Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
SHERATON HOTEL, njia panda ya machimbo, yombo buza!!!!!
wengi wao itakuwa Dar exit au mijitu ya kufugwa....!
mzee sikonge,
bila kusahau halaiki mazoezi national stadium na maziwa kwa mikate buuure.
na vikundi vya six batallion, jackson 8 nk.
nauli ya dmt kuanzia senti ishirini halafu inakadiriwa kwa umbali.
aah, acha ninyamaze mie.
LOL.....lazima utakuwa wakuja, maana naona hiyo Dar exit imeku-touch ile mbaya!
haya basi, mie pia mtoto wa flats za Ilala...la kwetu lile ambalo mbele kuna ule uwanja wa kuchezea watoto!! nilikuwa na mradi wa ashkrimu za ukwaju...LOL
Tulivaa mizula na milosis!
Ishue ni K-Tea Shop. Kama unaijjua unachangia kitu kuhusu hiyo K-Tea Shop. Kama huijui unajinyamazia.
K-Tea Shop is not just a tea shop, its more than just a tea shop.
game theory,kabla sijalikwaa pipa kuelekea alaska,pilau bab kubwa lilikuwa tawakal hotel,pale livingstone inapokutana na barabara ya msimbazi.ukiingia tuu hotelini waiter anakucheck kama wewe wa kuja au la,mara unamsikia mletee huyu wali jaa mchuzi tele.basi wewe kama mjini wa kuja unaona yes nimepewa priority napewa wali mwingi,kumbe lile neno jaa,maana yake wakuja huyu mletee wali wa jana
Hujanikuna, ila umenikumbusha mbali. Nilivyosoma nikakumbuka na mie nilivyokuwa nikicheka ndugu zangu nikirudi Sikonge. Wanasema nilikuwa naongea Kiswahili cha Kizaramo "...... n'likuwepo nakula pilau ...." Nakumbuka nililazwa Muhimbili na jioni chakula kilikuwa kizuriii. Asubuhi chai ya maziwa na mikate. Mchana ukaja tena wali na chuzi zito. Nikakataa kula kwa kujua mchana watakuja nichukua na nyumbani ntakuta msosi mkali sana. Mhhh, nilikuta ugali kwa maharage
haya basi, mie pia mtoto wa flats za Ilala...la kwetu lile ambalo mbele kuna ule uwanja wa kuchezea watoto!! nilikuwa na mradi wa ashkrimu za ukwaju...LOL
Kile kishule cha vidudu? Mie nilikataa kusoma hapo miaka hiyo kwani nilijua nikirudi kijijini, kaka zangu watanicheka sana kuwa nilisoma shule ya VIDUDU na mie pia ni kidudu.
SIdhani kama utakuwa unanifahamu kwani sikuwa mwenyeji sana zaidi ya jamaa wa Block 4 kama akina Rashidi, Mohamed, Deo na kaka zake, Ray, nk. Kwa mbali bwana Nguvu, kijana Paul na miwani yake, dada yake na wadogo zake. Mhh, zile chips za Mangi na soda zake tamu si kawaida. Ila baadaye mama wa kiarabu(mama Halidi-Marehemu) akaweka Kiosk chake chini ya dirisha letu la jikoni.... Block IV hiloooo baba, miaka hiyo wanaliita ghorofa la watu wanaoshindana. Ukiweka AC, wanajibu, ukiweka antena ya TV, wanakujibu, ukanunua gari, wanakujibu. Kiboko yao ni yule Msomali, ila mkewe alikuwa anatumia sijui mi LADYGAY?? Akipita basi unafeel Oxygen imekwisha. Sijui alikuwa anawezaje kupumua na hiyo harufu?
Nilikuwa pale mwezi wa tatu, nilipotea. Pamebadilika sana. Ikabidi nianze kutafuta nyumba yetu. Mungu bariki nikamuona mama Sembuli (dada ya Marehemu Sembuli wa Yanga)........, heee,kamaliza Chuo kikuu na degree yake ukutani. I was too proud of her. Wamepanda miti na nyuma ya Block IV, nasikia mama Mkapa kanunua lile eneo na ghorofa la Posta na wako busy kuweka jengo hapo. Too sad maana jamaa walikuwa wakicheza mpira hapo jioni (wazee) huku watoto wakichezea huku kwenye shule ya vidudu. Ilikuwa saa nne usiku na sikuonana na watu zaidi ya majirani wa karibu. Sikurudi tena pale. Miaka 10 sasa tangu niwe pale mara ya mwisho na karibu miaka 17 tangu niondoke........... Kumbe yule Mzaramo karibu na Wasabato walimuhamisha na wakajenga kanisa jipya ..... too much change.....