Kwann kubenea hakuchapa makala hii? Ezekiel kamwaga mwanahalisi so uwanja wa porojo wala propaganda

Jun 8, 2011
52
19
NIMEFURAHISHWA SANA NA KITENDO CHA MWANA JF KUHOJI KUHUSU KUONDOKA KWA MWANDISHI EZEKIEL KAMWAGA WA MWANAHALISI, INGAWAJE NIKO NJE YA NCHI NAOMBA NIWAONJESHE KIDOGO KUHUSU HUYU KAMWAGA ALIVYOANZA KUTUMIWA NA CCM NILIWAHI KUTUMIWA MAKALA HII NA RAFIKI YANGU AMBAYE YUKO TANZANIA ALIANDIKA MAKALA KWENDA MWANAHALISI LAKINI HAIKUCHAPWA, SASA KUBENEA ATWAMBIE KWANINI HAKUCHAPA MAKALA HII? NA EZEKIEL KAMWAGA YUPO SIMBA SASA HATUTAMWONA TENA MWANAHALISI!
Saed_Kubenea.jpg

EZEKIEL KAMWAGA MWANAHALISI SIO UWANJA WA POROJO NA PROPAGANDA

Katika gazeti la Mwanahalisi la jumatano,Machi30-Aprili5,2011 mwandishi Ezekiel Kamwaga aliandika makala yenye kichwa cha habari Msilale, CCM hawajaanza kugombana leo, nimeisoma mara tano makala hii ila nimeshindwa kuelewa iwapo makala hii kweli ilipaswa ichapwe kwenye gazeti la Mwanahalisi au Rai la Rostam Aziz?

Makala hiyo ya Ezekiel Kamwaga imetushangaza watu wengi hasa kwa jinsi ilivyoshindwa kuzama kwenye hoja za msingi kwanini CCM sasa inayumba kuliko wakati wowote katika historia ya chama hiko? Mimi nilitegemea Kamwaga atwambie kiundani je CCM ilipokumbwa na migogoro ilikuwa chini ya uwenyekiti wa nani? Chukulia mfano wa vuta nikuvute ya Nyerere na Kambona au kina Kassela Bantu, ikumbukwe kuwa wakati ule CCM ilikuwa chini ya Mwalimu Nyerere na hata ulimwengu mzima unamfahamu Nyerere ni nani katika unguli wa siasa za Afrika. Sasa Kamwaga anapodai tena kwa maneno rahisi tu kuwa kwa vile kipindi kile CCM au TANU ilipita salama basi hata awamu hii itapita salama! Hapa anatudanganya kwa maana anataka kumlinganisha Nyerere na Kikwete kiuongozi kitu aambacho hakiwezi kutuingia akilini hata kidogo.

Labda tuchukulie mfano rahisi tu utamlinganisha vipi Kikwete ambaye anadanganywa kila siku kiasi cha watu kumchakachulia mafuta ya gari na Nyerere ambaye hakutaka mzaha hata kidogo? Hapa ni dhahiri kuwa Nyerere na Kikwete hawana kinachowakutanisha kiuongozi hata kimoja kama Nyerere ni 70 basi Kikwete ni hasi (-)70 na hapa Kamwaga anapaswa kutambua kuwa uongozi huo uwe wa kitaifa au chama cha CCM.
Historia ipo wazi kuwa Kikwete hajapitia shida, hajui changamoto zozote ndio maana hata zinapoibuka hawezi kuzitatua, ndio maana kwa udhaifu wake huo ameshindwa kujipambanua yuko kwa wapinga ufisadi kina Mwakyembe na Sitta au kwa Lowassa na Rostam Aziz, huyu ndio Kikwete ambaye CCM inazidi kumfia mikononi mwake, huyu ndiyo Jakaya Kikwete aliyeshindwa kufanya kampeni kwa kutumia makada wa CCM badala yake akafannya kampeni za BMW yaani Baba, Mama na Watoto, au basi Kamwaga anataka kutuchekesha kwa kulinganisha uongozi wa Philipo Mangula na Makamba.

