Watu wa kanda ya ziwa na kupenda sifa

Watu wa kanda ya ziwa na kupenda sifa

Hivi mbona mnasema mkuu wa kaya ni mzinza na si msukuma ianakuwaje aimudu lugha ya kisukuma kuliko kizinza kwa sababu hata ukimsikiliza tu lafudhi yake ni kisukuma
Wapo watu wanaongea lugha nyingi kutokana na kukaa na jamii za lugha hizo kwa mda mrefu.Hata Mkuu wa kaya yeye ni Mzinza kama baba yake ila mama ni msukuma.Kwahiyo huenda kakaa sana kwa wajomba zake kuliko baba zake.
Sasa Why Dar Imeendelea Kuliko Huko
 
Nosenses kabisa, Mkuu wa kaya n MSUKUMA, hapohapo unasema watu wa kanda ya ziwa wanpenda sifa isipo kuwa WASUKUMA, sasa tukuelewe vipi...?
Ukitaka kuandika kitu filiria kwanxa kisha njoo
Sio msukuma mkuu wa kaya sema anaishi au amezaliwa katikati ya wasukuma
 
Anayejua mkuu wa kaya ni kabila gani atuambie sio mnarukaruka tu mara ooo sio msukuma bali kazaliwa katikati ya wasukuma sasa huko chatu kuna wasukuma asilimia ngapi mpaka asijue lafudhi ya kabila lake
 
Magufuli ni msukuma ila watu wana blah blah nyingi sijui ili iweje, pia yeye mwenyewe huwa anajitambulisha kwa hilo,.... Eti mzinza mara mkara...mara hiki..
 
kanda ya ziwa we run this country ndo maana mnatuonea wivu, afu muwe na heshima angalau kidogo basi. watu mnakula mema ya nchi kwa hisani ya wanakanda ya ziwa lakin bado mnaleta dharau!. tumewaletea uhuru wa nchi kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na kijana wa enzi hizo wa pale mwitongo 'NYERERE' tukaenda vizuri tu na nchi yetu na hata nchi yetu ilipovamiwa na nduli Amin kanda ya ziwa ilifanya kazi kubwa sana kupitia kijana wetu MAYUNGA na mipaka yetu ikakombolewa. haya sasa baada ya miaka 50 ya uhuru mkasema mnahitaji kubadili mfumo wa kuendesha nchi, kanda ya ziwa ikafanya yake mzee warioba mzee wa pale bunda akawapendekezea katiba nzuri sana afu mkashindwa nyie wenyewe, mkakaa pale dodoma mkaitoboatoboa sasa tuwasaidie nini tena! kanda ya ziwa we run TANZANIA, chama kikuu cha upinzani nchini, chama changu chadema baada ya kuona huwezi kufanikiwa bila kanda ya ziwa nchi hii kililazimika kufanyia mkutano wa baraza kuu taifa katika ardhi ya kanda ya ziwa na kikachagua katibu mkuu wa kanda ya ziwa na sasa kiko salama.
binti mdogo wa kanda ya ziwa kaunguruma ndani ya UN tanzania zima ikasalute ila wajinga wachache wanasema alikuwa anajisifia! kuna binti wa kanda ya ziwa tanzania one butogwa shija kafanya yake wajinga wanasema ni sifa! Sasa tunaye rais wa JMT ni mtoto wa kanda ya ziwa kuna mijinga inasema kanda ya ziwa ni washamba huyu rais anaprove wrong, hadi sasa hajashoboka kusafiri kwenda ulaya wala america ambapo kwa mshamba hata kama hana cha muhimu anachokifuata lakin akipata fursa ya kwenda huko hawezi kukataa, yuko radhi aache shughuli zake akazulule america.
kanda ya ziwa we run this country mtuheshimu.
 
