Special Thread kwa ajili taarifa za wajeruhi wa ajali kutoka hospital Mercy, Sioux City IA

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa Watumiaji wa JF kuhusu taarifa za wale wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent kwa sasa wapo kwenye matibabu Mercy Hospital, Sioux City IA: .Ntakuwa naweka Update kwenye hii thread kila baada ya muda kinaendelea.
Hiyo hospital wamelazwa hao watoto.
tmp_5159-IMG_20170519_125236909162462.jpg

=================
UPDATE:
Mei 18, Saa 1:54 (Saa za Afrika Mashariki)

HIVI PUNDE, Mercy Hospital, Sioux City IA:
MTOTO Sadia akiwa na Dkt. Steve Joyce, ambaye ni Daktari wake wa "Internal Medicine". MADAKTARI wanasema Binti Sadia ni MUUJIZA wa Mungu kutokana na HALI aliyokuwa nayo KABLA ya huduma ya UPASUAJI. Asanteni SANA kwa DUA na SALA zenu
tmp_15469-FB_IMG_1495140125420267925710.jpg
==============UPDATES
UPDATE:
Mei 18, Alhamisi
Saa 2:05 (Saa za Afrika ya Mashariki)

HIVI PUNDE, kutoka hospitali ya Mercy, Sioux City, IA

MTOTO Wilson kwa mara KWANZA ametoka NJE ya Jengo Kuu la Hospital ya Mercy akiwa kwenye "wheelchair", huku Mama na Daktari wake wakiwa na TABASAMU***
tmp_15469-FB_IMG_1495134260253-1411097359.jpg

=======UPDATES
Latest UPDATE:
Mei 18, Alhamisi
Saa 4:30 Usiku (Masaa ya Afrika Mashariki)

Habari za HIVI PUNDE kutoka Hospitali ya Mercy, Sioux City IA

MTOTO Doreen amemaliza KUFANYIWA UPASUAJI wa UTI wa MGONGO, kwa KILE ambacho MADKTARI wamesema kumefanikiwa kwa UFANISI Mkubwa, KUPITA matarajio yao. MTOTO Doreen alikuwa afanyiwe UPASUAJI kwa makadrio ya MASAA 5:30, LAKINI zoezi HILO lilikamilika kwa muda wa MASAA 4:00, Huku TEAM ya "Surgical Support" IKIWA na watu 6, na kwa PAMOJA wakiongozwa na MADAKTARI BINGWA 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. MTOTO Doreen amehamishwa KUTOKA chumba cha UPASUAJI na kupekewa ICU, na MADAKTARI wamesema KWAKUWA hali yake imeridhisha SANA, BAADAYE Leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya UPASUAJI, na kumrudisha WODI ya WATOTO ambako ataendelea na MAPUMZIKO. MUNGU amesikia
MAOMBI ya WATANZANIA na WOTE waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya MTOTO Doreen POPOTE Duniani.
tmp_15469-FB_IMG_1495138082599-1718135121.jpg

========UPDATES
UPDATE:
Ijumaa, Mei 19
Saa 4 Usiku (Saa za Afrika Mashariki)

Wakati WATOTO Doreen na Sadia wakiwa wamepumzika,
MTOTO Wilson alikuwa ANAPIGA piano mapema leo katika hospitali ya Mercy, Sioux City IA. Imeelezwa KWAMBA sasa ameanza kuamka kwa muda mfupi na kurudi kukaa kwenye kiti chake (wheelchair). TABASAMU lake linawagusa WOTE walio mbali na karibu. MUNGU awatendee WEMA. Doreen na Sadia wameelezwa kuendelea VIZURI siku yote ya LEO. (Picha kwa hisani ya Dana Meyer, Sioux City IA)

==========UPDATES
UPDATE:
Jumamosi, Mei 20
11:45 Alfajiri (Kwa Saa za Afrika Mashariki)

MADAKTARI wanaowatibu WATOTO Doreen, Sadia na Wilson wamesema HAPATAKUWA na idhini kwa ndugu, jamaa, na marafiki kwa sasa KUWAONA WATATOTO wakiwa hospitali kutokana na KILE walichokieleza KUWA bado wana MAUMIVU makali na wameanzishiwa "Rehab", (Mazoezi ya Viungo, na ya Kisaikolojia). IDHINI hiyo itatolewa na KUTANGAZWA mara MADAKTARI watakapojiridhisha na MWENENDO na hali ya WAGONJWA.
(Pichani, Mwakilishi wa Serikali yetu USA, Balozi Masilingi na Mama wakimjulia HALI MTOTO Sadia kwa NIABA ya SERIKALI na Watanzania WOTE) Picha kwa idhini ya DMS Sioux City IA.
tmp_10184-FB_IMG_14952553694141441517261.jpg

=========UPDATES
UPDATE:

Jumapili, Mei 21

IMERIPOTIWA kuwa MTOTO Doreen ameanza kupata HISIA (feeling) kwenye MIGUU yake yote MIWILI kuanzia JANA Jumamosi. WOTE mnaombwa KUENDELEA kumwombea apate UPONYANI kamili na aweze KUTEMBEA. Leo, Jumapili kutakuwa na MISA maalumu kwa ajili ya Doreen, Sadia, na Wilson katika Kanisa la Sunnybrook Community Church, Sioux City IA kuanzia SAA 1.00 (Saa za CST-Sioux City IA).

Jana Congressman Steve King-R, IA aliwatembelea WATOTO hospitalini kuwajulia hali)
(Picha kwa hisani ya DMS, Mercy Hospital, Sioux City IA)
tmp_10035-FB_IMG_1495397213080-871471779.jpg
tmp_10035-FB_IMG_1495397215800-168102072.jpg
tmp_10035-FB_IMG_14953972183211606945455.jpg

Taarifa zaidi nimeendelea kuzitoa kupitia thread hii. .Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy na wanaelekea kwenye makazi yao
=======UPDATE
UPDATE:-
Jumapili, June 4.
HATIMAYE MTOTO Doreen aruhusiwa kutoka Hospitali ya Mercy,
Sioux City, IA. (Picha kutoka WODI ya WATOTO, Mercy Hospital, Sioux City IA)
tmp_1613-FB_IMG_1496553780717-1161029597.jpg
 
I don't know what to tell my God all I can say is thank you Lord you are so faithful and you say Yes nobody can say No thank you Lord you are above all nothing is impossible or to difficult for you to slove I can see and have seen your hand on these angles we will keep on praying
 
Ungeandika pia kuwa updates hizo unazitoa kwa Mbunge Mh. Nyalandu anayezirusha.
Siyo kila mtu yupo instagram best...

Ugueni pole bado taifa linawatengemea na jamii kwa ujumla... Poleni kwa maumivu.. Mwenyezi Mungu yupo nanyi
 
Tuko Dunia Mbili Tofauti Kabisa.

Hebu linganisha na hali ilivyokuwa wakati wakiwa Kwenye hospital ya Hapa Tanzania.

Mungu aendelee kuwapigania.
 
Back
Top Bottom