Lakini kuna la zaidi katika makala ile ya Ezekiel Kamwaga ambayo nathubutu kuiita ni ya kipuuzi tu kwa maana inaonyesha jinsi gani mwandishi anatoa hoja mfu ambazo hata kama kuna ufufuko siku ya mwisho basi haziwezi kufufuka, lakini mimi kama mtu mwenye uzoefu na wanahabari wa taifa hili ambao ninawafahamu vizuri halafu na uzoefu na watu wa propaganda wa CCM na michezo yao michafu huku wakijijigamba kuwa hakuna chombo cha habari Tanzania kisichokuwa na bei kwa maana kuwa wanaweza kumhonga mwandishi huyu au yule nitumie fursa hii kuweka wazi kuwa Ezekiel Kamwaga ameingia kwenye mtego huu na yeye amenaswa sasa sijui kwa shilingi ngapi? Kwa maana kwa mwandishi kijana wa aina yake nilimtegemea hata kama kweli analenga kuandika makala ya mtindo ule basi angeandika hoja za msingi kuliko kujaza kurasa za gazeti kwa manenno ya kutumwa na Yusuph Makamba au Hizza Tambwe.

Jinsi makala ya Kamwaga ilivyokuwa ya kusifia uimara wa CCM ambao kiuhalisia kwa hivi sasa haupo tena mimi nilidhani iimeandikwa na Ridhiwan Kikwete au Miraj Kikwete au hata Mama Salma Kikwete ambao wanakila sababu ya kutetea hata yale yasiyokuwepo kwavile tu CCM ndio inawapa kula si baba yao Kikwete ndio mwenyekiti? Sasa yeye Kamwaga amepewa nini mpaka afanye kazi isiyomhusu?
Nichukue fursa hii pia kumkubusha kuwa anachofanya anajiharibia mwenyewe na katu hawezi kuliharibu Mwanahalisi kama ametumwa kufanya hivyo, watanzania wanafahamu kuwa Saed Kubenea ni mtetezi wao, wanajua kuwa kina Mwangulumbi, Mbaga, Assenga na Ndimara Tegambwage ni watu makini sana. Watanzania wanakumbuka kuwa umaarufu wa Mwanahalisi haujaja kwa kujipendekeza kwa CCM bali kwa jasho na damu ya Kubenea na Tegambwage ,nani asiyekumbuka jinsi wanaharakati hawa walivyopigwa mapanga na kumwagiwa tindikali? Hivyo anapotokea mpuuzi kama Ezekiel Kamwaga ambaye ametumwa na wapuuzi fulanifulani ambao ikibidi tutawataja wanaotaka kutuharibia gazeti hili sisi ni lazima tuseme kwa maana tunajua fika kuwa bila Mwanahalisi au Raia Mwema tusingekuwa hapa tulipo, tusingekuwa na uwezo wa kumhoji Rostam au Lowassa, mchango wa magazeti haya mawili ni mkubwa sana katika kuelekea mageuzi ya kweli nchini hivyo hatuwezi kufungia macho kadudumtu yoyote anayeleta porojo na propaganda chafu kwenye gazeti hili la Mwanahalisi mtetezi wa wanyonge wa taifa hili.

Kwanza kwa taarifa yake Kamwaga asidhani kuwa hao walioumtuma huwa hawasomi Mwanahalisi, aache upuuzi kwa taarifa yake kila jumatano Salva Rweyemamu lazima anunue gazeti la Mwanahalisi na Raia Mwema na ampelekee huyo Kikwete, amini usiamini hata Ridhiwan, Miraj, Salma, Makamba, Tambwe na wabunge wote wakitoa tamko tu lazima wakimbilie kuona waandishi makini wa Mwanahalisi na Raia Mwema wameandika au kuchambua vipi hicho walichozungumza na mara nyingi wamekuwa wakibadili mienendo yao kwa kweli Mwanahalisi sio chombo cha kubeza hapa hakuna porojo kuna uchambuzi , hakuna propaganda kuna habari za kitafiti sasa iweje Ezekiel Kamwaga afanyie kazi ya Hizza Tambwe kwenye gazeti hili? Haiwezekani!

Najua kwavile huyu Ezekiel Kamwaga ameshalambishwa asali ya pesa mpya za benki kuu ataibuka harakaharaka na kunijibu lakini hii haina maana kama atashindwa kuweka bayana kwanini ameanza kuandika makala zisizofanana na Mwanahalisi au zilizo chini ya kiwango tena hali hii imejitokeza ghafla? Najua haya hawezi kujibu kwasababu anaujua ukweli, labda mimi naona kuliko kulumbana na ukweli ninaomwambia ni bora akahama Mwanahalisi kisha aende Mtanzania, Uhuru au Mzalendo huko na imani kuwa atafanya kazi yake vizuri lakini sio humu, akifanyia humu hatutamvumilia kwa maana porojo na propaganda hazitakiwi humu Mwanahalisi.

