Nimeamka asubuhi na alfu tu, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya azam. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti alipofika kwenye maandazi akakuta kapoteza hela yangu, wakati anarudi aniambie, njiani kwa bahati akaokota alfu ambayo kuna mtu alipoteza ndio akanunua askrimu....kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake