Watu wengine wanaweza kuwa na wenza wenye ukimwi bila kuambikizwa kwa muda mrefu au hata wasiambukiz

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
[h=3]WATU WENGINE WANAWEZA KUWA NA WENZA WENYE UKIMWI

BILA KUAMBIKIZWA KWA MUDA MREFU AU HATA

WASIAMBUKIZWE KABISA-TAARIFA
[/h]

Utangulizi

Neno ukimwi ni kifupisho cha maneno “Upungufu wa Kinga Mwilini”. Ugonjwa huu usabishwa na virusi ambavyo hushambulia chembe chembe za kinga na kuufanya mwili ushindwe kujilinda dhidi ya maradhi ipasavyo au hata kushindwa kupambana na maradhi yaliyoingia tayari.

Ukimwi huambukizwa kwa njia mbali mbali kama;


  1. kuingia damu ya mtu mwenye ukimwi kwa hasiye nao-hapo ndo kuna vitu kama kuchangia nyembe, sindano, kuwekewa damu isiyo salama n.k.
  2. Kujamiiana- wadudu wa ukimwi wameonekana kuwemo kwenye majimaji ya sehemu za sili, hivyo kama kuna michubuko mtu akafanya tendo hili na mhadhilika kuna nafasi ya kuambukizwa.
  3. Mama mjamzito kumuambukiza kiumbe kilichopo kwenye mfuko wakewa uzazi.

Japo si jukumu la makala hii lakini kinga ni pamoja na kuzuia kuchangia vifaa vyenye ncha kali, kutumia kinga unapofanya tendo la ndoa, kuacha kufanya tendo la ndoa kama unaweza na mengine.

Kwa vile kuna uwezekano wa kupata ukimwi kwa kutenda tendo la ndoa, wanandoa ambao kimsingi wengi wao kama si wote, hawatumii kinga wanapofanya tendo hili. Katika hali hii, kama kuna uwezekano mmoja ni muathirika, basi nafasi ya kumuambukiza mwenzake huongezeka.

Taarifa ya kwanza (case report 1)


Mwaka tisini na na sita, rafiki yangu mmoja, mtoto wake wa miezi mitatu alilazwa Muhimbili. Baada ya kuona maendeleo ya tiba si mazuri waliamua kumpima, majibu yakaonesha ana virusi vya ukimwi. Majibu haya

yalimfanya daktari aliyekuwa anamtibu mtoto kuwashauri wazazi nao wapime na wakakubali. Walipopima mama alikuwa muathirika baba hapana, na watu hawa walikuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka miwili, wakila tunda lao bila kinga.

Baada ya taarifa kufika kwa ndugu wa mwanaume wakashauri waachane wagawane walichochuma pamoja. Wakati wamepelekana mahakamani, mwanamke akakana kwamba hawakuwahi kupima. Mahakama ikaamuru

wapime, wakapima tena kwa hospitali chaguo la mwanamke. Majibu yakawa yale yale mama anao baba hana. Wakakubali kuachana na kugawana walivyochuma pamoja kama walivyoorodhesha mahakamani na baba

kupangiwa kiwango cha kumlipa mama kwa malezi ya mtoto. Baada ya mwaka na nusu mtoto akapimwa tena na kugundulika hana ukimwi tofauti na alipokuwa amepimwa mwanzoni. Mpaka hapa ninapoandika wote wapo na afya njema, baba alioa mwanamke mwingine na wana watoto wawili na mama bado yupo anaendelea kutumia dawa za ARVs.
Uchunguzi usio rasmi ulionesha kuwa mama alikuwa na ugonjwa huo kabla hata ya ndoa hiyo.

Taarifa ya pili


Jamaa yangu mmoja naye alikuwa ameoa na kujaliwa kupata watoto wanne katika ndoa yake ya miaka 15. Baadaye mwaka 2008 mke wake akaanza kuugua magonjwa ya ajabu ajabu, yanapona yanarudi na mapya

yanajitokeza. Analazwa hospitali anarudi tena baada ya muda, akaamua kwenda kwa mganga Mpemba ambaye alimwambia mumewe ana mke mwingine kamtupia jini la damu. Akampa dawa hazikusaidia. Kutokana

na lawama za mahawara kuingia na bado hospitali na kwa waganga haponi, ikashauriwa wapime HIV. Wakakubali. Walipopimwa iligundulika kuwa mama anao na baba hana. Mama akazidi kuamini kuwa hata kama ameonekana ana Ukimwi basi atakuwa ametumiwa na huyo hawara wa mumewe. Ikawa kazi kumeza dawa,

anameza na kuacha anakwenda kwa waganga wake, mara ya mwisho akaamua kuokoka sasa japo hapo kichwa nacho kilishaanza kuvurugika. Huko ndo kabisa akaambiwa aache dawa kabisa YESU atamponya. Mwanzoni mwa mwaka huu tumemzika.
Ninazo taarifa za namna hii nne lakini mbili zinatosha kutoa mjadala.

