Bima ya afya kwa wote ingeanza na watoto na wazee 60+

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
221
528
Kuna kipindi serikali ilikuwa inanadi sera ya huduma za afya kwa watoto chini ya miaka 5 na wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kutolewa bure katika vituo vya serikali.

Pamoja na sera hiyo kunadaiwa na serikali kutoa taarifa kwenye makaratasi kwamba makundi hayo yanatibiwa bure lakini hali halisi haiko hivyo. Gharama kwa makundi hayo wanachangia kama kawaida labda kama kuna mashuhuda waseme hapa

Ili kufanikisha hii adhima nzuri ya serikali kwanini utaratibu mzuri usiwekwe?

Badala ya mzazi kutakiwa kwenda na kadi ya clinic ya mtoto na mzee kwenda na hati maalum ya msamaha kutoka serikali za mtaa ambapo hizo nyaraka ni kama hazi uzito kwa baadhi ya vituo vya afya kwasababu hawapewi huduma inavyostahili. Lazima walipe hela ndio watahudumiwa

Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya kwasasa umeshaanza kuzoeleka kwa watoa huduma na pengine kwa mtazamo wangu watoa huduma wengi ni kama wanaridhika nao kwani siku hizi wanachama wa mfuko huo angalau hakuna malalamiko mengi ya kunyimwa huduma kama zamani

Serikali inashindwa nini kupeleka hiyo ruzuku NHIF ili kila mtoto anapozaliwa atengenezewe Bima yake itakayodumu kwa miaka mitano tu ili kujihakikishia kuwa kweli serikali imedhamiria kutoa huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano?

Hivyo hivyo na kwa wazee wenye miaka 60 ruzuku yao ipelekwe NHIF wapewe kadi za bima zitakazo wawezesha kutibiwa kwenye vituo vya huduma za afya vya serikali.

Kwa kufanya hivi serikali itakuwa imekata mzizi wa fitina kwa wanaoshindwa kutoa hizo huduma
 
Back
Top Bottom