Watu weusi hatutaacha kudharaulika kamwe

Watu weusi hatutaacha kudharaulika kamwe

respect yourself you will be respected and the vise verca
We don't respect ourselves collectively. Kama tungekuwa tunajiheshimu tungejijengea mazingira ya mazuri ya kuishi, tungepajenga nyumbani kwetu vizuri, tungeelimika vya kutosha, tungejiandalia mazingira ya kuacha kuwa ombaomba kwa nchi za nje, na tusingegawa rasilimali zetu kwa watu wa nje bila uzalendo. Lakini hatufanyi yote hayo. Kama hatuheshimu nyumbani kwetu tunapokaa simply ni kwamba hatujiheshimu. Ndio maana tunadharaulika
Unaweza kujitengenezea heshima wewe kama individual (mtu mmoja) ila collectively as Africans we have a lot to do mpaka siku tujitengenezee hiyo heshima
 
Waafrika ni walalamishi.
Wananchi wanalalamika pia viongozi wanalalamika.
Uzi wako umejaa malalamiko pasi na kuweka ufumbuzi wa changamoto zinazolikabili bara hili.
Ufumbuzi wa Afrika labda tuwape wazungu waitawale Afrika 🤣
Afrika Kuna mengi mazuri ila ujinga ujinga umezidi sana
 
Watu ambao eti uchaguzi umemalizika lakini hata kuhesabu kura na kuzitangaza kwa mujibu wa hesabu wanashindwa sasa watu wajinga kama hao ni nani atawaheshimu..!!??😛😛😛

Hata hao nyani wanao fananishwa nao hawawezi kufanya ujinga kama huo.
 
Huko kote wako CCM ila wapo kwa majina mengine. Vitendo na siasa zao ndio zile zile
Nchi za mfano barani Afrika ni Malawi, Zambia na Ghana.
Nchi hizo zinabadirisha marais na vyama vya siasa kila baada uchaguzi, lakini hakuna mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutendaji kwenye mataifa hayo.

Maendeleo kidogo tunayoweza kuyaona Afrika yapo kwenye nchi zinazotawaliwa kidikteta kama Misri, Libya, Morocco Rwanda nk.

Hivyo, hata wewe na ulalamishi wako ukipewa nafasi ya kutawala nchi yoyote nje ya CCM hakuna cha maana utakacho badirisha.

Tuendelee kujiuliza watu weusi tunakwama wapi?
 
Lengo la uzi wangu ni kuelezea kwa nini hatuheshimiki, nilipanga kuandika kuhusu hilo na nimeandika tayari. Uzi umekamilika. Nani alikuambia ukiandika mada kuhusu tatizo lazima uandike suluhisho lake hapohapo kwenye hiyo mada?

Kwa kutumia hii logic yako, basi naweza kusema hata wewe ni mlalamishi, unalalamikia uzi wangu kuwa hauna suluhisho la tatizo badala ya wewe kufikiria na kuleta suluhisho
Asichokijua hata hao wanaojaribu kuleta suluhisho wanaitwa wahaini au wachochezi....
 
Nchi za mfano barani Afrika ni Malawi, Zambia na Ghana.
Nchi hizo zinabadirisha marais na vyama vya siasa kila baada uchaguzi, lakini hakuna mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutendaji kwenye mataifa hayo.

Maendeleo kidogo tunayoweza kuyaona Afrika yapo kwenye nchi zinazotawaliwa kidikteta kama Misri, Libya, Morocco Rwanda nk.

Hivyo, hata wewe na ulalamishi wako ukipewa nafasi ya kutawala nchi yoyote nje ya CCM hakuna cha maana utakacho badirisha.

Tuendelee kujiuliza watu weusi tunakwama wapi?

Hizo nchi unazosema zina maendeleo Misri, Libya, Morocco nk. ni kuwa hujafika , Watu huko roho ziko juu , hakuna utulivu wa nafsi. Ukienda Misri hao watu wanaoomba ni hatari. Na usijambe polisi wameshafika. Watu wanaishi kama wako jela. Libya ndio hakusemeki, na Morocco vijana wanaogelea kutaka kujiingiza Spain .
Malawi, Zambia na Ghana hiyo demokrasia si imeanza juzi tu miaka yote nchi imevurugwa na vyama vyenye chapa ya CCM kama kwetu. Huku kwetu ndio usiseme humjui alosoma wala asosoma, ujinga NA WIZI ndio hausemeki wa akina kIKWETE
 
Hebu fikiria, mtu mweusi akienda Ulaya anabaguliwa, akienda Marekani anabaguliwa, akienda Japan, China, South Korea, India, Australia kila kona anadharauliwa, why?
Lakini wao wakija huku tunawaheshimu sana.

