Watu. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu. . .

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Lizzy, Mar 14, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Umewahi kuwa na mtoto mdogo <---5 sehemu ya public, akawa analia alafu watu kibao wanaopita au waliopo karibu wakaanza kukwambia anachohitaji huyo mtoto (kulala, kula, kubebwa, kucheza) bila kujua kwamba pengine ndio kaamka, kamaliza kula, alianza kulia akiwa mgongoni. .mabegani au mapajani, alikua anacheza n.k?

  Je watu wanaofanya hivyo ("jamani mbebe. . Mpakate alale huyo atakua na usingizi tu. . .huyo ni njaa huyoo ndo inayomsumbua" nk ) ndo wanakua wanajali sana watoto? Wanaona watoto wanaonewa? Wanajisikia kumwambia mtu fanya hivi au vile au inakuwaje?

  Nimeona sana hii kitu lately sema sijaweza tu kuwauliza wahusika. Yani unaweza ona mtu anainuka kabisa alipokua amekaa akamfuata mtu mwingine aliyeko na mtoto akaanza kumwambia huyo mtoto anachohitaji.

  Au yaweza kuwa hata gia ya kutongozea? Maana kuna dada last week alitoka alipokaa (kwenye kijiwe fulani hivi) akamfuata kaka aliyekua amemaliza kula sehemu hiyo na tayari yuko nje anaondoka kumwambia au sijui niseme "KUMUOMBA"(maana alikua anabembeleza) ambebe mtoto aliyekua nae wakati hata hakua analia au anasumbua abebwe.
   
 2. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ...we ukimkuta mama... mwanae akilia huoni uruma?
   
 3. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Anataka ujue kama na yeye ana katoto nyumbani.
  Miafrika ndivyo tulivyo - source : Rais wa wabeba maboksi / Mbeba maboksi pekee ambae ana permission ya kuhuzuria vikao vya UN
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Hapa sababu zaweza kuwa nyingi.

  Watoto wote mara nyingi hupendwa na watu, tena ukute mtoto mwenye mvuto wa kubebwa na watu, unakuta ukitoka naye kila mtu anataka kutoka naye wengine hatavkupiga naye picha wakati haamfahamiani. Na mara nyingi mkaka akiwa na mtoto peke yake, afu akakutana na mwanamke, moja kwa moja mwanamke ana-assume kaka hajui mambo mengi kuhusu watoto anaamua kumpa msaada.

  Pia huwa inakera kwenye public labda kanisani, mtoto analia afu mtu aliyenaye hafanyi kitu chochote. Wanavyotoa options zao ni katika kujaribu kusaidia by trial and error.
   
 5. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Unajua mtoto akilia ni ngumu sana kujua anataka nini, hata wewe uliyekuwa naye unaweza usijue exactly mtoto anachotaka. Wapita njia wanajaribu kutoa msaada tu wa ushauri, just in case............ siyo lazima kufwata wanachosema
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huruma ntaona ila siwezi kwenda mwambia "mpe nyonyo ana njaa huyo" wakati sijui mambo yao binafsi na ndio kwanza nimewaona hivyo sijui kama ni kula mara ya mwisho alikula saa ngapi, au kama ni kulala kawaida yake huwa saa ngapi n.k

  Ila TU nikiona huyo mama anahangaika naweza muuliza tatizo ni nini na kama naweza kumsaidia.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hhhmmm. . .Mbona hata hawaelekei? Au labda wanatamani ila hawana?
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa msaada wa ushauri wakati mtu HAJUI CHOCHOTE kuhusu huyo mtoto na aliyeko nae?

  @Konnie. . .
  Nimekusoma ila binafsi naamini hamna mtu anaemuelewa mtoto kama yule aliye nae. Yani kidogo kinachowezekana kuelewa/fahamu kuhusu mtoto ni yule aliyeko nae, iwe mzazi, ndugu au dada yake mlezi.Unless nae ndio mara ya kwanza kumwangalia huyo mtoto ofcourse. Kwahiyo sioni haja ya mtu ambae hata jina la huyo mtoto halijui kusema na kuonyesha anajua sana MAHITAJI na MATAKWA ya huyo mtoto.
   
 9. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ...wengine huruma inazid mpaka anajikuta katoa neno... Ilimradi tu...kujarib toa msaada.
   
