Watu weusi hatutaacha kudharaulika kamwe

Watu weusi hatutaacha kudharaulika kamwe

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
Hebu fikiria, mtu mweusi akienda Ulaya anabaguliwa, akienda Marekani anabaguliwa, akienda Japan, China, South Korea, India, Australia kila kona anadharauliwa, why?
Lakini wao wakija huku tunawaheshimu sana.

Ukweli ni kwamba sisi watu weusi hatutakuja kuheshimika kwa kulia lia tu eti watu weupe waache ubaguzi. Sisi ndio tunaopasww kuijenga hiyo heshima la sivyo tutaendelea kudharaulika na kila race hapa duniani
Wanasemaga "RESPECT IS EARNED"

Ukiangalia inventions zote za muhimu duniani zimefanywa na watu weupe. Zipo chache zilizofanywa na watu weusi ila ukiangalia watu hao ni wale walioelimika nchi za watu weupe

Nchi zote za watu weupe ni tajiri na nchi zote za watu weusi ni masikini. South Africa imejengeka vizuri vile na walioijenga ni watu weupe. Nchi tajiri Africa karibia zote sio za watu weusi (Morocco, Algeria, Egypt, Tunisia, Seychelles, Mauritius etc). Nchi hizi ukiziangalia ni tajiri kuliko nchi zote za watu weusi duniani kasoro South Africa (ambayo ilijengwa na watu weupe)

Fuatilia miji ya Morocco au Egypt, utaona ni miji misafi, ina miti mingi, imepangiliwa vizuri na ina mwonekano mzuri sana ukifananisha na miji ya nchi za watu weusi

Nchi masikini zaidi Ulaya watu wake wana maisha mazuri kuliko nchi tajiri zaidi Africa, pia nchi masikini zaidi North America ni Haiti, ambayo ni nchi ya watu weusi

Zimbabwe ilipokuwa chini ya watu weupe, Harare ndio ulikuwa mji msafi na organised zaidi Africa. Baada ya watu weusi kupewa Zimbabwe yao sasahivi Harare umekuwa mji mchafu na disorganised

Miji yetu hapa Tanzania utagundua maeneo organised (Oysterbay Dar es Salaam au Uzunguni, Mbeya) yalijengwa na watu weupe, halafu yale maeneo disorganised tumejenga sisi watu weusi

Africa imekuwa ikisumbuliwa na Malaria kwa miaka. Watu walikuwa wanakufa tu bila kujua chanzo, mpaka wazungu walipokuja ndio wakajua kinachowaua wakazi wa Africa ni malaria, na inasambazwa na mbu. Mpaka dawa za Malaria wakatengeneza watu weupe.
Sasahivi kila ugonjwa unaoanzia Africa (UKIMWI au Ebola) ni watu weupe ndio watagundua unavyosambaa, na tiba yake au namna ya kujikinga

Hapa Tanzania kila tukitaka kujenga madaraja, tunatumia makampuni ya Kichina au Korea, Uturuki nk.
Nyumba zetu tunajenga wenyewe ila ikija suala la kujenga tu ghorofa refu, tunawaita Wachina

Africa imejaaliwa resources nyingi sana. Lakini tulikuwa hatujui mpaka walipokuja watu weupe. Hata sasahivi, tayari tunajua kuwa tuna resources ila bado zinafaidisha watu weupe.
Mgodi wa Buzwagi kule Kahama, wazungu wamejichimbia dhahabu hadi sasahivi yamebaki kidogo, mgodi umefungwa bado Kahama ni masikini na haujatunufaisha ipasavyo Waafrika

Mpaka leo nchi za watu weusi mahali popote pale duniani zina matatizo common
Bado maji ni ya shida, umeme wa kusuasua, umasikini umeshamiri, watu tunazaliana kwa wingi bila mipango ya maana ya kiuchumi, viongozi mafisadi, miji michafu, ajira hakuna, viwanda vya kuhesabu, slums kila kona yani hali ni mbaya everywhere
Hata Botswana na Namibia ambazo tunasema zipo vizuri kwa hapa Africa na zenyewe bado umasikini ni mkubwa na viwanda vichache. Ni vile tu wana afadhali kuliko Waafrika wengine, ila sio kwamba wako vizuri sana

