Watu wa mikoani (Vijijini), badilikeni too much!

Safari yako tunaomba irudiwe..ila mkoan kwetu ili uone ustarabu wa watu wa huku..
 
Habari za muda huu wana Jf.

Kuna katabia fulani wanacho baadhi ya watu waishio mikoani huwa inaudhi na kukera sana, mno yani. Tunafahamu, huko ndio chimbuko la uzao wa walio wengi umeanzia, tunaelewa umuhimu wenu, na tunapaswa kuwasaidia.

Ila hiyo dhana ya kudhani mtu nakitoka mjini anakuja na mafurushi ya hela itoeni kabisa kilini mwenu. Nyie ndio mnaofanya watu waonekane wameasi kwao, unaweza kuta mtu amekaa miaka zaidi ya mitano (5) hajaenda kwako.

Kwa namna moja ama nyingine hii inaweza kuwa sababu moja wapo.

Mnaomba sana mpaka mnaboa...inafika wakati unatamani kwenda kusalimia ndugu wengine lakini unakosa uhuru kutokana na balance uliyonayo na sisi wengine tumelelewa vyema huwezi kumnyima mtu mzima hela.

Yani nimefika kijijini leo siku ya tatu lakini mpaka nakosa amani, yani mtu anatoka nyumbani kwake tena sio hata ndugu wa karibu, anakuja kabla hata hujaamka kisa kaambiwa huko kilabuni kuna mtoto wa fulani ametoka DAR kuja kusalimia, hivyo hawezi kosa chochote.

Atakaa hapo ale anywe na akiondoka umpe chochote, leo asubuhi nimekuta watu 6, achilia mbali juzi na jana...kila mtu ana badget zake.

Leo imebidi nimwite mzee chemba. Nimemkabidhi fungu lao, na nikamwambia kabisa nimebaki na hela ya mafuta ya kunirudisha Dar, sasa kama wewe ndio umewaambia nipo hapa kawape hizo zako na mkeo.

Siku tatu nitumie 600k just kwa kugawa gawa tu nakulisha familia za watu wasijue hata mjini na ishije

Mtanisamehe kwa kweli, kama nitatafsirika nina roho mbaya acha ionekane hivyo.

Mliokutana na huu upuuzi hebu changieni tupate la kujifunza.
Hutosikia mtu wa Tabora akilalamika hivi, hiyo hela utaitoa bila kuombwa, wanajua kupokea mgeni hawahitaji hela yako wala zawadi labda wewe ndio uwafikirie uwape.
 
Acha uchoyo mzee yaani umekaa miaka miwili hujaenda mkoa unashindwa kuweka hata laki 2 ya kusafisha jina angalau umpe mzee heshima??yani hata dumu la Lita 20 la pombe za bush halifiki elfu 15 pia unashindwa??Tatizo lako uchoyo hayo in ya kawaida mikoani.
 
Acha uchoyo mzee yaani umekaa miaka miwili hujaenda mkoa unashindwa kuweka hata laki 2 ya kusafisha jina angalau umpe mzee heshima??yani hata dumu la Lita 20 la pombe za bush halifiki elfu 15 pia unashindwa??Tatizo lako uchoyo hayo in ya kawaida mikoani.
Soma vizuri mzee nimechoma laki 6
 
Back
Top Bottom