Watu wa Kurugenzi ya Habari Ikulu hawana uwezo, walilipwa fadhila

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,200
103,735
FB_IMG_1514917875497.jpg

Nimesoma press ya Ikulu ikizungumzia matukio mawili aliyofanya Mheshimiwa Rais leo. La kwanza ni kutembelewa na familia ya Nguza Vicking (Babu Seya) na la pili kuhudhuria msiba wa mke wa Naibu Waziri Kangi Lugola na kutia saini kitabu cha maombolezo.

Kuna makosa ya kitaaluma ambayo hayakupaswa kufanywa na taasisi nyeti kama Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu. Kwa nia njema kabisa napenda kuyabainisha ili usaidia kuboresha tasnia hii adhimu ya habari.

Mosi
Taarifa ya Rais kutembelewa na Babu Seya imepewa uzito mkubwa kuliko taarifa ya Rais kushiriki msiba wa mke wa Naibu Waziri Lugola. Hii si sawa. Rais kushiriki msiba ni habari kubwa kuliko Rais kutembelewa na familia ya Nguza.

Unapokuwa na habari zaidi ya moja ni muhimu kupima ni habari gani ya kuipa kipaumbele (Lead story). Lazima uhakiishe Lead story inakua a uzito kuliko habari zingine ulizonazo. Unaweza kupima uzito wa habari kwa kutumia vigezo kama Prominence (ukubwa wa mwenye habari). Kwa mfano Rais JPM angetembelewa na Rais wa Marekani lazima habari hiyo ingekuwa kubwa kuliko ya msiba wa Lugola. Lakini si kutembelea na familia ya Babu Seya.

Vigezo vingine ni impact. Habari ya msiba ina impact kubwa kuliko kutembelewa na Babu Seya. Hii ni kutokana na nafasi ya Kangi Lugola katika serikali, na tukio lililomkuta ambalo ni msiba.

Pia kuna vigezo kama Bizzare (tukio la kustaajabisha). Kwa mfano akina Babu Seya wangefika Ikulu then watolewe "nduki" kwa viboko hiyo ingekua habari, lakini kama wamepokelewa vizuri hiyo sio habari. Kwenye taaluma ya habari tunasema mbwa kumuuma mtu si habari lakini mtu kumuuma mbwa ni habari. Thatz Bizzare.!

Vigezo vingine vinavyoweza kutumika kupima habari na ukubwa wake ni kama Timeliness (muda), Proximity (ukaribu wa tukio ether physically or psychologically), Human Interest, Conflict, etc.

Kwa ujumla vigezo hivi huitwa NEWS VALUES. Hivi ndio ambavyo Wahariri huvitumia kujua ni habari ipi iwe Lead Story, ipi iwe Strap story ipi iwe Anchor Story, na ipi itupwe kapuni.

Sasa kwa matukio mawili ambayo Rais ameshiriki leo, ni wazi tukio la msiba lilipaswa kupewa uzito mkubwa zaidi kama Msigwa angezingatia kanuni za kitaaluma.

Huenda Msigwa amezingatia "msisimko" wa tukio la kuachiwa huru kwa Babu Seya na familia yake na kuamua kuipa uzito habari ya Babu Seya kuliko ya msiba. Lakini ukweli ni kwamba msisimko hutokea pale ambapo habari inabreak kwa mara ya kwanza (breaking news). Na kwa Babu Seya breaking news ilikua pale walipoachiwa, sio walipomtembelea Rais leo.

Mbili
Kurugenzi ya mawasiliano kupoteza umakini katika kuripoti habari zake. Mara kadhaa kurugenzi hiyo imeonekana kukosa umakini katika kuripoti takwimu, taarifa, maeneo, majina etc. Hili ni kosa kitaaluma. Katika "Principle of Ethical Journalism" ni lazima unapotoa taarifa/habari iwe na ukweli, na umakini (Truthfullness and Accuracy) na kama ni data ziwe credible. Kunahitajika umakini mkubwa unaporipoti data au taarifa nyingine hasa majina ya watu au mahali. Ni makosa kutumia majina bandia kwenye habari unless uwe umefanya "intentionaly" ili kumlinda source.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imewataja watoto wawili wa Nguza kuwa Papii Nguza na Nguza Mbangu. Lakini hakuna mtu anayeitwa Papii Nguza kwenye familia ya Nguza Vicking. Jina halisi ni Johnson Nguza, na jina lake la kisanii ni Papii Kocha. Hilo la "Papii Nguza" sijui Msigwa kalitoa wapi.