Ukweli ni kwamba sisi watu weusi hatutakuja kuheshimika kwa kulia lia tu eti watu weupe waache ubaguzi. Sisi ndio tunaopasww kuijenga hiyo heshima la sivyo tutaendelea kudharaulika na kila race hapa duniani
Wanasemaga "RESPECT IS EARNED"

Ukiangalia inventions zote za muhimu duniani zimefanywa na watu weupe. Zipo chache zilizofanywa na watu weusi ila ukiangalia watu hao ni wale walioelimika nchi za watu weupe

Nchi zote za watu weupe ni tajiri na nchi zote za watu weusi ni masikini. South Africa imejengeka vizuri vile na walioijenga ni watu weupe. Nchi tajiri Africa karibia zote sio za watu weusi (Morocco, Algeria, Egypt, Tunisia, Seychelles, Mauritius etc). Nchi hizi ukiziangalia ni tajiri kuliko nchi zote za watu weusi duniani kasoro South Africa (ambayo ilijengwa na watu weupe)

Fuatilia miji ya Morocco au Egypt, utaona ni miji misafi, ina miti mingi, imepangiliwa vizuri na ina mwonekano mzuri sana ukifananisha na miji ya nchi za watu weusi

Nchi masikini zaidi Ulaya watu wake wana maisha mazuri kuliko nchi tajiri zaidi Africa, pia nchi masikini zaidi North America ni Haiti, ambayo ni nchi ya watu weusi

Zimbabwe ilipokuwa chini ya watu weupe, Harare ndio ulikuwa mji msafi na organised zaidi Africa. Baada ya watu weusi kupewa Zimbabwe yao sasahivi Harare umekuwa mji mchafu na disorganised

Miji yetu hapa Tanzania utagundua maeneo organised (Oysterbay Dar es Salaam au Uzunguni, Mbeya) yalijengwa na watu weupe, halafu yale maeneo disorganised tumejenga sisi watu weusi

Africa imekuwa ikisumbuliwa na Malaria kwa miaka. Watu walikuwa wanakufa tu bila kujua chanzo, mpaka wazungu walipokuja ndio wakajua kinachowaua wakazi wa Africa ni malaria, na inasambazwa na mbu. Mpaka dawa za Malaria wakatengeneza watu weupe.
Sasahivi kila ugonjwa unaoanzia Africa (UKIMWI au Ebola) ni watu weupe ndio watagundua unavyosambaa, na tiba yake au namna ya kujikinga

Hapa Tanzania kila tukitaka kujenga madaraja, tunatumia makampuni ya Kichina au Korea, Uturuki nk.
Nyumba zetu tunajenga wenyewe ila ikija suala la kujenga tu ghorofa refu, tunawaita Wachina

Africa imejaaliwa resources nyingi sana. Lakini tulikuwa hatujui mpaka walipokuja watu weupe. Hata sasahivi, tayari tunajua kuwa tuna resources ila bado zinafaidisha watu weupe.
Mgodi wa Buzwagi kule Kahama, wazungu wamejichimbia dhahabu hadi sasahivi yamebaki kidogo, mgodi umefungwa bado Kahama ni masikini na haujatunufaisha ipasavyo Waafrika

Mpaka leo nchi za watu weusi mahali popote pale duniani zina matatizo common
Bado maji ni ya shida, umeme wa kusuasua, umasikini umeshamiri, watu tunazaliana kwa wingi bila mipango ya maana ya kiuchumi, viongozi mafisadi, miji michafu, ajira hakuna, viwanda vya kuhesabu, slums kila kona yani hali ni mbaya everywhere
Hata Botswana na Namibia ambazo tunasema zipo vizuri kwa hapa Africa na zenyewe bado umasikini ni mkubwa na viwanda vichache. Ni vile tu wana afadhali kuliko Waafrika wengine, ila sio kwamba wako vizuri sana

Nchi nyingi za Asia zilikuwa masikini miaka ya 1960, angalia Singapore, Qatar, South Korea na China. Leo hii zimetajirika mno. Kama kutawaliwa hata Singapore, South Korea na China zilitawaliwa na zilipoachiwa huru zilikuwa masikini kama Africa tu. Ila miaka ilivyozidi kwenda maji na mafuta yakazidi kujitenga
Nchi zao zikawa tajiri na very industrialized, sisi tumebaki masikini na hadi leo tukifanikiwa jambo dogo mno tunajipongeza hadi basi

