Watoto waliotelekezwa kupatiwa bima ya afya

Tangu lini sirikali ikajenga msikiti au kanisa???

Huyo amekumbatiwa na kubebwa na GSM ila mwisho wake mtausikilizia maana mzigo ukimshida punda mateke yanakuhusu
 
...Je watalipiwa kwa mwaka huu tu au wataendelea kulipiwa hadi wafikishe miaka 18 ?
 
Well and good, hizi fedha anapata wapi wakati wakuu wengine wa Mikoa hawapati? anafanya biashara? ipi? na nani?.
Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Tangazo alilotoa kuwapatia Bima ya matibabu Watoto waliotelekezwa na Baba zao ni jambo Jema sana ,SANA TU.kwa ustawi wa watoto hao.
Kwa mtazamo mfupi waweza sema ni zoezi linalolenga kukomoa..!yapasa kujiuliza nani hasa anakomolewa?Ni baba aliyetelekeza..!Pengine alikuwa (sina hakika sana)mzinzi,muasherati..!bila kumwangalia mtoto aliyetelekezwa!ambaye ana maisha marefu mbele..!watu tumefikia hatua kuwatetea watelekezaji?wengine ni wazinzi na waasherati?hili ni aibu kweli.
Kwa BIMA YA AFYA KWA WATOTO...Big up MAKONDA.

Akili ya kuambiwa, changanya na za kwako. "Big up" kwa lipi? Nani atailipa hiyo bima na kwa bajeti ipi? Ni zoezi endelevu (sustainable) au pambio la kisiasa kutafuta front page? Unakubali kuhadaiwa karne hii kwa propaganda zisizo na mashiko! Mwl. Nyerere alisema "mtu akikuambia kitu cha kijinga, na anajua kuwa wewe unajua ni cha kijinga, lakini wewe ukakikubali, basi anakudharau". Usikubali kudharaulika kienyeji hivi hata na mtu wa "fa fa fa" form 4!!!
 
Ndio maana tunasema siasa imewaingia mpaka kusiko ingilika. Kama unashindwa kutenga suala binafsi na shughuli ya ofisi ya umma sasa una haja gani ya kuwa mchangiaji JF? Why usiwe huko FB na wenzako wa hali yako?
 
Akili ya kuambiwa, changanya na za kwako. "Big up" kwa lipi? Nani atailipa hiyo bima na kwa bajeti ipi? Ni zoezi endelevu (sustainable) au pambio la kisiasa kutafuta front page? Unakubali kuhadaiwa karne hii kwa propaganda zisizo na mashiko! Mwl. Nyerere alisema "mtu akikuambia kitu cha kijinga, na anajua kuwa wewe unajua ni cha kijinga, lakini wewe ukakikubali, basi anakudharau". Usikubali kudharaulika kienyeji hivi hata na mtu wa "fa fa fa" form 4!!!
Usichanganye mada mkuu..!BIMA YA AFYA KWA WATOTO Wote ni jambo Jema!Achilia jambo mbali jambo hili kafanya nani?hata angekuwa ni GODBLES LEMA kafanya basi angepongezwa..!sasa izo hela zimetoka wapi ni jambo lingine la kupata ufafanuzi tu..!
 
Ni kweli kabisa kuhusu bima ya afya juu ya watoto hao ni jambo jema sana.Ila upande wangu najiuliza hilo fungu linatoka katika bajeti ipi? ...litatoka serikalini?, ni fedha za mkuu wa mkoa? au ni fedha za wahisani?
Hilo ni swali la msingi sana. Nasikia kuna "mfadhili" eti amejitolea kulipia gharama za bima bila kujali idadi ya watoto. Nafikir tunahitaji kumfahamu huyo mfadhili...
 
Usichanganye mada mkuu..!BIMA YA AFYA KWA WATOTO Wote ni jambo Jema!Achilia jambo mbali jambo hili kafanya nani?hata angekuwa ni GODBLES LEMA kafanya basi angepongezwa..!sasa izo hela zimetoka wapi ni jambo lingine la kupata ufafanuzi tu..!

Hujui usemalo. Soma uelewe. Hakuna asemaye bima si jambo jema. Tunazungumzia sustainability hapa.
 
Maswala kama haya ni ya kushughulikiwa na ustawi wa jamii na mahakama kando ya taasisi za dini, sio jukumu la Makonda.

Yeye ana tuhuma zake na bado hajazitolea majibu. Anapenda sana kurukia sakata ili kujipatia umaarufu feki.

Sasa usishangae hapo kuna wanasiasa wa upinzani labda na viongozi wa kidini wanaopenda kuikosoa hii serikali ndio walengwa. Worthless Exercise Indeed.
 
Back
Top Bottom