Watu wa kanda ya ziwa bhana..
1. Tumejengwa kujiamini na kuwa wanaume wa shoka..so tuna confidence na high self-esteem. So mfano ukizingua hatukupotezei; tunakutwanga/ kukupa makavu live. Lengo ni kujirishisha kwamba sisi ni wa shoka..So We utaona sifa kumbe kwetu ni normal tunalinda heshima katika macho ya jamii yetu tu, wala hatufanyii sifa.

2. Sisi ni watu tunaosocialize sana..mane no mengi, Utani mwingi na katika utani lazima uoneshe wewe ndiyo Kali ya mtani wako.. Sasa akipita mdaresalama atajua unatafuta sifa.. Kumbe wapi.. Ni sehemu ya maisha tu..

3. Tunatoka katika mazingira ambayo 'hero' ndo anaheshimika zaidi. Tunatoka kwenye slums, viporo, pasi ndefu n.k
So, when we make it lazima tucelebrate na marafiki; boys and girls tuliotoka same hood with.. So we utaona nafanya sifa kununua kreti tano kwa mtu mmoja kumbe wala.. Naridhisha nafsi tu tunaua maumivu ya zamani. And coz I made it; I deserve some respect..au sio wazee?
Kweli!
 
Mi mwenyewe sielewi huu ushamba anaousema ni upi sisi ni wapole na hatuna shida na mtu tuko bize na shughuli zetu tofauti na hawa mashoga wa dar.
Hapana huyu sio wa Dar es salaam, wa Dar hawezi kuanzisha thread ya ki mbwa hivi...
 
Kuna wajaluo nao kwa kupenda sifa na kuringia elimu yao wako vzr, mtoa mada naona umewasahau
Wajaluo nawafaham, ukienda huko kwao sijui utegi sijui shirati soko la bholo nk wao tatizo lao ni ukabila, popote walipo wakikutana tu wao nikutwanga kijaluo 24/7.

Wanapenda sifa sana ila hawawafikii wahaya ingawa katika historia inasemekana wahaya na wajaluo wana uhusiano(sina uhakika sana).

Mnaweza kua mko kwenye basi mjaluo mmoja yuko viti vya nyuma wingine yuko viti vya mbele wakaamuoa kubonga kijaluo wote kwenye gari itabidi mnyamaze muwasikilize.

Tatizo lao ni ukabila na kusengenya wako kama wajita kwa kusengenya ila ni wakarimu sana huwezi kufika kwao ukaondoka unalalamika njaa. Utapiga msosi mzito sana sema ndio vile utasengenywa sana.
 
Hivi timu ya mpenda sifa wa lake zone inaweza kweli kukamilika bila uwepo wa mjaluo?
 
Wajaluo nawafaham, ukienda huko kwao sijui utegi sijui shirati soko la bholo nk wao tatizo lao ni ukabila, popote walipo wakikutana tu wao nikutwanga kijaluo 24/7.

Wanapenda sifa sana ila hawawafikii wahaya ingawa katika historia inasemekana wahaya na wajaluo wana uhusiano(sina uhakika sana).

Mnaweza kua mko kwenye basi mjaluo mmoja yuko viti vya nyuma wingine yuko viti vya mbele wakaamuoa kubonga kijaluo wote kwenye gari itabidi mnyamaze muwasikilize.

Tatizo lao ni ukabila na kusengenya wako kama wajita kwa kusengenya ila ni wakarimu sana huwezi kufika kwao ukaondoka unalalamika njaa. Utapiga msosi mzito sana sema ndio vile utasengenywa sana.
Karibu shirati mkuu.. Tule Sato na Ugali wa mihogo mixer mtama..halafu wajaluo tukikutana usipozungumza kilugha na mwenzio ni kama umeamua kujiharibia hiyo siku..maana kila mtu atakudisi kwa namna anavyoweza.. Yaani utaonekana baradhuli haswaa na limbukeni wa hali ya juu.. Especially kama ulitoka village halafu unajifanya kusahau kilugha..
 
Back
Top Bottom