Watu, Taasisi, na Mifumo...

Watu, Taasisi, na Mifumo...

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,079
Reaction score
136,509
Mifumo ni watu. Taasisi ni watu. Na vyote hivyo ni kwa ajili ya watu.

Hakuna mfumo uliojiumba wenyewe tu na unaojiendesha wenyewe. Hakuna taasisi iliyojitengeneza yenyewe. Hakuna taasisi inayojiendesha yenyewe. Kumekuwepo na manung’uniko mengi sana kuhusu ukosekanaji wa mifumo bora na taasisi bora hapa Tanzania.

Muundo wa serikali yetu kwa sasa ni ‘top heavy’. Rais wetu ana madaraka makubwa sana na mengi mno. Sawa, hiyo ni kweli kabisa. Lakini, kilicho cha muhimu kabisa kabla hatujaanza kubadili namna tunavyojiongoza, ni lazima kuwepo na mabadiliko ya kifikra.

Ni lazima tubadilike kifikra na ndipo tutaweza kujenga mifumo imara na taasisi zilizo bora. Fikra kama za ‘ameula’, pale mtu anapoteuliwa kwenda kuutumikia umma, hazijengi chochote kile kilicho bora na imara.

Fikra za kwamba ‘Rais hakosei’, hazijengi chochote kilicho bora na imara. Fikra za kumuona Rais ni kama mungu mtu flani hivi, ni lazima zikome.

Fikra za kinafiki nazo lazima zikome. Kama mtu upo serikalini na hukubaliani na mwelekeo wa serikali unayoifanyia kazi, achana nayo. Jiuzulu. Siyo kujifanya unaunga mkono ili mradi tu uendelee kuitwa waziri lakini kumbe moyoni huamini katika chochote serikali hiyo inachokisimamia!

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki endapo kweli tunataka kuliendesha taifa letu kiutofauti na tunavyoliendesha sasa. Hata tukija kupata katiba bora kabisa duniani, endapo fikra zetu hazitobadilika, katiba hiyo itakuwa ni kazi bure tu. Our collective national ethos has to change. No two ways about it!

Peace ✌️. I’m outta here like last year.
 
Katiba mpya ni muhimu, na umuhimu wake utaonekana pale ambapo katiba hiyo itawang’ata pale watakapoleta mazoea
Ili watu waweze ‘kung’atwa’, inabidi watu tubadilike kweli kweli.

Tuache kuogopana. Tuache kulindana.

Makaratasi ya katiba na maandishi ya katiba hayawezi ‘kumng’ata’ mtu pasipo na watu kuliwezesha hilo kutokea.
 
Shida ya katiba ya sasa, ni kwamba yenyewe haijilindi. Hakuna anayetakiwa kuwa juu ya katiba. Kwetu, rais yupo juu yake. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna.
 
Japo kuna uhutaji wa katiba mpya, suala hili nchi hii lipo kisiasa sana. Sehemu kubwa ya push ya katiba ni kwa ajili ya upinzani wapate madaraka wala sio nia ya dhati ya kusaidia taifa.

Ndio maana wananchi wa kawaida hata hawasukumi hayo mabadiliko yafanyike.
 
Shida ya katiba ya sasa, ni kwamba yenyewe haijilindi. Hakuna anayetakiwa kuwa juu ya katiba. Kwetu, rais yupo juu yake. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna.
Mwisho wa siku sisi watu, wananchi, ndo tunawajibika.

Kwa nini tumwachie mtu mmoja awe juu ya katiba?

Sisi wananchi tuko wengi sana, wengi mno kuliko Rais. Rais ni mtu mmoja tu.

Tukiamua, Rais hawezi kutufanya chochote kile.

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki hata iweje, endapo kweli tunataka mabadiliko.
 
Japo kuna uhutaji wa katiba mpya, suala hili nchi hii lipo kisiasa sana. Sehemu kubwa ya push ya katiba ni kwa ajili ya upinzani wapate madaraka wala sio nia ya dhati ya kusaidia taifa.
Ndio maana wananchi wa kawaida hata hawasukumi hayo mabadiliko yafanyike.
Una hoja ya msingi…
 
Kwamba?