Nchi nyingi za Asia zilikuwa masikini miaka ya 1960, angalia Singapore, Qatar, South Korea na China. Leo hii zimetajirika mno. Kama kutawaliwa hata Singapore, South Korea na China zilitawaliwa na zilipoachiwa huru zilikuwa masikini kama Africa tu. Ila miaka ilivyozidi kwenda maji na mafuta yakazidi kujitenga
Nchi zao zikawa tajiri na very industrialized, sisi tumebaki masikini na hadi leo tukifanikiwa jambo dogo mno tunajipongeza hadi basi

Leo hii dunia nzima utakuta bidhaa za Wachina ( Xiaomi, Lenovo, Huawei, Hisense, BYD etc), Wakorea (Samsung, LG, nk), Wajerumani (Volkswagen), Wamarekani (Apple, Microsoft, HP, Dell), Wajapani (Sony, Play Station, Sharp Aquos, Toyota), Taiwan (Asus) nk lakini hautakuta makampuni ya Nigeria, Tanzania, Kenya, Uganda, Angola, Somalia nk

Miradi yetu mikubwa hapa Tanzania tunawapa Wachina na Waarabu waiongoze, kwamba sisi tunashindwa kuiongoza.

Sisi tuna mzaha hata na viongozi tunaowachagua. Kama kiongozi anawapa rasilimali watu wa nchi za nje bila hofu wala chembe ya uzalendo unadhani hao watu unaowapa hizo rasilimali wanakuonaje? In fact wanakuona kama zezeta ambalo halijali kuhusu nchi yake, na ndio la kulitumia kutajirisha nchi zao wao wanaojitambua.

Sisi karibia kila kitu tunaboronga. Kuanzia elimu, afya, kilimo, umeme, ajira, viwanda, usafirishaji, chakula, teknolojia, uchumi, maisha ya watu, uongozi, uchimbaji madini nk. Ni watu masikini, mafisadi, wala rushwa na tunapenda mno kujipongeza kwa achievements ndogo ambazo wenzetu walishafanikiwa miaka ya 1980s huko

Hivi hata wewe ukifikiria, kwa jinsi sisi watu weusi tulivyo nyuma kwenye kila kitu unadhani nani atatuheshimu? Ndio maana tunabaguliwa mno nchi za watu na watu wengi hawapendi black immigrants kwenye nchi zao. Sisi tunasikitisha sana.

It's painful but it's the truth. Katika human races zote duniani sisi ndio tunadhalilisha
 
Kwenye hizi picha kuna mji mmoja wanaishi watu weupe na mwingine wanaishi watu weusi
Ndio utajua tofauti ya maji na mafuta
olpe_header_luftbild-1800x900 (1).jpg
stock-photo-mbeya-tanzania-drone-view-to-city-in-africa-2261608023.jpg
 
Waafrika ni walalamishi.
Wananchi wanalalamika pia viongozi wanalalamika.
Uzi wako umejaa malalamiko pasi na kuweka ufumbuzi wa changamoto zinazolikabili bara hili.
Lengo la uzi wangu ni kuelezea kwa nini hatuheshimiki, nilipanga kuandika kuhusu hilo na nimeandika tayari. Uzi umekamilika. Nani alikuambia ukiandika mada kuhusu tatizo lazima uandike suluhisho lake hapohapo kwenye hiyo mada?

Kwa kutumia hii logic yako, basi naweza kusema hata wewe ni mlalamishi, unalalamikia uzi wangu kuwa hauna suluhisho la tatizo badala ya wewe kufikiria na kuleta suluhisho
 
Hakuna watu wabaguzi kama waafrika weusi:

Mtu anakuita " wewe mtu mweusi njoo"
Wewe unakasirika, ulitaka akuite mtu mweupe?

We unatakiwa kusema tu "nakuja mtu mweupe"

Kwanza hakuna ngozi nzuri duniani kama Waafrika:
Tuna waafirka weusi kama Sudani Kusini.
Tuna waafrika Weupe kupita Wazungu;

Tuna Waafrika maji ya chungwa, damu ya mzee, brown, wekundu, wa Kaki nk.

