Watuhumiwa wa biashara kongwe zaidi duniani waanikwa

Hamna hata jina moja la kihaya na hizo sura hamna kabisa.
Unyanyasaji wa kijinsia, ukiukwaji wa haki za binaadamu miili ni yao wenyewe, kama wameamua wafanye hivyo kwa hiari bila ya kulazimishwa na mtu sioni kama kuna kosa au aibu..

Nchi kama Uholanzi na Nchi za Scandinavia kufanya Umalata Sio kosa,.. Kosa ni kulazimishwa mtu kufanya Umalata..

Wewe mleta huu uzi una Akili ya mgando, bado uko nyuma kimawazo na fikra, sasa unataka hao wanawake waje Kukuomba kula ndio utafurahi??!
 
Hahaha kwanini wasipewe vitambulisho vya machinga?! Huo ni ujasiliamali, au wao wanaonaje?!
Ila wasichoke rais wa wanyonge akipata taarifa atawakumbuka.
Naunga mkono hoja, this is the oldest professional, na ndio ajira iliyoajiri watu wengi duniani kuliko ajira zote na inafanyika kwa namna kuu mbili.
1. The lucky ones, hawa ni wale wenye bahati, anatokea mtu ananunua jumla kwa kulipia bei ya jumla (mahari), ukiisha lipia unakuwa umenunua jumla, wafanyakazi wafanya kazi full time kwa kumuuzia bidhaa ile mteja mmoja tuu kwa bei ya jumla na hupewa majina mazuri, mke, mchumba, mpenzi, partner, etc.

2. The unlucky ones hawa hawakupata bahati ya kupata mteja mmoja wa kununua bei ya jumla, hivyo wao wanauza bei ya reja reja kwa mteja mmoja mmoja.

Nilitoa Ushauri huu


P
 
Huu sio udhalilishaji ni njia mojawapo ya kukomesha hii biashara. Hongera aliyeibua huu uozo hadharani

Binafsi naamini kuwa kati yako na hao waliowamuru washike hizo hati za mashtaka hamko salama.
Naamini ingepitiswa operartion ya haki na kila mtu akawa muwazi kusema, basi wewe na hao walioamuru mngekuwa haitiani na mgepaswa mshike hayo mabango.
Ni nani kati ya wanaowatuhumu hajawahi kufanya uhasherati au kuzini?
Tusiwahukumu bure.Waweza soma hii habari:

YOHANA 8:3-11 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”
 
Mwanamke hawezi kufanya umalaya peke yake.
Hivi kwa mfano mie niwe na wadhifa kwa mfano waziri wa Ardhi au Barabara na katika zunguka zunguka nikawa zalisha mabinti wauza baa, jee huo ni umalaya au ni bahati mbaya?
Au ndio nilikuwa natimiza agizo LA zaeni muijaze dunia?
 
Rahabu mmewahimsikia? na kamba yake nyekundu? mwisho wake nani alizaliwa toka huko? tuwaombee na kuwawezesha wabadili maisha
wafanyao na wasiofanya hii biashara hakuna mwenye uhakika wa rehema ya Mwenyezi Mungu.
Tukisema hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
 
Hili zoezi naliunga mkono.kama kuwaonyesha hivi itawafanya waogope kutenda uovu huo naafikiana na polisi.Nitatafuta zawadi niwape hao askari polisi.
Ukipeleka zawadi unapewa kesi ya hujumu uchumi, hahaha hahaha umalaya upo kila Kona ya dunia. Ilo halikwepeki
 
Huku sio Zanzibar

Polisi wanawakamata kinadada poa wanawaandikia mabango wanapiga picha wanatuma kimtandao

Huu ni udhalilishaji tena ni kinyume na katiba yetu ya mambo ya faragha

Kwa nini MTU adhalilishwe kutumia mwili wake

Kwa nini atangazwe kama jambazi

Kwa nini ni Tanzania tu ?

Je hii ni nchi ya kidini

Tusimame kupinga hiki kitendo hiki cha udhalilishaji dhidi ya wanawake wa Tanzania View attachment 1162250View attachment 1162251View attachment 1162252View attachment 1162253
Tukianza na wewe ulishindwa vipi wasitiri sura yakabaki majina!?. Huoni Kama umesaidia kuwadharirisha mkuu...?
 
Back
Top Bottom