"kwa ajili ya upinzani wapate madaraka wala sio nia ya dhati ya kusaidia taifa."

😂😂😂😂😂😂!

Nani kakwambia hayo?
 
Mwisho wa siku sisi watu, wananchi, ndo tunawajibika.

Kwa nini tumwachie mtu mmoja awe juu ya katiba?...
Kama rais akiwa juu ya katiba, wananchi si lolote si chochote. Tena kama rais anatumia mkono wa chuma, na hakuna kipengele kwenye katiba cha kumwajibisha, tena hata akitoka madarakani ana “immunity” basi tusahau tu na wananchi siyo wa kulaumiwa hapo kwa maoni yangu.
 
Mwisho wa siku sisi watu, wananchi, ndo tunawajibika.

Kwa nini tumwachie mtu mmoja awe juu ya katiba?

Sisi wananchi tuko wengi sana, wengi mno kuliko Rais. Rais ni mtu mmoja tu.

Tukiamua, Rais hawezi kutufanya chochote kile.

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki hata iweje, endapo kweli tunataka mabadiliko.
Mfano rais wa awamu ya tano, alitumia hadi jeshi kuzima maandamano ambayo yanalindwa na katiba Kwani ni haki ya wananchi. Kwasababu hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote hata akiondoka madarakani, basi anaweza kufanya lolote analotaka bila kujali “consequences”
 
Kama rais akiwa juu ya katiba, wananchi si lolote si chochote. Tena kama rais anatumia mkono wa chuma, na hakuna kipengele kwenye katiba cha kumwajibisha, tena hata akitoka madarakani ana “immunity” basi tusahau tu na wananchi siyo wa kulaumiwa hapo kwa maoni yangu.
That’s a defeatist attitude that I don’t subscribe to.
Fikra kama hizo zako ni ushahidi mwingine kuwa tunahitaji mabadiliko ya kifikra kwanza kabla ya kubadili hayo mengine.

Hukujifunza chochote toka kwenye Orange Revolution huko Ukraine?

Hukujifunza chochote toka kwenye Arab Spring?
 
Mfano rais wa awamu ya tano, alitumia hadi jeshi kuzima maandamano ambayo yanalindwa na katiba Kwani ni haki ya wananchi. Kwasababu hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote hata akiondoka madarakani, basi anaweza kufanya lolote analotaka bila kujali “consequences”
Hata Hosni Mubarak alitumia jeshi kutaka kuzima maandamano.

Kilichotokea wote tunajua. Na huyo ni mtu aliyekaa madarakani karibu miaka 30!

Come on Mangi. You need to get rid of that defeatist attitude.
 
That’s a defeatist attitude that I don’t subscribe to.
Fikra kama hizo zako ni ushahidi mwingine kuwa tunahitaji mabadiliko ya kifikra kwanza kabla ya kubadili hayo mengine.

Hukujifunza chochote toka kwenye Orange Revolution huko Ukraine?

Hukujifunza chochote toka kwenye Arab Spring?
Hivi unadhani uko unapopasema ni sawa na sisi?

Kuna story moja kuhusu mazungumzo ya Siad Barre wa Somalia na mwalimu Nyerere, ambapo mwalimu alimwambia kuwa wewe kwako hakuna Amani na una wananchi milioni tano tu, na kwangu nina wananchi milioni 30 na kuna amani.

Siad Barre akamwambia, wewe unaongoza kondoo milioni 30 na mimi ninaongoza chui wachache!
Katiba hii ni ya kikoloni na hakuna ujanja. Niambie walioenda kinyume na Maghufuli wako wapi? Ben Saanane mwenyewe alihoji PhD yake akapotezwa.

Katiba yetu ni ile ya mkoloni. Unadhani tulipata uhuru kwasababu wananchi waliamuwa? Wakoloni wangetaka kubaki wangeweza. Mashinikizo hayakuwa ya wananchi, bali UN ikiongozwa na wamarekani.
 
Back
Top Bottom