Mzungu anaita "wewe nyani"
Unakasirika nini kama wewe sio Nyani:
Mwambie " Nakuja kwako Tumbili"
 
Umelalamika sana bila kutoa chanzo cha tatizo wala suluhisho. Classic African. Badala yake watakuja wengine kuja kuunga mstari wa malalamiko.

Wewe kama wewe, chanzo au vyanzo vya yote hayo unadhani ni nini na masuluhisho ni nini?
 
Leo nimeamua niandike chanzo cha sisi kudharaulika. Siku nyingine nitaandika suluhisho
Vipi wewe, una suluhisho lolote unalotaka kushare? Au na wewe unalalamika tu kuhusu kwa nini sijaandika suluhisho?
"Classic African" as you said

Actually nilishawahi kuandika mada kuhusu namna ya Tanzania kujiondoa kwenye umasikini lakini sikuingia deep kihivyo. Leo nimeamua niandike sababu za sisi kutoheshimika.
Kwa hiyo sometimes naandika kuhusu suluhisho ila leo nimeamua kuandika kuhusu tatizo. Kwa nini hatuheshimiki

Nimewahi kuandika kuhusu namna ya kuimprove kilimo pia.
Lakini mawazo ya mtu mmoja hayatoshi. Ningependa kupata mawazo ya watu wengine pia
 
Nilikuuliza hilo swali ili nione majibu yako alafu ndio nichangie mchango wangu.

Cha kwanza ni hakuna mtu anayembagua Mwafrika. Kubagua na kubaguliwa ni internal reaction inayotokana na self worth na class aliyojiwekea ya mtu husika kutokana na uhalisia au maneno ya kuambiwa. Kama fundamentally unajiona si chochote basi ni haki yako kubaguliwa. Kinyume cha mantiki hii ni kutokujali au kutokuona kabisa ubaguzi, especially kama unaishi ndani ya homogeneous environment.

Cha pili ni kwamba maendeleo ya kitechnolojia ni masuluhisho tu ya changamoto husika mbalimbali. Hakuna universal definition. Kibanda cha udongo na Cathedral ni matokeo yanayojitegemea na sio sign ya existence or lack of intelligence.

Cha tatu kila uvumbuzi unaouona leo duniani umetokana na asilimia 0.0001 tu ya watu wote waliopo duniani. Sio Europeans wote. Hivyo sio sawa kusema Waafrika kiujumla hatujagundua chochote, kwani Europeans 99.9% hawajandua chochote vilevile. Kilichofanya wavumbuzi wengi kutoka huko ni aina ya changamoto zao ambazo hazifanani duniani kote.

Cha nne ni kwamba maendeleo mengi yametokana na civilization, kwa maana ya mijumuiko mikubwa ya watu yenye muda mrefu, na uzoefu wa maelfu ya miaka. Kitu ambacho ni common Europe na Asia kutokana na wingi wa watu kuliko ardhi. Afrika ilikuwa na ardhi kubwa na watu wachache waliojitenga kwenye makundi madogo madogo. Kila kundi likijitegemea kivyake, lenye changamoto zake na masuluhisho yake. Hadi leo hii bado hatujafikia mjumuiko wenye ushirikiano wa kuleta mabadiliko ya kiujumla kwa kasi inayotakiwa kwenye ulimwengu huu mpya uliojaa mifumo jumuishi. Suluhisho ni muda.

Cha tano ni kwamba Afrika ilivamiwa na kuingiliwa na watu haohao unaodai wanakubagua. Waliturudisha nyuma kwa kutuharibia jumuia zetu, tamaduni zetu na mienendo yetu. Kugeuza watumwa mababu zetu, kuwatumikisha, kuwatesa na kuwasafirisha pia. Na walihakikisha vizazi vyao vinajidharau na kujiona sio kitu. Yote hayo yalitokea ndani ya miaka 70 iliyopita.

Hizo zote ni deductions za akili yangu binafsi, sio AI na wala hutozikuta popote. Na sio makaririsho wala bullet points za history books. Unachokifanya hata kwenye nyuzi zako nyingine ni kumention symptoms superficial, superficially, ambazo zipo kila sehemu. Unatakiwa kudadisi na kufikiri, sio kuona tu.

In case hujanielewa:
Summary ni madai yako yote sio sababu ya kufanya mwingine akubague, ubague au wewe ujihisi kubaguliwa. Binadamu ni kiumbe binafsi aliye juu ya vipimo vya kipuuzi na asiyeelewa au kutambua hilo anapaswa kupuuzwa.