Halafu hata Nguza Mbangu (mtoto mkubwa wa Nguza Vicking) ni jina la kisanii. Jina lake halisi ni Michael Nguza. Kwa hiyo Msigwa angeweza kuandika Michael Nguza halafu akaweka bracket akaandika (Nguza Mbangu), ili kuonesha umakini.

Pia kuna makosa ya usanifu kama "mwanae" badala ya "mwanaye". Lakini kwa kuwa ni orthographical error, its tolerable. Kwenye hili tunaweza kumpa "benefit of doubts" kuwa alipitiwa. Lakini huko kwingine ni vizuri wafanyie kazi makosa hayo na wajirekebishe.!
 
View attachment 666611

Shule hii imenijenga sana!!
 
kati yako na Godbless Lema nani mtunzi wa andiko hili? kama si wewe na hujamtambua nawe umefanya makosa hayohayo yanayoelezwa ktk waraka.
 
Lowasa kuhamia ukawa sio habari,ila petrobas kuhamia CCM ndo habari.proximity
 
Unapokuwa na habari zaidi ya moja ni muhimu kupima ni habari gani ya kuipa kipaumbele (Lead story). Lazima uhakiishe Lead story inakua a uzito kuliko habari zingine ulizonazo. Unaweza kupima uzito wa habari kwa kutumia vigezo kama Prominence (ukubwa wa mwenye habari). Vigezo vingine ni impact.
Pia kuna vigezo kama Bizzare (tukio la kustaajabisha). Kwenye taaluma ya habari tunasema mbwa kumuuma mtu si habari lakini mtu kumuuma mbwa ni habari. Thatz Bizzare.!

Vigezo vingine vinavyoweza kutumika kupima habari na ukubwa wake ni kama Timeliness (muda), Proximity (ukaribu wa tukio ether physically or psychologically), Human Interest, Conflict, etc.

Kwa ujumla vigezo hivi huitwa NEWS VALUES. Hivi ndio ambavyo Wahariri huvitumia kujua ni habari ipi iwe Lead Story, ipi iwe Strap story ipi iwe Anchor Story, na ipi itupwe kapuni.

Katika "Principle of Ethical Journalism" ni lazima unapotoa taarifa/habari iwe na ukweli, na umakini (Truthfullness and Accuracy) na kama ni data ziwe credible. Kunahitajika umakini mkubwa unaporipoti data au taarifa nyingine hasa majina ya watu au mahali. Ni makosa kutumia majina bandia kwenye habari unless uwe umefanya "intentionaly" ili kumlinda source.
.!
Mkuu OKW BOBAN SUNZU, ukisikia ubobezi ndio huu, hii ni shule tosha!, naamini dogo amekusoma na next time atakuwa makini zaidi.

Paskali
 
Hata kama tuna uwezo wa kujiamulia mambo yetu wenyewe lakini kwa hili la kina Papii kupewa kipaumbele linaleta taswira ambayo si nzuri sana, ninakuunga mkono. Najua kabisa rais ni wa wote, wabaya na wazuri, walioonwa na sheria na ambao sheria imewafumbia macho.

Hatukai kisiwani, kama ndani tulishangilia kuachiliwa kwa wabakaji basi ingeishia hapo hapo na si rais kuandaa 'karamu' kwa hawa wasanii waliohukumiwa kwa ubakaji/ashakum ufiraji na ubazazi uliowakuta na hatia mahakamani.
Msigwa angetafakari zaidi maana anaexposure kubwa labda kama taarifa imeandikwa na aliyewahost.

Siwahi foleni, natembea kwa miguu

source_1.gif
 
Back
Top Bottom