Rais Samia ni bepari

Rais Samia ni bepari

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
4,027
Reaction score
6,802
Kama Marekani,Rais Samia tungemuita 'Republican.'
Sijui jambo gani linatokea Mbeya. Sijafuatilia. Sijapata muda wa kupeleleza. Naona ni vurugu tu kama nyingine nyingi ambazo zimetokea nchini.

Lakini naumiza kichwa kufikiria ni jambo gani linatokea hapa. Huyu Rais ana siasa za Mlengo wa Kulia.

Ukitazama katika historia,utaona kwamba Waingereza walikuwa na Industrial Revolution. Mapinduzi ya Kibepari.
Waliyafanikisha vipi? Waliyafanikisha Kwa kuwapora wakulima wadogo ardhi.

Mapinduzi ya Kibepari yalikuwa peaceful Uingereza kuliko Ufaransa Kwa sababu Waingereza walifanikiwa kuwalaghai watu wao kwamba Yale mageuzi yana faida kwao. Kwa hiyo mabadiliko yote umiliki wa ardhi yalifanyika Kwa kupitia sheria za Bunge. Na hivi walivyoleta haya mabadiliko Kwa amani ndio wakafanikiwa kuitawala Dunia,na kuwaibia watu wote.
Kama hapa Tanzania ambapo Wabunge wameruhusu Waarabu wapewe bandari Kwa miaka mia,na Ngorongoro wapewe Waarabu.

Ufaransa pia,wakafanya Mapinduzi ya Kibepari,French Revolution.
Mapinduzi yote haya, Uingereza na Ufaransa, walikuwa wanapinga Dini,wanaituhumu inawasaidia Watawala.
Yaani ,Dini inafundisha mtu umemwona mwenyewe,kazaliwa maskini,leo hii anatajirika,unalalamika, unalalamika nini?
Kwa hiyo Dini kwa mafundisho kama haya,ikapigwa vita.

American Revolution pia,yakatokea Mapinduzi ya Kibepari.

Unapoongea kuhusu Mapinduzi ujue kuna Mapinduzi ya Kibepari na Mapinduzi ya Maskini.

Ndio siasa za Rais Samia. Ni siasa za kuwatajirisha watu wachache.
Wanasema " maendeleo , maendeleo ', lakini watu hawana hela mfukoni.

Ndio Walter Rodney alikuwa anasema Mkoloni hakujenga reli ili wewe uweze kusafiri,aliijenga kusafirisha bidhaa alizopora.

Kwa hiyo katika kuwasaidia Watawala ndio Dini zimejikuta kwenye matatizo.
Matatizo ya Dini hayajawaji kuwa kwamba inawazuia wananchi kutenda dhambi.
 
Andiko bora kabisa
SAMIA na CCM linapokuja suala la kujitajirisha wao na watoto wao wanaishi kipebari ila linapokuja suala la siasa wanataka kuishi kijamaa.

Hapo ndo CCM imeshindwa kuongoza nchi.
Wachache wananufaika wengi wanalia
 
Anafuata nyendo za Mentor wake Jay Kay! Na yeye anatisha kwenye kujilimbikizia mali. Hawajawahi kuwa wazalendo kwa nchi hawa viumbe.
 
Back
Top Bottom