Halikadhalika labda nimpe siri moja Ezekiel Kamwaga ambayo itamsaidia kama kweli anataka kufanikiwa huko kwenye jukwaa lake jipya la CCM , kwa kawaida ukiwa bongo lala kama wewe wa kusifia tu watakudharau huko CCM hata wenyewe sikuhizi wanataka watu wenye uwezo wa kuhoji na kutoa changamoto hivyo jijengee utamaduni wa kuwa huru kimawazo ndio watakuheshimu huko CCM vinginevyo kwa jinsi upeo wako na maandiko yako yalivyo ya kishabiki bila shaka na wewe utaonekana gamba tu halafu watakuvua kwasababu huna faida kwao.
Hivi wewe Kamwaga unadhani kwa mwendo unaokwenda nao utadumu humu Mwanahalisi? Au unadhani kina Saed Kubenea watakuvumilia kupotosha umma? Bila shaka haiwezekani tayari maandishi yameshaandikwa ukutani siku zako za kukaa humu Mwanahalisi zinahesabika, na hata wakikutetea hatutakubali tutahoji na ikibidi tutajitokeza waziwazi hata kwenye TV kama umoja wa wasomaji wa Mwanahalisi na kuweka wazi kuwa HATUKUTAKI!

Fanya toba , omba msamaha anza upya vinginevyo utaangamia kwenye anga la habari za kiuchambuzi, mwishowe nitoe angalizo kuwa uchambuzi wangu umetawaliwa na hoja hivyo hata ikibidi kujibiwa iwe kwa misingi ya hoja hivohivyo lakini pia wakati ukijiandaa kujibu tuhuma hizi Bwana Ezekiel Kamwaga kumbuka kuwa hoja sio wewe kutetea CCM bali ni kwanini unafanya kazi ya Hizza Tambwe na Yusuph Makamba kwenye gazeti makini la Mwanahalisi?....Tafakari!

Mwandishi wa makala haya ni Ilunga Msekela , ni msomaji mkererketwa wa Mwanahalisi, aliwahi kusoma chuo kikuu Makerere cha nchini Uganda na ni mwanahabari katika moja ya mshirika ya kimataifa nchini ,anapatikana kwa anwani ya barua pepe; mpambanaji@live.com
 
Duh! Mkuu tunasubiri utaje majina ya hao wanaotumiwa na magambaz kuwahadaa waandishi ktk magazeti makini kama ulivyosema 'ikibidi' tuwabaini.
 
Mimi sikubahatika kulisoma mwana halisi la tarehe tajwa hapo juu,lakini inawezekana mwandishi alilenga wapinzani wasibweteke na kuona wana 100% assurance ya kifo cha ccm japo dallili za kifo hicho ziko wazi!.Badala yake waendelee kujiweka sawa zaidi kwa maana ya kutodharau nguvu ya 'Mbogo mjeruhiwa'.Kwa upande mwingine naona Kamwaga ameendelea kuandika makala ktk Mwanahalisi japo mengi yanaonekana kuibeba/kuiamsha zaidi CUF;labda kwa maana pana ya upinzani na si chama kikuu cha upinzani tu(CDM).Unless mtoa taarifa ana with hold more details,mpaka hapa cjaona kibaya
 
Kwa makala kama hii, isingekuwa busara kuitoa kwenye Mwanahalisi maana mwandishi ametumia lugha kali sana, tena kwa mwandishi wa Mwanahalisi. Kamwaga ni mwandishi mzuri sana, nitashangaa kama ameacha mwanahalisi na kwenda kuwa msemaji wa Simba, maana naona anaweza akafanya kazi zote mbili kwa wakati mmoja. Anaziweza zengwe za uongozi ambazo zipo kila siku kwenye klabu zetu hizi mbili? Kutoka kutumia kalamu kwenda kutumia mdomo?
 
mi nilipomwona Kamwaga yupo Klozi na TBC kipindi kile nikajua kwisha habari yake.........ndo wale wale kama mbunge wangu wa kigoma!
 
