Watu wa mikoani mnatujazia jiji letu

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
415
1,032
Nina hasira sana.

Naanza na nyie watu wa mikoani ambao kila kukicha tunawapokea stand ya magu na mabegi yenu ya shangazi kaja, mkifika pale mnatapeliwa kwa kuuziwa sabuni eti mnadanganywa simu.

Nakukaribisha kwangu, kwenye chumba changu unapagawa na flat nchi 55 ukutani, sofa kali kitanda kikubwa unabaki unaduwaa maana hivi vitu vigeni kwenu ushamba huooo.

Nakupa pamba zangu huendane na watu wa Dar wasikushangae kwa manguo yako ya kishamba na maviatu yako meusi kama wanafunzi wa msingi, acheni ushamba.

Baada ya weeks kadhaa mnajiona tayari mshajua jiji na kuanza kubadilisha lafunzi eti niaje mwana kudadeki, nakulisha nakuvisha alafu unajiona mjanja wa Dar pumbavu zako.

Naomba serikali yangu iweke kuja Dar lazima uwe na Visa, maana mnajaza bure jiji letu pendwa kila mtu wa mikoani unawaza kuja tu Dar tushawachoka sasa.

Bakini huko Bush kwenu kwa hao mademu zenu wasiojua kukata mauno, hii ndo Dar.
 
Ni kweli watu huenda wanakuja na ushamba kutoka "mikoani", ila si wote wanadumu nao. Huenda wewe au wazazi wako pia u/walikuja wakiwa washamba na "maviatu meusi" ila wakapambana mpaka wakamiliki hizo "flat screens" unazoona ndio kutoboa maisha.

Relax! Dar haina mwenyewe; watu wanatimba hapa na ushamba wao na ndani ya miaka kadhaa wanakuacha ukipambania daladala na vurugu na mwenye nyumba wako, au ukiishi uswahilini na wao waki-occupy apartments za city center.

Acha makasiriko. Kama hutaki mtu kwako mkatae tu. Siyo unaleta manyanyaso then akitoboa ndo unaanza kujivunia kuwa alifika kwako. Kuna watu wana ndugu na marafiki Dar ila hawakufikia kwa ndugu wala marafiki na sasa ni watoto wa mjini wanakula bia za teni teni kule Wavuvi.

Kila mtu ana maisha yake. Hakuna mtu ambaye ukimkataa atang'ang'ana. Labda kama hajaja kutafuta maisha seriously.

FYI wenye Dar yao hata hawaishi tena Dar. Dar ni commercial hub ya Tanzania, na haina mwenyewe. Kila mwenye akili ana haki ya ku-hustle hapa. Huna haki ya kumuona mtu hastahili kufanya maisha kwenye mji huu.
 
Wazaramo ni wastaarabu sana. Kelele nyingi unazozisikia ni zile za wakuja.
Tupo wenyewe tumenyamaza tu watoto wa Shomvi. Mzaramo hasa hawezi kusema maneno haya, hawa ni wale wakuja tu, si unaona hata Kiswahili kinawapiga chenga mtu anaandika "lafunzi" badala ya lafudhi.

Watu wa asili wa miji mikubwa kikawaida huwa hawana ubaguzi, wanapenda wageni, huko kukosa ubaguzi ndiko kumefanya miji hiyo kufanikiwa.

Kuna siku nilikuwa New York City, naongea na OG mmoja mzee mweusi wa New York City, tulikuwa tunaongelea ubaguzi katika watu wa New York City wanaojiona wao watoto wa mjini. Akaniambia kuwa, wale watu wa New York City wenyewe wa asili miaka nenda miaka rudi huwa hawana noma na mtu, hawana ubaguzi, ila wale waliokuja miaka 10 au 20 iliyopita kutoka the Carolinas, Mississippi, Puerto Rico etc., ndio wenye kujifanya kwamba wao watu wa New York City saanaa, bado wanalimbuka na mji.

Sasa sisi ambao baba za bibi zetu ndio walijenga hayo majumba ya katikati Dar (baba yake bibi yangu kajenga kanisa la Azania Front, wamemaliza kujenga mwaka 1903, na kabla ya hapo familia ilikuwepo Dar es salaam) huwezi kutusikia tunatukana watu wa kuja.

Huwezi kumsikia Ali Tambaza akitukana watu wakuja na kwamba familia yao ya Jumbe Tambaza ndio wenyeji wa Dar. Huwezi kuwasikia kina Pambe wakitoa kashfa hizo.

Na Jumbe Tambaza kamkaribisha mpaka Baba Kabwela Mwalimu Nyerere mjini. Mwalimu Nyerere mwenyewe kasema habari hizi mara kadhaa, mpaka hotuba yake ya kustaafu karudia alivyorushwa makaburini akifanyiwa tambiko la Wazaramo na Jumbe Tambaza.

Sasa Jumbe Tambaza angesema huyu Nyerere wakuja, hatumtaki sisi watu wa mjini, tungepata uongozi uliotupatia uhuru bila ya kumwaga damu wa Mwalimu Nyerere?

Huwezi kusikia sisi kina Chanzi, kina Pazi, kina Shomvi, kina Chamgui tunawasema wakuja, labda kama utani wa jadi na watani wetu kina Rupia na Wanyamwezi, na huu tunafanya kwa kujuana wenyewe bila kuhatarisha mahusiano, kuna sanaa yake. Kwanza tumeoana sana, ukiwatukana Wasukuma utajikuta umewatukana watu wengi sana ambao ni ndugu zako, binamu zako, baba zako, wajomba zako etc.

Ukiona mtu anashikia bango kuwa yeye mtu wa Dar, na wengine ni wakuja, ujue huyo si mtu wa Dar.

Kiranga ChaNgeda Sakala Kandumbwa
Misheni Kota/Mwembetogwa/Mchafukoge/Kinyasini/ Upanga/ Oysterbay/ New York City.
 
Ni kweli watu huenda wanakuja na ushamba kutoka "mikoani", ila si wote wanadumu nao. Huenda wewe au wazazi wako pia u/walikuja wakiwa washamba na "maviatu meusi" ila wakapambana mpaka wakamiliki hizo "flat screens" unazoona ndio kutoboa maisha.

Relax! Dar haina mwenyewe; watu wanatimba hapa na ushamba wao na ndani ya miaka kadhaa wanakuacha ukipambania daladala na vurugu na mwenye nyumba wako, au ukiishi uswahilini na wao waki-occupy apartments za city center.

Acha makasiriko. Kama hutaki mtu kwako mkatae tu. Siyo unaleta manyanyaso then akitoboa ndo unaanza kujivunia kuwa alifika kwako. Kuna watu wana ndugu na marafiki Dar ila hawakufikia kwa ndugu wala marafiki na sasa ni watoto wa mjini wanakula bia za teni teni kule Wavuvi.

Kila mtu ana maisha yake. Hakuna mtu ambaye ukimkataa atang'ang'ana. Labda kama hajaja kutafuta maisha seriously.

FYI wenye Dar yao hata hawaishi tena Dar. Dar ni commercial hub ya Tanzania, na haina mwenyewe. Kila mwenye akili ana haki ya ku-hustle hapa. Huna haki ya kumuona mtu hastahili kufanya maisha kwenye mji huu.
Kama wewe ndo hatukutaki kabisa
Yani tukikuona stand tunaita mwizi kudadeki,relax broo maisha hayahitaji nguvu sana
 
Back
Top Bottom