Ah..kwetu hiyo.. Mitaa ya MkunguniSwahili,,Mafia,Masasi,Narung,ombe,Tandamti,Pemba,Kongo,Twiga,Nyamwezi,Aggrey,etc...
Misikiti,Kwa Mtoro,Idrissa,makanisa,KKKT Kariakoo..
Zahanati,kwa Dr Maro,yule wa kihindi Dr nani vile? Na pale Pan African kwa Dr Makene..Baadaye,Al Jumaa..pale Mafia na Sikukuu..
Siwezi sahau miilk shake,na ice cream za Bakhressa pale Livingstone.. Na mikate ilikuwa ya ukweli enzi hizo.. Mitamu ina ladha..
Mahoteli,Mico Hoteli,Hadhara Mount(Pemba na Msimbazi)...
Kulikuwa na askari mmoja alikuwa na mikogo miaka fulani pale Msimbazi Police.. Akiitwa Koplo Mukama Sharp!
Palikuwa na mama mmoja maarufu wa kihindi mama Songambele... Marehemu mzee Chaurembo alikuwa mjumbe wetu wa nyumba kumi.. Tulikuwa tunaenda duka la kaya kupimiwa sukari na unga...
Mambo mengi jamani..