Watoto Wilson na Sadia walipowasili uwanja wa ndege mjini Sioux City, Iowa mapema

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
'UPDATE: Watoto Wilson na Sadia walipowasili uwanja wa ndege mjini Sioux City, Iowa mapema usiku kuamkia leo
tmp_30537-FB_IMG_1494919808994-1057510568.jpg
tmp_30537-FB_IMG_1494919811652-91116729.jpg
tmp_30537-FB_IMG_1494919814090-2057397516.jpg
tmp_30537-FB_IMG_14949198165951070533450.jpg

Dkt Elias Mashalla wa Mt Meru hospital akiwapokea na kuwajulia hali WATOTO Sadia na Wilson walipowasili kwa ndege yao Sioux City pamoja na mama zao, na Muuguzi , na waendesha ndege wa Phoenix Air jets. Dkt Mashalla alikuwa ametangulia kwa ndege tofauti iliyo muwahisha MTOTO Doreen kutokana na ushauri wa madaktari (Picha kwa hisani ya [HASHTAG]#samaritanpurse[/HASHTAG]
tmp_2712-FB_IMG_1494943105254806635770.jpg

======

UPDATE: Wote wamewasili Sioux City salama na WATOTO wote wako hospitali ya Mercy na wameanza huduma ya kutibiwa. Mtoto Doreen aliingizwa Moja kwa Moja kwenye chumba cha upasuaji mara alipowasili kutokana na hali ailyokuwa nayo. Sadia na Wilson watafanyiwa UPASUAJI kesho. Akina mama wote wamepatiwa kila Moja Mkalimani wake kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano, na Dk Mashalla na Nurse wa Mt Meru wako bega kwa bega na madaktari wenzao kusaidia watoto.


======

UPDATE: Dkt. Steve Meyer, Bingwa wa Mifupa akiongozana na team ya madaktari wengine wanaingia kwenye Chumba Cha UPASUAJI katika hospitali ya Mercy majira ya saa 1 asubuhi (CST-Sioux City IA). MTOTO Sadia, aliyepo kwenye picha hapa chini anaingizwa na kuanzishiwa huduma akiwa ameumia na kupata 'fracture' kwenye shingo, na sehemu kadhaa ambapo aliumia mifupa.
UPDATES
KUTOKA Kwa Daktari Steve Meyer, ndani ya chumba cha UPASUAJI, Mercy Hospital. Marekani. Hivi punde.
"Finished Wilson surgery went phenomenally well fixtures elbow is on both sides and fixed his V fracture he's doing great now operating on Saadia".
FASIRI: "Nimemaliza UPASUAJI kwa MTOTO Wilson, na umefanikiwa vizuri SANA, kiwiko cha mkono pande zote na 'V fracture', anaendelea vema, sasa nafanya UPASUAJI kwa Sadia."
tmp_23896-b27fd428b732ff09b81f90d2ce76abd5222613127.jpg
 
'UPDATE: Watoto Wilson na Sadia walipowasili uwanja wa ndege mjini Sioux City, Iowa mapema usiku kuamkia leoView attachment 509912 View attachment 509913 View attachment 509914 View attachment 509915
==============UPDATES
UPDATE: Wote wamewasili Sioux City salama na WATOTO wote wako hospitali ya Mercy na wameanza huduma ya kutibiwa. Mtoto Doreen aliingizwa Moja kwa Moja kwenye chumba cha upasuaji mara alipowasili kutokana na hali ailyokuwa nayo. Sadia na Wilson watafanyiwa UPASUAJI kesho. Akina mama wote wamepatiwa kila Moja Mkalimani wake kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano, na Dk Mashalla na Nurse wa Mt Meru wako bega kwa bega na madaktari wenzao kusaidia watoto.
TOFAUTI YA MADAKTARI WA HUKO NA HAPA, WATOTO WAMEWEKEWA HADI WANASESERE ..... TZ SASA!!!!
UNAAMRISHWA NA KUBURUZWA BURUZWA KAMA MNYAMA!!!
UJIKUTE MWANANYAMALA KISHA UWE HUTAKI KUTOA RUSHWA kama ni mjamzito utajifungulia kwenye mabenchi, Tanzania tumelogwa
 
Dah. Sa nyingine huwa tunawachukia wazungu kwa kutunyonya ila hawa jamaa wana roho nzuri sana.

Saa nyingine huwa natamani hawa jamaa warudi watutawale. Kutawaliwa na msukuma bora mzungu aseee.

Hawa watato wawili tu, serkal yetu ilikuwa haishindwi kuwapeleka nje kufanyiwa watibabu. Sema tu kuna viongozi wana roho ya paka.
 
Nawaza, hivi hali za hao watoto wanamtambua mtu au wako mahututi kabisa!!
Ahsante wazungu kwa kutujali, Ewe Mwenyezi Mungu peleka mkono wako kwa viumbe hao wanaoteseka, waponyeshe baba wapate kurudia hali zao za awali. Naomba na kushukuru kwa jina la Yesu. Ameeeeeeeeeen
 
Mh, Nyalandu abarikiwe sana, huyu baba anamoyo wa ajabu sana, ndio maana haishiwi mibaraka.
 
Back
Top Bottom