Watu watano wafariki dunia katika ajali ya gari la abiria na la mizigo jijini Dar es Salaam

Ohooo pale noma kuna siku nilishuhudia boda boda mmoja aliburuzwa chini ya uvungu wa basi cha ajabu akatoka mzima kavaa koti lake pana ajabu mpaka wale trafiki wakabaki wanacheka yani maana raia tulishahesabu.

Ikabidi akapumzishwe kwenye kile kibanda chao alafu jamaa atakuwa mkigoma yule si bure.
 
Ohooo pale noma kuna siku nilishuhudia bodaboda mmoja aliburuzwa chini ya uvungu wa basi cha ajabu akatoka mzima kavaa koti lake pana ajabu mpaka wale trafiki wakabaki wanacheka yani maana raia tulishahesabu.

Ikabidi akapumzishwe kwenye kile kibanda chao alafu jamaa atakuwa mkigoma yule si bure.
Ilikuwa mwaka gani? Naweza kuwa namfahamu
 
Shida ya maeneo yale sio matuta, panaweza kuwekwa matuta na tatizo likawa lipo kama kawaida, shida ya pale ni mataa. Muda mwengine yanakuwa yanajichanganya na kuonesha njia mbili kwa wakati mmoja kuwa zimeruhusiwa.

Iliwashahi kutokea siku moja, kutokea taifa imeruhusiwa na kutokea kibasila pia imeruhusiwa. Na hivyo kupelekea mkanganyiko kwasababu anaetokea taifa yuko highway na anaetokea kibasila anakatisha. Muda mwengine mataa huwa hayafanyi kazi kabisa. Afadhali police. traffic wakiwepo huwa wanasaidia sana.
 
Ilikuwa mwaka gani? Naweza kuwa namfahamu
Ilikuwa mwaka jana mkuu,ila pale boda boda wanapata sana ajali kutokana na presha ya wale askari wanaokamata madereva wa boda boda wanaokatiza eneo lile,wale jamaa ni kama wanavizia vile.
 
Atakua huyo chizi alipita na nyekundu.. Daladala huwa wanatabia moja kwa kuwa wanapita hapo kila siku asubuhi hadi jioni huwa wanakua washazoea mtirirko wa taa sasa mda mwingine anaona kabisa taa ishahamia njano inakwenda nyekundu ana assume roli bado gia hazijaingia hapo sasa ndio kimbembe.

Alhamisi iliyopita tulitaka kugongwa hapo na roli dereva alifanya hivo nilivyosema ali underestimate power ya roli ghafla tu yukaona hili hapa ubavuni sema liliminya breki likasimama ka muujiza hivi.
 
ohooo pale noma kuna siku nilishuhudia boda boda mmoja aliburuzwa chini ya uvungu wa basi cha ajabu akatoka mzima kavaa koti lake pana ajabu mpaka wale trafiki wakabaki wanacheka yani maana raia tulishahesabu.

Ikabidi akapumzishwe kwenye kile kibanda chao alafu jamaa atakuwa mkigoma yule si bure.
Kwani kigoma wakoje mkuu??
 
Mi nashauri Ma dereva wote wa Daladala warudi shule,maana sasa hivi DAR kuna mabarabara mapya tena ya kisasa!! Sizani Kama wanajua kutumia hizo alama mpya za barabarani!!
Huu ushauri wako sikubaliani nao moja kwa moja kwa sababu udereva ni ule ule tu isipokuwa wanatakiwa kuongezewa uelewa kwenye matumizi ya alama za barabarani, na hii ni kutokana na kuongezeka kwa baadhi ya alama za barabarani.
 
Huu ushauri wako sikubaliani nao moja kwa moja kwa sababu udereva ni ule ule tu isipokuwa wanatakiwa kuongezewa uelewa kwenye matumizi ya alama za barabarani, na hii ni kutokana na kuongezeka kwa baadhi ya alama za barabarani.
Poleni sana wafiwa ndg na jamaa popote walipo mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali Pema peponi.
 
Back
Top Bottom