Binafsi mimi nilikuwa mshabiki mkubwa wa Kamwaga. Nilianza kuona dalili za uandishi wake kubadilika! Akawa anatumia muda mwingi kumwandika Lipumba na CUF Bara. Hatimaye akaibuka na makala ile. Nilipomaliza tu kuisoma nilimwandikia sms nikimwambia huyu siye yeye tunamjua! Kwa mtu anayeisoma makala ile kwa umakini atajua tu 'imepikwa' ila akisoma kwa haraka ataona kama anawatonya wapinzani. Hakuwahi kunijibu ila leo nimefarijika kuona kumbe kuna mtu aliandika makala nzima! Kamwaga alitoka Mtanzania kabla hajaanza kuandika Mwanahalisi. La msingi kujua alitokaje huko ingawa kule alikuwa akiandika sana habari za michezo. Ni msomi mzuri kielimu akiwa ni graduate wa Makerere. Kwangu mimi naweza nikasema alikwenda Mwanahalisi kwa hasira na kuanza kuandika habari za kuwananga mabosi wake wa zamani. Zilianzishwa harakati za kumpoza ikiwemo kupewa nafasi ya uchambuzi wa mpira wakati wa kombe la dunia pake TBC. Yawezekana wenzake pale Mwanahalisi walimshitukia na kuanza kum-sideline. Akashituka na kuamua kuomba kazi Simba. Anyway hayo ni maono yangu lkn najua ukweli utajulikana hivi karibuni!
 
Huitaji elimu ya chuo kikuu kubaini kwa nini hii makala haikuchapishwa. Na siamini aliyeiandika ni mwandishi wa kiwango kilichodaiwa hapa, vinginevyo ajitokeze kwa jina lake halisi kama kweli ni jasiri.

Ni malezo yenye kubanisha chuki ya mwandishi kwa Kamwaga na hakuna hoja zozote zenye mashiko zaidi ya shutuma, matusi na chuki.

Namfahamu Kamwaga na hata sababu zilizomtoa Mtanzania nazifahamu na hata mipango yake kwenda Simba niliifahamu siku chache kabla hajaondoka Mwanahalisi.

Makala iliyosababisha shutuma zote hizo niliisoma, ni makala inayompa msomaji uwanja mpana wa kujadili maudhui yake, ndio maana mmoja hapa amesema yeye alielewa kuwatahadharisha upinzani wasilewe na mafanikio waliyoyapata na kuchapa usingizi wakiamini CCM imeisha.

Hii hulka ya watu kutokubali maoni tofauti na wanavyoamini wao ndiyo iliyoifikisha CCM hapo ilipo na nawaona upinzani nao wakianza kuugua ugonjwa huo huo, wanataka kusifiwa hata pale wanapofanya madudu na sio kukosolewa.

Mtoa maoni, humfahamu Kamwaga, hivo sio ungwana kufikiri kwa niaba yake.
 
Mkuu,

Ni kweli kabisa makala hii ingekuwa vigumu kuichapisha kama ilivyo. Lakini Mhariri hakuwa na sababu za msingi za kuacha kuifuatilia. Sio kwamba yote yaliyoandikwa ni ‘rubbish’ kama inavyotaka kujengwa picha hapa. Mhariri angeweza kufanya yafuatayo pia. Kuwasiliana na mleta makala na kumwambia kwamba ajaribu kuipitia upya na kujaribu kuandika bila jazba. Mhariri angeweza kuipitia na kuihariri na baadaye kumtumia kopi mwandishi wa makala hiyo ili aipitie na kuona kama inaweza kutolewa hiyo ‘edited format’ Wewe kung’ang’ania mwandishi ajitokeze kwa jina lake halisi kungekusaidia nini? Wewe hilo hapo juu ni jina lako halisi? Ukisoma makala ile kwa makini utaelewa tu kuwa mwandishi hana chuki na Kamwaga ila alichukizwa na makala yake.

Kuna kila dalili makala ya Kamwaga haikuwafurahisha Mwanahalisi. Nitakwambia. Baada ya makala ile Kamwaga amekuwa anaandika mara chache sana. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa gazeti lile utaona kuwa Joster Mwangulubi ambaye zamani alikuwa na Makala moja kwa kila wiki sasa hivi ameongeza na anakuwa makala mbili au tatu.

Mkuu umesema kwamba unazijua sababu za Kamwaga kuondoka Mtanzania na hata za juzi kwenda Simba. Kwa nini usizitaje hapa ili kuondoa minong’ong’ono mingi inayosambaa kwenye mitandao kuhusu na huyu Bwana Mdogo.

Unaweza kuwa sahihi kabisa kuwa ile makala ya Kamwaga ilimpa msomaji uwanja wa kujadili maudhui. Mkuu kila gazeti lina ‘corporate culture’ yake. Corporate culture ya Mwanahalisi inajulikana kwa kila msomaji wake. Ile makala ya Kamwaga ilikuwa siyo yenyewe kabisa kwa Mwanahalisi bila kutafuna maneno. Ndio maana mimi baada ya kuisoma tu nilimwandikia Kamwaga kistaarabu tu kumwambia mbona vile?

Mkuu wewe umemtetea sana Kamwaga na kutuambia unamfahamu japokuwa hukutuambia unamfahamu kivipi! Rafiki yako, Kaka yako, mdogo wako, mfanyakazi mwenzio au ni wewe mwenyewe. Hivi kumfahamu mtu ndio inatosha kumwamini na kukubali kila anachofanya? Ingekuwa hivyo mbona ndoa zisingekuwa zinavunjika! Kuna wanaofahamiana zaidi ya mke na mume? Mbona bado huja kusalitiana? Kina Yuda Iskariote walifanya nini pamoja na kufahamu Kijana wa Yusufu? Kumfahamu Kamwaga haitoshi wewe kumkingia kifua kwa sababu bado anaweza akafanya kitu bila kukutaarifu hata kama wewe ni baba yake mzazi labda kama unatuambia wewe ndiye EZEKIEL KAMWAGA.

Sio kweli kabisa kwamba mtu hana budi kukubali maoni ya kitu anachoambiwa hata kama hakiamini! Mwisho wa siku utaitwa ZEZETA! Matatizo ya CCM huwezi ukayaeleza kwa mstari mmoja eti “Hii hulka ya watu kutokubali maoni tofauti na wanavyoamini wao ndiyo iliyoifikisha CCM hapo ilipo…..” Labda kama Mkuu huijui CCM! CCM ina kansa! Haitibiki kwa sasa zaidi ya kurefusha maisha yake! JK pale alipo anasema ngoja nilipelekepeleke lisije nifia mikononi! Moja ya matibabu ambayo CCM inatumia kurefusha maisha yake ni hii ya kununua waandishi ambao machoni pa watu wanaoenekana ni MAKINI! Kamwaga ni mwandishi wa ukweli! Kila anayemfahamu analijua hilo hata Magamba wanalijua hilo. Sio ajabu kabisa kwa mtu kama yeye ‘kulainishwa’ ila kwa wale ambao wanamfahamu uandishi wake akiwa Mwanahalisi walishituka kwamba makala ile haikuwa ‘corporate culture’ ya Mwanahalisi.

OMBI: Kwa sababu upo karibu na Kamwaga, mwambie akupe kopi ya makala ile uiweke kwenye thread hii ili na wengine nao waione na wachangie.
 
Hata Kubenea naye si msafi wala mahiri kama anavyoonekana. Alipandishwa chati na kutupiwa tindikali. Binafsi nilikuwa nikiandikia gazeti l a Mwanahalisi. Lakini baada ya Kubenea kuona makala zangu zinatingisha kuliko zake ambazo mara nyingi huwekwa safu ya kwanza, akaamua kunifanyia visa na visasi nikaachana naye. Hivyo msishangae Kamwaga kumwaga manyanga. Amefanya kazi na Kubenea tangia Habari Corp. Anamjua alivyo kizabazabina na mpenda sifa hata kama hana. Siandiki haya kwa kinyongo bali ukweli. Wanaokumbuka makala za Nkwazi Mhango wanajua ninachomaanisha na ndiyo maana sikuona sababu ya kutumia jina bandia wala nini. Kubenea ni wa hovyo kuliko anavyoonekana. Mwanzoni alikuwa hachapishi makala zinazozungumzia uoza wa CUF kwa sababu ajuazo mwenyewe. Baadaye alibadilika baada ya kuona CUF imegeuka nyumba ndogo ya CCM. Naye hajulikani amesimama wapi zaidi ya kutumia gazeti kusaka ulaji ingawa wengi hili hawajalibaini. Jiulize kwanini anaendelea kugharimiwa na CCM hiyo hiyo kwenda India kila mara kutibiwa kama hayuko kitandani na CCM?
 
Back
Top Bottom