Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
687
1,360
Unakuta mtu kazaliwa na wazazi wastaarabu na wenye dini lakini baada ya kuyajua ya ke na me(mapenzi) mtu huyo anawakana hadi wazazi kwa tabia mbovu na za kishenzi kwa kisingizio cha usasa

Wengi wetu tumezaliwa na familia duni na za kawaida kiasi ila baada ya kuyajua ya duniani mtu anaacha ya kwao kwa kigezo cha usasa na kuanza kuvaa vichupi na kukaa uchi tafauti na alivyo lelewa.

Hata waliozaliwa katika utajiri bado familia zao hazikuwa nyuma kuwalea katika maadili lakini badala yake wakawapuuza wazazi kwa kisingizio cha usasa

Wazazi wengi wanashindwa kuwalea watoto katika maadili kwa kisingizio cha usasa badala yake watoto wanakuwa wapumbavu, watembea uchi na wagawaji kiholela na wavuta bangi ilhali wazazi hao wapo stable kimaadili na kiuchumi pia

Matokeo yake jamii imekuwa haiangaliki, haishauriki na haitamaniki kwa uovu na ukahaba uliopitiliza unaochagizwa na uvaaji wa nguo fupi na tabia mbovu mbovu za vijana na watu wazima kwa kisingizio cha usasa baada ya kushindwa kwa uwajibikaji wa wazazi kwenye famila zao hatimae kuiharibu jamii kwa ujumla.
 
Usiwasukumie vijana lawama zisizo wahusu, hizo lawama zipeleke moja kwa moja kwa hawa wazee kwa kuharibu hiki kizazi.

Unampa mtoto malezi ya kighaibuni alafu huyo mtoto aje kuishi maisha ya kiafrica. Utamlaumu bure huyu mtoto

Mzazi umeweka Demokrasia kwenye malezi, mtoto anayohaki ya kuchagua anachokitaka, huyu akikua akafanya maamuzi yake bila kumsikiliza mtu utamlaumu?

Kama unampa mtoto malezi ya kimagharibi basi hakikisha anakwenda kuishi huko, Hapa Africa ataonekana hana adabu na anaendekeza ukisasa ambao kiuhalisia kapewa na wazazi wake.
 
Je nikikwambia usasa ni kuvaa nguo ?
Au hizo Imani / Dini za Ughaibuni utasemaje ?
1707814901153.png

To each their own....
 
Usiwasukumie vijana lawama zisizo wahusu, hizo lawama zipeleke moja kwa moja kwa hawa wazee kwa kuharibu hiki kizazi.

Unampa mtoto malezi ya kighaibuni alafu huyo mtoto aje kuishi maisha ya kiafrica. Utamlaumu bure huyu mtoto

Mzazi umeweka Demokrasia kwenye malezi, mtoto anayohaki ya kuchagua anachokitaka, huyu akikua akafanya maamuzi yake bila kumsikiliza mtu utamlaumu?

Kama unampa mtoto malezi ya kimagharibi basi hakikisha anakwenda kuishi huko, Hapa Africa ataonekana hana adabu na anaendekeza ukisasa ambao kiuhalisia kapewa na wazazi wake.
Kuna baadhi ya vijana wanastahiki lawama unakuta familia zao wazazi wanajitahidi sana kuwalea kimaadili ila wao wanajificha kwenye muda na kuwaona wazazi wao wamepitwa na wakati
 
Mkuu kila jamii ina utamaduni wake, hao waliovaa mavazi hayo huwezi kuwafananisha na hawa wanaoongeza hadi shape ili kuwashawishi wanaume kingono
1707815964590.png

Again to each their own....;

Uzuri wa kuwepo varities kila mtu anachagua roho inapenda...; tukianza kupangiana utamaduni na asili utagundu chochote ulichovaa hapo dakika hii huenda sio asili yako...
 
Unakuta mtu kazaliwa na wazazi wastaarabu na wenye dini lakini baada ya kuyajua ya ke na me(mapenzi) mtu huyo anawakana hadi wazazi kwa tabia mbovu na za kishenzi kwa kisingizio cha usasa

Wengi wetu tumezaliwa na familia duni na za kawaida kiasi ila baada ya kuyajua ya duniani mtu anaacha ya kwao kwa kigezo cha usasa na kuanza kuvaa vichupi na kukaa uchi tafauti na alivyo lelewa.

Hata waliozaliwa katika utajiri bado familia zao hazikuwa nyuma kuwalea katika maadili lakini badala yake wakawapuuza wazazi kwa kisingizio cha usasa

Wazazi wengi wanashindwa kuwalea watoto katika maadili kwa kisingizio cha usasa badala yake watoto wanakuwa wapumbavu, watembea uchi na wagawaji kiholela na wavuta bangi ilhali wazazi hao wapo stable kimaadili na kiuchumi pia

Matokeo yake jamii imekuwa haiangaliki, haishauriki na haitamaniki kwa uovu na ukahaba uliopitiliza unaochagizwa na uvaaji wa nguo fupi na tabia mbovu mbovu za vijana na watu wazima kwa kisingizio cha usasa baada ya kushindwa kwa uwajibikaji wa wazazi kwenye famila zao hatimae kuiharibu jamii kwa ujumla.
uovu na tabia mbaya zisipokemewa hatua za mwanzo kabisa hukomaa na kua haki ya watenda uovu na ubaya huo....🐒

ndicho kinachotokea nyakati hizi 🐒
kuvaa uchi ni haki tena inatetewa kwa nguvu zote na mafeministi 🐒

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
View attachment 2902585
Again to each their own....;

Uzuri wa kuwepo varities kila mtu anachagua roho inapenda...; tukianza kupangiana utamaduni na asili utagundu chochote ulichovaa hapo dakika hii huenda sio asili yako...
Mkuu hayo ni kulinda ukiukwaji wa maadili unaoendelea duniani kwa tamaa za pesa na ngono kwa kigezo cha usasa

Hizo picha ulizotuma haziwezi kuuziba ukweli kuhusu maadili mabovu ya kujiuza, na udangaji unaofanyika kwenye jamii
 
Ngono ni nini ? Na hizo so called ngono sasa hivi wewe au kipindi cha Babu zako mtoto anachumbiwa akiwa na miaka mitatu ipi / wapi unaweza kusema ni udhalilishaji na mbaya kwa jamii
Hizo picha ulizotuma haziwezi kuuziba ukweli kuhusu maadili mabovu ya kujiuza, na udangaji unaofanyika kwenye jamii
Unajua the old Proffession in the World ?

Kujiuza na Udangaji ni tangia enzi na enzi..., hivyo kama kuna wanunuaji basi hio ni huduma..., Uzuri kama wewe unaona hapa hapafai inabidi uchague choice inayoendana na wewe......
 
Back
Top Bottom