Mjadala


Katika taarifa zote mbili inaonyesha wahusika wote walishakaa pamoja wakila matunda yao bila kinga ndo maana wakapata watoto. Kwanini hawakuambukizana inawezekana walikuwa wanakula tunda lao bila

michubuko yeyote katika kipindi chote walichokuwa pamoja. Sababu nyingine yawezekana wanaume hao wana kinga dhidi ya virusi vya ukimwi au chembe chembe zao za kinga hazina vipokezi (receptors) vya wadudu wa

ukimwi. Tafiti zimeonyesha virusi wa ukimwi huweza kuingia kwenye chembe chembe za kinga kupitia vipokezi katika hali ya kama ufunguo na kitasa au au nati na boriti. Kama mtu hana vipokezi hivi hawezi kuambukizwa.

Dr Matthew Dolan, daktari bingwa katika jeshi la anga la marekani anasema, anasema "Genetic resistance to AIDS works in different ways and appears in different ethnic groups. The most powerful form of resistance, caused

by a genetic defect, is limited to people with European or Central Asian heritage. An estimated 1 percent of people descended from Northern Europeans are virtually immune to AIDS infection, with Swedes the most likely to be

protected. One
theorysuggests that the mutation developed in Scandinavia and moved southward with Viking raiders.

All those with the highest level of HIV immunity share a pair of mutated genes -- one in each chromosome -- that prevent their immune cells from developing a "receptor" that lets the AIDS virus break in. If the so-called CCR5 receptor -- which scientists say is akin to a lock -- isn't there, the virus can't break into the cell and take it over. (haya yamenizengua kuyatafsiri)


Mtoto kuonekana ana ukimwi akiwa na miezi miatu na baada ya mwaka mmoja na nusu hana hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto anayezaliwa na mama mwenye virusi vya ukimwi huwa na antibodies dhidi ya virusi vya

ukimwi kutoka kwa mama yake. Unapopima ukimwi kutumia kipimo cha eliza ambacho uangalia antibodies hizi, basi mtoto huonekana hanao, lakini kama mtoto hakuambukizwa wadudu basi, antibodies hizi huondoka kwenye damu yake kadri muda unavyo kwenda.


Hitimisho

Kuna baadhi ya watu si rahisi kuwaambukiza ukimwi


Mapendekezo

Kutokupa ukimwi kwa muda mrefu huku ukila tunda na mwenye nao kwa muda mrefu haikuhakikishii kuwa huwezi kuupata kwa hakikisha unafuata masharti ya kinga

Mtoto anayezaliwa na mama au wazazi wenye ukimwi si lazima awe nao fuata ushauri wa daktari na hasa kupima wakati wa ujauzito

Tuangalie namna ya kuwadhibiti waganga wa jadi na watumishi wa mungu wanaoshauri watu wasitumie dawa za kuongeza maisha Ukimwi na Magonjwa ya Zinaa
 
Thx mkuu kwa kukujuza,vp kwa mwanamke naye pia anaweza akashiriki tendo la ngono kwa muda mrefu na asiambukizwe? Maana mifano yako yote ime base kwa mwanaume tu ambaye aliishi na mwanamke mwenye hiv carrier.
 
Thx mkuu kwa kukujuza,vp kwa mwanamke naye pia anaweza akashiriki tendo la ngono kwa muda mrefu na asiambukizwe? Maana mifano yako yote ime base kwa mwanaume tu ambaye aliishi na mwanamke mwenye hiv carrier.
kwa mwanamke ni rahisi sana kupata maambukizi kutona na sehemu yake kua laini sana na nitofauti na sehem ya mwanaume
 
Asante kwa taarifa.
Stigma bado kubwa sana kuwa na mahusiano kati ya mtu aliyeambukizwa VVU na ambaye hajaambukizwa.
 
Hizi ni gaps zilizopo kwenye research juu ya hiv.
CCR5 factor inayokuwa juu ya cells ndo inasaidia attachment ya hiv. Hakuna hakika kama ndicho pekee kinachozuia maambukizi, lakini recently kuna case ilitibiwa ujerumani nadhani. Jamaa mwenye hiv alikuwa ana bone marrow cancer, akahitaji implantation. Wakamuwekea bone marrow za mtu asie na ccr5, eventually akapona hiv kabisa (cell zenye hiv zilipokufa newly produced cells hazikuweza kuambukizwa)

nimeshuhudia cases 2. Moja watoto mapacha, wakiwa form one mmoja akagundulika ana hiv na twin wake akiwa negative. Mama alishafariki bila kupimwa. Baba alipimwa na kukuta ana hiv. Conclusion ilikuwa kurwa alizaliwa normally na kuambukizwa hapo, doto alizaliwa kwa operation.
Case ya pili, rafiki yangu mmoja anadai gf cum wife ana hiv. Wana mtoto mmoja asiye na hiv na wanategemea wa pili anytime now. Mkaka hapati hiv, manake anajilipua kwa sababu ana allergy na latex. Ni ngumu kuamini lakini wanapendana haswa na mkaka anapima hiv kila wakati na hajapatwa. Ni study very interesting kujua ni nini kinapelekea, sema ndo third world tena.
 
Back
Top Bottom