Watu wa kusini tumesahaulika sana katika teuzi mbalimbali

Bwana mkubwa ametusahau sana , sisi watu wa kusini hupati shida kutambua majina yetu. Ukisikia majina kama tembo, komba, mapunda, ngonyani, simba, nyoka , mwakinyonga, mwakimpusa, sanga, lupembe, msigwa, n.k

Nimepitia teuzi nyingi hayo majina hayapo kabisa sijui kwa nini . Mkuu sisi ni watu pia ijapokuwa majina yetu ni ya wanyama.

Tunaomba radhi kama tulikukosea , kwani na wewe ni binadamu wakati mwingine unakwazika, najua wakati mwingine tumeponzwa na watu wa mbeya kwani wakati wa kampeni walizomea kampeni zetu, naomba uwasamehe kwani adhabu uliyotupa inatosha, na tumejifunza sasa .

Kidumu chama changu cha CCM. kidumu milele , kidumu kisitoke madarakani
Ushamba...
 
Tumwombee Lizabon ateuliwe atutowe kimasomaso, manaake anafanya kubwa ya unafk na uwongo kama ilivyo hulka yetu watu wa kusin
 
iringa, mbeya, rukwa, mpanda mikoa minne waziri mmoja tu mwakyembe na mzigo lukuwi
 
  • Thanks
Reactions: 365
Hayaaa tumesikia na tutawafikia! Ccm hawana jipya kabisa nasubiri 2020 nione nani anajifanya anazijua fitna amuwekee zengwe Juma!
 
Kusini ipi? Wacha kutusanifu arifu.
Hapo kwenye mlima umesikia jina lolote?
Hanma noma. Kodi zetu mnazitaka ila sisi hamtutaki.
Haya banaaa.
Maringeni, duh...nimecheka sana...ina maana mnaisoma namba baada ya 'kutesa' kwa muda mrefu???
 
iringa, mbeya, rukwa, mpanda mikoa minne waziri mmoja tu mwakyembe.

Duh, hivi Lukuvi ni wa wapi vile? Hivi Njombe haina waziri? Haa, Dr.Mahiga huenda anatoka Mara pengine...tehtehtehtehteh...no research no right to speak..an old adage goes..
 
Kweli kabisa kanda ya juu kusini ndio kabisa sio miradi ya maendeleo wala nn..utasikia kiwanda mwanza kiwanja mwanza Barbara geita..labda wanazani huku sio tz ni Malawi ama zambia tujue moja
 
Back
Top Bottom