Watu watano wafariki dunia katika ajali ya gari la abiria na la mizigo jijini Dar es Salaam

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,191


Ajali mbaya imetokea asubuhi hii jijini Dar es Salaam ikihusisha magari mawili moja likiwa Scania Semi - Trailer na Daladala, inasemekana abiria wa daladala wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Pamoja na kuwekwa taa za kuongozea magari, eneo hilo la Chang'ombe linasemekana kuwa hatari kutokana na ajali za mara kwa mara, kwa pamoja tuzidi kuwaombea majeruhi, tujitahidi kuwasimamia madereva wa gari za abiria kama daladala na mabasi mengine waende kwa umakini zaidi.

-----
Watu watano wamefariki Dunia papo hapo na wengine kumi kujeruhiwa katika eneo la Chang'ombe, Da es salaam. Ajali hiyo imehusisha magari mawili moja likiwa gari la kubeba abiria maarufu daladala na lingine ni Scania Semi - Trailer.

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni mwendokasi wa dereva wa daladala eneo hilo maarufu kama chinja chinja. Dereva wa daladala amekimbia na anatafutwa na polisi.

Screenshot_20201005_085206.jpg

1601879452982.png
 
Ajali mbaya imetokea asubuhi hii jijini Dar Es Salaam ikihusisha magari mawili moja likiwa Scania Semi - Trailer na Daladala, inasemekana abilia wa daladala wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Pamoja na kuwekwa taa za kuongozea magari, eneo hilo la Chang'ombe linasemekana kuwa hatari kutokana na ajali za mara kwa mara, kwa pamoja tuzidi kuwaombea majeru, tujitahidi kuwasimamia madreva wa gari za abilia kama daladala na mabasi mengine waende kwa umakini zaidi.

Machinjioni hapo pameanza tena
 
Poleni
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Awaponye Haraka Sana Majeruhi
Waweze Kulijenga Taifa
 
Back
Top Bottom