Define yourself or be defined by someone else.
 
Sio kweli, hizo ni sababu za Africans kudharaulika. Kama tungekuwa tunafanya mambo makubwa kama Wachina watu wasingetudharau. Hapa naongelea dharau ya jumla, sio ya mtu mmoja mmoja
Pili, sijasema tunakosa intelligence. Binafsi naamini binadamu yoyote wa race yoyote anaweza kuwa genius, kilaza au mwenye akili ya kati. Sisi tunachokosa ni uthubutu, sio akili.

Pia, kama case ni kuwa colonised, vipi kuhusu mataifa ya Asia yaliyokuwa colonized na kuachwa yakiwa masikini wa kutupwa miaka ya 1960s. Mbona leo hii yamekuja kuwa mataifa makubwa na kuendelea sana?
Sisi ni wazembe, na wengi wetu hatuna uzalendo especially watu waliopo kwenye ngazi za juu ambao wao ndio wana nafasi kubwa zaidi ya kuibadilisha jamii. Lakini hatuna huo uzalendo ndio maana hatuoni umuhimu wowote wa kuendeleza nchi zetu haraka ipasavyo
Kwa sasa tulipofikia uanzishaji wa viwanda vikubwa na vya kutosha, usambazaji wa maji ya uhakika, upangiliaji wa miji yetu wenyewe, kufanya slums upgrade, kuendesha miradi yetu wenyewe nk ni vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu 100% lakini ni sisi wenyewe ndio hatuna uthubutu

Kama Burkina Faso wamezindua kiwanda cha magari ya umeme kwa msaada wa serikali yao na uchumi wao hata sio mkubwa, kwa nini nchi nyingine za watu weusi zishindwe kufanya hivyo
Kuna nchi kama South Korea au Singapore ambazo hadi kufikia miaka ya 1960 zilikuwa masikini wa kutupwa na zenye viwanda vichache
Leo hii wanatengeza simu, TV, laptops, tablets, magari na almost everything. Na kumbuka kwenye historia ya South Korea empire zake zimevamiwa mara nyingi, na wametawaliwa na Wajapani vya kutosha kutokana na kuwa taifa dhaifu. Lakini kwa nini wameweza kulijenga kwa muda mfupi taifa lao?

On other hand, Africa ilitawaliwa na wakoloni. Walipoondoka mfano hapa Tanzania walituachia viwanda vingi vya kuanza navyo hapo Tanga. Tumeshindwa kuviendeleza, vimekufa. Bongo tunatengeneza magari ya kijeshi ya Nyumbu tangu miaka ya 1990s huko, sijui kama bado tunaendelea kutengeneza ila hiyo ni sign kwamba tunaweza kuanzisha kiwanda cha magari ya kawaida au mabasi makubwa kama tukitaka. Lakini hatujaamua. Hiki ndio kinaniuma the most
Kwa nchi masikini kama Tanzania ambayo haina hela serikali ndio inapaswa kuwa mwanzilishi mkuu wa viwanda, miaka kadhaa baadae kutatokea makampuni mengi binafsi baada ya uchumi kukua

Kama ukoloni uliturudisha nyuma, haya tuna miaka 60+ bila ukoloni. Nini kinafanya tusiendelee hadi leo?
 
View attachment 3527749mtoa mada, ni vyema ukafocus na vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wako ilikuongeza tija na ufanisi.
Wewe unaongelea kwenye personal level, ulichoweka hapo kinakuwa applied kwa mtu yoyote yule sio tu Mwafrika
Sasa naongelea collective. Yani haijalishi hata kama tukasema tuache kusikiliza mawazo ya watu juu ya Waafrika, sawa. Tuanze kufocus na mambo yetu bado tu niliyoandika yanatuhusu sisi wenyewe watu weusi

Mimi natamani watu weusi tubadilike tuanze kuzijenga nchi zetu. Kuhusu kudharaulika inaweza kuwa point extra ila soma mada nzima. Binafsi inaniuma kuona Africa inashindwa kuendele kwa sababu ambazo najua zipo ndani ya uwezo wetu lakini hatutaki kuzishughulikia
 
Back
Top Bottom