 10. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hata mtu aliye na mtoto sometimes hawezi kumwelewa, ndo maana watu wanajaribu tu kutoa ushauri, na sometimes it works....... mpita njia tu anaweza kukuambia jaribu kumpa maji, ukampa na akanyamaza. mimi sioni ubaya wowote kumshauri mtu kwa mtoto anayelia
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na wale wa mtaani hua wanawaonea huruma au ni hawa wenyewe walezi wao tu?
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwanini wasiulize?

  Binafsi bado sijajiona nna huruma kwakumwambia mtu "mpe maji, mlaze, mbembeleze mwanao/huyo mtoto" unless nna uhakika kwamba ndicho anachohitaji. Na siwezi jua hilo bila ya kuuliza nikaambiwa huyo aliyenaye anafikiria nini.
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kumbe kumbeba mtoto siku hizi imekuwa ni gia ya kutongozea? Hii ni kali ya mwaka.
   
 14. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,138
  Likes Received: 947
  Trophy Points: 280
  Lizzy umenikumbusha tabia za watu. Mfano uliotoa wa mtoto kulia mi mmoja kati ya mifano mingi. Gari yangu iliharibika ghafla nikaiegesha pembeni ya barabara na nilipoanza kutoka kuchek kitu nilichokuwa na waswas nacho kwenye injini tayari kundi la watu lilikuwa limeshanizingira.Kila mmoja wao alikuwa mtaalam wa gari na alijua tatizo la gari langu."Umeweka maji ya kutosha kwenye redieta?" aliuliza mmoja. "Hiyo itakuwa fuel pump, imeziba" alitabiri mwingine. Kila mmoja alikuwa na sababu yake kwa nini gari ina matatizo.Mama mmoja nilimsikia akisema ni pancha.

  Mimi kimyaaa! Nikafungua hood na kuchungulia mahali nilipopashuku.Kumbe kweli, waya(cable) ya accelerator ilikuwa imefyatuka. Nikaiweka sawa na kuwasha gari na kuondoka. Kwenye tatizo, kila mtu anajua chanzo! Pengine ndo maana hatuendelei kwa sababu watu ni wajuaji mno!
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yeaahh. . .
  Kijana mzuri mzuri kama wewe ukibeba katoto kazuri utaona wadada watakavyokuingia na gia ya "jamani katoto kazuriiii!!" " Mama yake unemwacha wapi?" "Jamani mbona hujambeba vizuri, embu nikusaidie!!" "Jamani anafanana na wewe. . .mpaka macho." mpaka ukome mwenyewe.
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa embu ona. . .
  Wewe ndie mwenye gari na unaijua gari yako kuliko wengine,anaekuzidi labda fundi wako. Alafu all of the sudden kila mpita njia anaonyesha kuijua zaidi badala ya kukuuliza wewe 'unadhani' tatizo liko wapi na kutoa msaada kama utahitaji.
   
 17. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Swahiba umehusianisha vyema sana!...
  unatokea upande gani hapa dar???lift nayo inahusika tukiwajua watu kama nyie...LOL!
   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...kama ni mwanamke makini ataonesha juhudi za kumsaidia mwanae na walioko jirani wataelewa yule mama anaju!
  inaboa na kusababisha watu kutoa izo OPTIONS pale unapokuta mtoto analia, mama hana habari...hashtuki wala haoneshi kujali kile kinachoendelea pale (mtoto kulia)...
  watanzania pamoja na umaskini wetu, tumeumbwa na roho ya UPENDO!
   
 19. D

  DOMA JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Me mwanaume bye
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hiyo roho ya 'UPENDO' mbona hamuwaonyeshi wale wanaouhitaji kweli kama watoto wa mitaani? Wenyewe mnawaona kero. . .waliopendezeshwa na kulishwa vizuri na wazazi/walezi wao ndio mnawaonyesha upendo ambao wanapata wakutosha tayari.

  Nwy. . .swala la mtu kutulia linaweza likatokana na mtu kujua kwamba anachohitaji huyo mtoto hakipo pale na ni lazima asubirie kitu kabla hajaondoka. Mf. mtoto anaelia njaa huwezi kumbembeleza tu na "Ohhh ohhhh" anyamaze maana hiyo 'Ohhhhh ohhhhhhh' haiondoi njoo, kwahiyo mtu anachofanya ni kumaliza kinachomuweka pale alafu ndio akaridhishe hitaji/takwa la mtoto.
   
Loading...