Watu maarufu waliopata vifungua mimba 2021

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Ni matamanio na furaha ya kila mwanandoa kubarikiwa na watoto wenye afya, baada ya safari ndefu ya ujauzitoMwaka wa 2021, tumeona na kushuhudia baadhi ya watu mashuhuri ambao wamebarikiwa na vifungua mimba wao.
Hii hapa baadhi ya orodha ya watu waliobarikiwa na watoto wa kwanza mwaka wa 2021;

1.Vera Sidika na Brown Mauzo
Mwanasosholaiti Vera na mumewe Mauzo, walibarikiwa na kifungua mimba wao tarehe 20/10, huku wakifichua kwamba msichana wao alizaliwa saa nne na dakika 21 asubuhi.
images - 2021-11-03T191547.148.jpeg

2.Vanessa Mdee na Rotimi
Msanii Rotimi na Vanessa walipatana kwa sherehe ambapo wallijuana na baada ya muda kuanzisha uhusiano wao.
Wawili hao walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza Septemba 29.
images - 2021-11-03T190742.781.jpeg

3.Mulamwah na Soni
Mchekeshaji huyo na mpenzi wake wamekuwa pamoja kwa muda sasa, na ni wapenzi wa kupigiwa mfano mwema na wengi.
Mwaka huu walibarikiwa na kifungua mimba wao Septemba 20.
Miongoni mwa watu wengine ni pamoja na Willis Raburu na Ivy Nyamu, mwanablogu Xtian Dela na mpenzi wake.
images - 2021-11-03T191825.484.jpeg

4. Jackline Wolper na Rich Mitindo
Wolper ambaye pia ametaja jina kamili la Mtoto wake kuwa ni Paschal, yeye na Baba Mtoto wake wamesema Sababu ya kumpa jina hilo ni kwakua amezaliwa Pasaka.
Mtoto wa Wolper amepewa Ubalozi wa Duka la Lorah linalojihusisha na uuzaji wa vitu vya Watoto kama nguo, viatu na vitu mbalimbali.
images - 2021-11-03T235330.845.jpeg

5.Elizabeth Michael na Majizo
Msanii anayetamba katika tasnia ya filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu alijifungua mtoto wa kiume.
Taarifa hizo zilithibitishwa Jumamosi Julai 17, 2021 na mme wake Francis Ciza ’Majizo’ kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Katika ujumbe wake huo, Majizo aliandika, ”Ililibaki kama jina la kufikirika, mimi na Mama yake tulikuwa tunalitumia (Baba G/Mama G) wakati mtu mwenyewe hayupo.
images - 2021-11-04T000250.651.jpeg
 
4: Jackline walper na richi mitindo.

Nao wamebarikiwa mtoto mzuri kabisa wa kiume mwaka huu, japo hayanihusu ila jina la mtoto hapana kwakweli sijui jaki kalitoa wapi sijui ni la ba mkwe woteva ila hapana....kwa wenye jina hilo samahanini nikianza na Paskali mayala.
 
Asante sana kwa kuboresha taarifa

enzi za ujana nilizaaga huko mitaani, nikataka kumtaja jina mtoto jina likianzia na B, mamake akanambia hilo ni jina la x wake nisilitaje, nikabadilisha faster. tuwe makini na haya majina.
 
4: Jackline walper na richi mitindo.

Nao wamebarikiwa mtoto mzuri kabisa wa kiume mwaka huu, japo hayanihusu ila jina la mtoto hapana kwakweli sijui jaki kalitoa wapi sijui ni la ba mkwe woteva ila hapana....kwa wenye jina hilo samahanini nikianza na Paskali mayala.
Kwani sisi akina Paskali tumekukosea nini Mchuchu?
 
Linawafaa nyie wahenga bana limekaa kizee zee flani hivi amaizing, bora hata angempa Patrick..... Paskali hapana asee
Wacha mtoto atuwakilishe bana.

Kwanza umewahi kuona Paskali mlevi au muhuni muhuni? Hili jina limebarikiwa ati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom