Watu, Taasisi, na Mifumo...


..wapinzani wanataka katiba mpya ili waingie ikulu?

..ccm wanang'ang'ania katiba mbovu ili wasitoke ikulu?
 
Yote kweli ila wananchi (ukiondoa wanasiasa) wanataka nini?

..wanasiasa nao ni sehemu ya wananchi.

..kwa hiyo inahitajika katiba inayotoa HAKI SAWA kwa vyama vyote vya siasa.

..wengine wasiohitaji chochote kwenye katiba waachwe waendelee na maisha yao.
 
Hakuna institutions bila watu!

Institution siyo mashine.

Watu ndo wanatengeneza hizo strong institutions.

Mabadiliko ya kifikra ni ya lazima. Hayaepukiki.

Huwezi kuwa na katiba nzuri, katiba ya ‘wananchi’, bila ya watu kuiandika, kuifuata, kuilinda, kuihifadhi, na kuitetea.

Unaweza kuwa na katiba mpya, ambayo ni nzuri kabisa, lakini huifuati, huilindi, huitetei, na kadhalika.

Hakuna tume huru ya uchaguzi inayojiendesha yenyewe.

Hakuna bunge wala mahakama zinazojiendesha zenyewe.

Na ukitaka mabadiliko ya kweli kwenye hizo taasisi, basi ni lazima pia ubadilike kifikra.

Hakuna mabadiliko yoyote yale ya maana pasipo na mabadiliko ya kifikra.

Mindset lazima ibadilike. Matendo nayo lazima yabadilike.

Ukibadili katiba na ukaacha kubadili fikra, hutoenda popote.

Utaishia kukwama pale pale ulipo.
 
Hayo maneno ya motivesheni spika tu, katiba mpya ndio mpango mzima.
 
Jamaa baada ya kuona muda wa kukaa madarakan kwa mujibu wa katiba umekwisha akatumia ushawish wake kuondoa ukomo wa kukaa madarakan km katiba inavyoelekeza ili aendeleze mapambano na km mungu akimjaalia uhai miaka michache ijayo atatimiza miongo miwili na yupo mstar wa mbele kupigania katiba mpya ya jamhur,najiuliza atajisikiaje ikiwa Bi Mkubwa akituletea katiba mpya km tunavyotaka lkn akakopi kipengele cha ukomo wa kukaa madarakan km katiba ya cdm inavyojitanabaisha???
 
Kwa hiyo Katiba ya South Africa unadhani inaheshimiwa kwa sababu ya mindset za watu au sababu ya institutions imara ambazo ni mazao ya Katiba?
 
Nyumbu hawawezi kukuelewa, wanakomalia mfumo huku wao wamemkumbatia Mbowe
Hapa mbona CCM ndiyo hawawezi kuelewa? Alichoandika mwanzisha mada ndicho kina Mbowe wanapigania. Utapunguzaje nguvu za madaraka ya rais bila kubadili katiba? Utabadilishaji mawazo ya watu bila kubadili sheria na kanuni za na namna uchaguzi unavyoendeshwa ili watu wasione tena kama vyeo ni ''kuula''?
 
Umeelezea vizuri sana. Lakini bila kwanza mabadiliko ya katiba mabadiliko ya fikra hayawezi kuja, au yatakuja baada ya muda mrefu sana. Kama ulivyosema tatizo kubwa la Tanzania ni wananchi karibu wote kuona kuwa kuwa kiongozi ni ''kuula''. Si hilo tu ila uongozi wa kisiasa unachukuliwa kama certificate ya kufanya chochote kwa wananchi. Kwa kifupi maono yetu kuhusu uongozi ni nini bado ni yale ya zamani wakati wa Watemi, Wamangi nk. Leo kuna waziri wa Afya wa Uingereza amelazika kujiuzu kwa sababu ya kumbusu mwanamke wake wakati kuna social distancing rule. Hebu fikiria ingekuwa Bongo! All in all namna tunavyowapata viongozi na katiba kwa ujumla vibadilike ili kusukuma watu wabadilike mawazo
 
Leo tunacheza mziki wenye rythm moja.. Ukitaka kufurahii, kila jumamosii.. njoo uburudike na wanasikinde oyee..!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna majitu ni makorofi humu JF ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Ndugu,
Labda turudi nyuma kidogo.
Kati ya kuku na yai nani alitangulia? Au basi nani anafaa kutangulia? Nani ndio amlete mwingine?
Kwa hapa tulipo yafaa tuanze na katiba bora.
Hii itatuwezesha kujenga misingi imara kufuta madhaifu yaliyopo na hatimae mifumo bora ya uendeshaji wa nchi na taifa bora.
 
Amen
 
Akina Ndugai wanajiwekea 'kinga' ili wasiwajibike kwa matendo yao maovu. Sasa wanafanya vioja na kukejeli wananchi kila uchao. Ni miungu watu.
 
Cc Nyani Ngabu
 
Yote yanaweza kwenda sambamba.

Mabadiliko ya kifikra huchukua muda. Pengine hata vizazi na vizazi.

Licha ya hivyo, mabadiliko ya kifikra bado ni ya lazima.

Hatuwezi kuwa taifa tunalotaka na kutamani kuwa bila kubadilika kifikra.

Imagine tuna katiba mpya. Inakiukwa lakini hakuna la maana tunalofanya na wakiukaji wanaendelea kukiuka bila hofu yoyote ile.

Change of mindset is a must. No two ways about it. No way around it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…