Leo hii dunia nzima utakuta bidhaa za Wachina ( Xiaomi, Lenovo, Huawei, Hisense, BYD etc), Wakorea (Samsung, LG, nk), Wajerumani (Volkswagen), Wamarekani (Apple, Microsoft, HP, Dell), Wajapani (Sony, Play Station, Sharp Aquos, Toyota), Taiwan (Asus) nk lakini hautakuta makampuni ya Nigeria, Tanzania, Kenya, Uganda, Angola, Somalia nk

Miradi yetu mikubwa hapa Tanzania tunawapa Wachina na Waarabu waiongoze, kwamba sisi tunashindwa kuiongoza.

Sisi tuna mzaha hata na viongozi tunaowachagua. Kama kiongozi anawapa rasilimali watu wa nchi za nje bila hofu wala chembe ya uzalendo unadhani hao watu unaowapa hizo rasilimali wanakuonaje? In fact wanakuona kama zezeta ambalo halijali kuhusu nchi yake, na ndio la kulitumia kutajirisha nchi zao wao wanaojitambua.

Sisi karibia kila kitu tunaboronga. Kuanzia elimu, afya, kilimo, umeme, ajira, viwanda, usafirishaji, chakula, teknolojia, uchumi, maisha ya watu, uongozi, uchimbaji madini nk. Ni watu masikini, mafisadi, wala rushwa na tunapenda mno kujipongeza kwa achievements ndogo ambazo wenzetu walishafanikiwa miaka ya 1980s huko

Hivi hata wewe ukifikiria, kwa jinsi sisi watu weusi tulivyo nyuma kwenye kila kitu unadhani nani atatuheshimu? Ndio maana tunabaguliwa mno nchi za watu na watu wengi hawapendi black immigrants kwenye nchi zao. Sisi tunasikitisha sana.

It's painful but it's the truth. Katika human races zote duniani sisi ndio tunadhalilisha
Mkuu upo sahihi kabisa.. lkn kitu ambacho sisi waafrika wengi hatujui ni kuwa ,tuko very powerful kuliko race yoyote hapa duniani. Shida akili zetu zimeharibiwa sana.
 
Hizo nchi zenye unazosema zina maendeleo Misri, Libya, Morocco nk. ni kuwa hujafika , Watu huko roho ziko juu , hakuna utulivu wa nafsi. Ukienda Misri hao watu wanaoomba ni hatari. Na usijambe polisi wameshafika. Watu wanaishi kama wako jela. Libya ndio hakusemeki, na Morocco vijana wanaogelea kutaka kujiingiza Spain .
Hiyo ndiyo nguvu ya udikteta.
Nchi za kiarabu karibu zote ni udikteta.
Watu wanasema heri udikteta wenye maendeleo kuliko demokrasi isiyo na kitu.
Mi binafsi ni muumini wa demokrasi ya kweli hata kama inachelewesha maendeleo.
 
Sikuwahi kujua kama weusi wetu unachukuliwa kama ni laana mpaka nilipotembelea Ujerumani. 🙌

Narudi kwenye mada: Wazungu hawatudharau bure, wana sababu ya msingi.
 
Hiyo ndiyo nguvu ya udikteta.
Nchi za kiarabu karibu zote ni udikteta.
Watu wanasema heri udikteta wenye maendeleo kuliko demokrasi isiyo na kitu.
Mi binafsi ni muumini wa demokrasi ya kweli hata kama inachelewesha maendeleo.

Tatizo mfumo wetu wa kidemokrasia bado Kiongozi anakuwa hawezi kushitakiwa. Tungalifuata kama walivyofanya Singapore tungalikuwa mbali. Huko uarabuni tunakoona kuna maendelo kwa kweli maendeleo hayapo kwani almost kazi nyingi bado zinafanywa na wageni. Bado wagonjwa wao wanawapeleka India na nchi nyengine kutibiwa. Baadhi ya haki zako kama huna uwenyeji ,wenyewe wanaita ,wasta mambo yako hayaendi.

Mimi nadhani demokrasia ilianza vizuri Zanzibar mwaka 1963 lakini kwa uchoyio na ujinga wa Nyerere akaivamia chini ya msaada wa waingereza. Matokeo yake yale yote yaliyotokea Zanzibar yameikumba Tanganyika.

