Hamna kitu hio simu ni kwajili ya fashion tu... Uhondo wote upo simu za Android tabaka la juu kama Samsung, lg, nokia, sony, Google pixel, xiaomi, n.k. yani hapa iphone anafunikwa, lakini pia kuna simu za android tabaka la kawaida zilizotengenezwa kwa vifaa vya bei rahisi kama vile tecno, infinix na itel hizi huwa zinapitwa kwenye speed na camera sababu ya vifaa vyake lakini vitu vingine iphone bado yupo nyuma.
-Iphone sio simu yenye kamera nzuri kuliko simu zote kama wengi wanavyo danganywa, Kwenye zile simu za android tabaka la juu zipo mashine kama google pixel na xiaomi zinamgaragaza iphone, tatizo la wabongo wanachokosea wanalinganisha camera ya iphone na zile simu za android daraja la kawaida.
-Cable za iphone zinachaji taratibu, zina kasi ndogo ya kuhamisha mafaili na zina ubora mdogo, kampuni ya iphone walishupaza shingo mda mrefu lakini hatimae wamekubali kuanza kutengeneza simu zitazotumia usb cable za android.
-iphone haina tundu la earphones, ni mpaka uwe na earphones za kuchaji zisizo na waya, simu za android unaamua mwenyewe utumie earphones zipi kusikiliza ziwe zenye waya au wireless, unaweza tumia za waya huku unachaji zisizo na waya.
-android kuna apps na games nyingi sana kuliko iphone,
-iphone haiwezi kurekodi simu unazopiga / kupokea
-iphone inatengenezewa vifaa vyake kibao na makampuni ya simu za android.
-iphone haina apps za kutumia internet bure, kwa android kuna apps kama ha tunnel, wire tun, nic vpn na nyingine kibao watu wanazitumia kufaidi internet bure bila kununua vifurushi, kuna kipindi flan hapo mwaka jana watu waliukamua kweli kweli mtandao mwekundu, kushusha gb 20 kwa siku ilikuwa kawaida.
-iphone haina memori kadi, yani simu yako ikiungua au ikifa inaenda na mafaili, android hata simu ikipata hitilafu unabaki na kopi ya mafaili kwenye kadi.
-iphone ni ngumu kuhamisha mafaili kwenda kwa computer, mfano mrahisi simu za android ukitaka kuprint kazi stationery, unachomeka cable, unaifungua simu kwa password, unafungua file la kuprint, yani zoezi la dakika tu, kwa iphone mambo ni mengi inabidi uingize kwanza software kwenye computer ili ufungue mafaili, waweza tumia dakika 10 kumaliza zoezi dogo.
-iphone haina radio, kusikiliza radio ni mpaka uwe na data, ukienda sehemu haikamati internet ama hakuna internet huwezi sikiliza radio.
n.k,,,,
mimi nimeandika kwa uchache tu, kuna pozt ipo humu humu jamiiforums imeelezea mapungufu kibao, kama unataka kuisoma
>> minya hapa B]
iphone ni kama vile vimbwa mbwa wadogo kama yule wa wema sepetu wanauzwa milioni 3 ila ni kwajili ya mapambo tu (sijui kama wana kazi nyingine), wale mbwa hata kumtisha paka ni ngumu, ila kuna mbwa waliopitia mafunzo wanauzwa laki 8 wana miili wenye afya, wakibweka hata kama unapita nje mwili unasisimka, wana mbio, hawaumwi magonjwa hovyo hovyo, mwizi akiruka ukuta anashughulikiwa na hata kwenye urafiki ni mbwa anaekuchangamkia.