ya ndoa hivyo. Hata kama mwanzo bibi Harusi alibakwa, alilazimishwa, alishurutishwa, alihadaiwa, as long as amekubali kuolewa kwa kusaini hati ya ndoa, na hadi leo bado anadumu kwenye ndoa hii, ndoa hii ni halali, na uwepo wake, unahalalisha kila kilichotokea kabla kwa kanuni ya the end justify the means!, muungano upo na utadumu milele!.

P.
 
Asante kwa Makala hii na mahojiano haya. Viongozi wetu wengi, huondoka duniani bila kuacha maandishi yoyote. Mpaka sasa, mashuhuda wa Muungano wetu adhimu waliobaki hai ni wawili tuu, Balozi Job Luside na Hassan Nasor Moyo wa Zanzibar. Wakichomoka hawa, bila kuhojiwa kuhusu muungano na kuachwa maandishi, hakuna atakayeijua siri ya Muungano kati ya Nyerere na Karume.

Kwa sasa rais Mwinyi yu hai, Mkapa yu hai, Kikwete yu hai, natamani watokee waandishi mahiri, wafanye mahojiano ya kina na viongozi hawa kwa lengo la hifadhi ya historia kwa ajili ya Vizazi vijavyo.

Mpaka sasa, sijui ni waasisi wangapi wa Tanu bado wako hai?. Mawaziri wa baraza letu la kwanza la mawaziri, amebaki mmoja tuu, Job Lusinde. Sijui ni wangapi wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi, wangalipo hai Zaidi ya Moyo.

Wazee hawa ni hazina adimu, kima chao chapita marijani!, tuwatafute, tuzungumze nao, tutunze kumbukumbu hizi adimu.

RIP Kingunge Ngombale Mwiru.

Paskali

My brother,

Take up the challenge. I believe you can do this assignment very well. Hujui tuu Lakini you also have a special place kwenye tasnia ya uandishi nchini mwetu. I remember wakati tunaingia mjini.....kipindi chako kwenye TV......kilikuwa si cha kukosa. So don't underestimate yourself. Take up the task and your fellow Tanzanians (wa leo na kesho) watakushukuru kwa hilo!)
 
Wasomi wa zamani walikuwa wanasoma sana, tofauti na wa siku hizi wanasoma kukariri.
WA sasa wanasoma ili wapate kazi na wakishapata kazi wawatawale na sio kufanya kazi...kuna tofauti kubwa Sana Kati ya manager WA zamani na manager WA Leo..wa zamani utakua nae field na atafanya kazi na wewe ILA WA sasa Ni WA instructions Tu..ndo maana mitaba inapitishwa bila kusomwa na mkuu WA kitengo anajitetea nilimwamini mtu WA chini yangu
 
Ni kweli mkuu..Tatizo kizazi hichi hakitaki fikra za kina na maamuzi sahihi..kwenye muda sahihi..na misimamo isiyoyumbishwa...maana fikra zilikua za muda na za kina
Mungu hakumuumba binadamu kwa sura na mfano wake,bali binadamu ndio humfikiria Mungu kwa mfano na sura yake ya kibinadamu!!Yaani ni sawa na wale wanaosema siku ya kwanza ukiona sindano ina ukubwa wa mkonge wa Tembo,utajua sindano zote zipo hivyo.

Kusoma Falsafa ni raha sana.Hii ndio "Ajenda" ya Kanisa Katoliki na ndio maana licha ya "madudu" yake linaendelea "kutawala" ushawishi wa dunia,sababu waumini mnahubiriwa kifalsafa mpaka mnalegea.

Ili Padre wa Kanisa Katoliki apakwe mafuta,anaingia darasani kusoma Falsafa kwa miaka mitatu,yaani muda wote huo unasoma mawazo ya watu wanaosema "dini ni upuuzi",unasoma mawazo ya watu wanaosema "Hakuna Mungu",unasoma "African Philosophy" before the coming of Westerners.Unasoma kuwa shetani ni wewe na matendo yako na wala sio kiumbe muasi.

Utasoma kuwa kilichoandikwa kwenye Biblia ni mawazo ya Wanazuoni wa Kiisraeli,na utajifunza kuwa dini ni utamaduni na hivyo kilichopo katika biblia na utamaduni wa watu waliondikwa humo.

Baadae unaingia darasani miaka minne kusoma juu ya "Theolojia".Hapa sasa ndio unajifunza juu ya Mungu.Unawasoma wanatheolojia wabobezi kama kina Thomas Acquinas.Hapa unajifunza juu ya Mungu wa Wamisionari na namna ya kumtangaza.Hapa ndio unajua sasa Martin Luther aliamua kuachana na Wataliano akaanzisha "Lutheran Church-Church of Luther" na Mfalme wa Uingereza akaanzisha "Anglican Church-Anglo-British).Ili kuondoa dhana ya Mapapa wa Kiitaliano kupitia Roman Church-Rome Italy) kuitawala dunia kwa njia ya Papacy Authority.

Ukiyajua haya,utaona kuwa Kingunge yupo sahihi sana.Kwamba hizi dini ni "usanii" mtupu,kwani "Maadili bila dini" ndio msingi wa maisha.

Wamisionary wa Mwanzo kuingia Kilwa Kipatimo walifikia kwa kina Kingunge,na Kingunge alibatizwa kwenye lile kanisa Kongwe na Kilwa Kipatimo ambalo lilikuja kupata dhoruba wakati wa vita vya Majimaji.Alibatizwa na kumbukumbu za Kitabu cha Ubatizo kinaonyeshwa alibatizwa usiku wa Mkesha wa Pasaka na aliitwa "Ambrose"
 
Back
Top Bottom