Bila ya kuwepo yale mavamizi ya Nyerere, Zanzibar ingalikuwa iko mbali sana kimaendeleo
 
Malawi, Zambia na Ghana hiyo demokrasia si imeanza juzi tu miaka yote nchi imevurugwa na vyama vyenye chapa ya CCM kama kwetu. Huku kwetu ndio usiseme humjui alosoma wala asosoma, ujinga NA WIZI ndio hausemeki wa akina kIKWETE
Demokrasi kwenye nchi zote za Afrika imeanza mwanzoni mwa miaka ya 90.
Nchini Zambia kwa mfano waliachana na chama kilichotawala tangu uhuru cha UNIP kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1991.

Na tangu hapo nchi hiyo imeshuhudia demokrasia ya kweli.

Maana marais sita kutoka vyama tofauti wametawala taifa hilo lenye hazina kubwa ya madini ya shaba na dhahabu.
Waafrika kwenye nchi nyingine ikiwemo Tanzania tunataka tuone namna siasa kwenye nchi hiyo zinavyoweza kumkomboa mwafrika.

Miaka 35 sasa hakuna cha maana ambacho wazambia wamenufaika nacho.
Hapo ndipo tunayoweza kusema kuwa mwafrika ni mzigo kwa binadamu wengine wa Dunia.
 
Demokrasia ni pana. Inahusisha Accountability pia. Sio tu free and fair elections
 
Mimi nadhani demokrasia ilianza vizuri Zanzibar mwaka 1963 lakini kwa uchoyio na ujinga wa Nyerere akaivamia chini ya msaada wa waingereza. Matokeo yake yale yote yaliyotokea Zanzibar yameikumba Tanganyika.
Nyerere na wenzake akina Milton Obote, Augostino Nettò, Jomo Kenyatta, Seletse Khama nk wote ni waafrika na akili zao za kiafrika.
Mwafrika ni mwafrika tu.
 
Demokrasi kwenye nchi zote za Afrika imeanza mwanzoni mwa miaka ya 90.
Nchini Zambia kwa mfano waliachana na chama kilichotawala tangu uhuru cha UNIP kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1991.

Na tangu hapo nchi hiyo imeshuhudia demokrasia ya kweli.

Maana marais sita kutoka vyama tofauti wametawala taifa hilo lenye hazina kubwa ya madini ya shaba na dhahabu.
Waafrika kwenye nchi nyingine ikiwemo Tanzania tunataka tuone namna siasa kwenye nchi hiyo zinavyoweza kumkomboa mwafrika.

Miaka 35 sasa hakuna cha maana ambacho wazambia wamenufaika nacho.
Hapo ndipo tunayoweza kusema kuwa mwafrika ni mzigo kwa binadamu wengine wa Dunia.

Halafu Kuna choyo na Roho mbaya, Huku Zanzibar Kuna watu wamekuja kutaka kufanya investments Za kujenga refinery , Tanganyika wamekataa, Huyu Bakhresa alitaka kujenga bandari, , Serikali imekataa, Kuna watu walitaka kujenga upya hosåitali ya Wete , serikali imekataa na wakajenga hospitali nje ya mji. Eti Pemba Kuna wapinzani wa CCM kwa hivyo wanawatia adabu. Yaani ujinga juu ya ujinga.
 
African continent is a fallen kingdom! Zamani waafrica ndo walikuwa wamestaraabika kuliko watu wa mabara mengine!
Chanzo cha kuwa fallen kingdom ni kutokana na sababu mbalimbali lakini sababu kuu ni kuabudu sanamu badala ya mungu wa kweli(YEREMIA 46:1-9)! Hata wamisri wa zamani walikuwa weusi tii! Sio hawa waarabu wa leo ambao kazi yao kuu ni kutafuta utajiri ulioachwa kwenye mapiramids mbalimbali! Mtu mweupe ameamua kumpumbaza mtu mweusi hadi amemtungia historia ya uongo! Eti, us africans came from primates! Yaani ni shida tu mwanawane! Ila wakati wa sisi kuwa inferior umekwisha! Ila tunacheleweshwa na mambo mengi kama waisrael walivyocheleweshwa kupewa uhuru wao sababu ya dhambi zao kwenye kitabu cha DANIEL! Ngoja niishie hapa!
 
Back
Top Bottom