Watu watatu wafikishwa kortini wakikabiliwa na shitaka la kusafirisha Dawa Za Kulevya aina ya Heroine Kg 30

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,242
2,000
Mkazi wa Mbezi Tangibovu Said Mbasha(24), na wenzake watatu, wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 30.

Wengine ni Joseph Dalidali(27) maarufu Kama Mbezi Tangibovu; Allu Murugwa( 24) mkazi wa Kijitonyama na Fatima Shomari(24).

Akiwasomea mashtaka yao, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakim Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya, alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao, Machi 3, 2021 katika eneo la Kijitonyama Wilaya Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 30.6, wakati wakijua ni kosa kisheria.

Pia, Dalidali na Shomari, wanadaiwa Machi 3, 2021 katika eneo la Kinondoni mtaa wa Kasaba , washtakiwa hao wanadiwa kukutwa na gramu 2.63 za bangi, wakati wakijua kufanya biashara hiyo ni kosa kisheria.

Upelelezi haujakamilika na Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 24, 2021 itakapotajwa.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

1615475234784.png

1615475272482.png
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,390
2,000
KILOGRAM THERATHINI?

30 KG?

Watoto wadogo wanaendesha Range Rover si tunapambana miaka nenda rudi ndio tunapata Passo used 4th end baada ya kuchukua mkopo NMB. Dah.
Hao ni wageni wa kazi hiyo
Inaelekea walipopata line hiyo
Walikuwa na wenge mambo mengi
Acha wanyooshwe kg30 hawatoki kirahisi
Rahisi sahv na walivyokuwa warembo huko
Jela watabadilika

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,390
2,000
Hawa haiba tu zinaonyesha ni watu wa unga. Kama mimi ni hakimu nawalima miaka bila hata kusikiliza ushahidi.
Hawa walikuwa wanatumika kama chimbo&supply ni wageni wa kazi hiyoo

Wangejua sahv unga kuushika kukaa nao ni soo
Majigambo pia yamewaponza ndomna kesi yao mahakamani mpka bongomovie wasanii walienda kusikiliza mpk wengne wakaawa wanalia

Maana kutoka hawa ni mtihani

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 

fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
10,207
2,000
Inafanyika mzg mingi inatoka msumbiji
Na watu wageni wa biashara hii ndiyo wanapata
Line wengi wao wenge linawaponza

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Mtu anafanya biashara kama hiyo anajimwaga mtaani kama vile anafanya biashara halali kweli hawa vijana wanaonekana bado wana ujinga na ushamba mwingi! Apo watatoka jela wakiwa pengine na miaka 50
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom