Watoto halaiki waandamana Kigoma kudai haki zao

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Watoto wa halaiki walio kuwepo jana katika uwanja wa Tanganyika tar.14/10/2010 wakati wa kuzima mwenge wameandamana kwenda ofisi ya mkuu wa Mkoa Kigoma wakiimba "Tunataka haki zetu" Wanadai pesa zao.

-Inasemekana huduma za kibinadamu kama maji walikuwa hawapewi juzi wamelazwa kwenye maturubai siku ya kilele wameshinda kwenye jua.

-Dataz zaidi zinadai kuna wakufunzi wametoka Dar kwa siku kazaa wanakula posho tu huku wakiwasahau hao watoto halaiki.

Nawakilisha inatia uchungu sana wakubwa wamesha chukua chao watoto wamewaacha hivi hivi.
 
du ufisadi hata kwa watoto pesa wameshaingiza kwenye kampeni hizo tayari
 
Watoto wa halaiki ya mbio za mwenge zilizo hitimishwa jana mkoani Kigoma nakuhudhuliwa na Mh Jakaya Kikwete leo hii wamefunga barabara (Kigoma) wakidai malipo yao.

BNN
 
:A S thumbs_up:

H
awana effect kwenye uchaguzi wa mheshimiwa ndio maana wamelizwa
, wangekuwa ni potential ungesikia fasta wamelipwa. Hii ndio sirikali ya mh. bwana
 
Dhuluma kwa malaika ni kutafuta laana tuu bse sara zao ni za mshale huenda moja kwa moja kwa mola.
Dalili za JK kushindwa as hasira za Mola zitamwangukia
 
Wanafunzi waandamana na kufunga barabara Kigoma baada ya kutopewa pesa walizoahidiwa kupewa baada ya kuhudhuria kuzimwa mwenge jana. Wenye details watupe


Source: Radio Free Africa
 
hiyo ilikuwa ni sherehe ya serikali sio CCM tafadhali rekebisha kichwa cha habari hii

Duh, sijajua tofauti ya CCM na serikali. Maana CCM wanatumia magari ya serikali kwenye kampeni, wanachota fedha BOT kwa ajili ya kamapeni na vitu kama hivyo. Kwa hiyo CCM na serikali ni haohao.
 
Ni wale waliocheza halaiki wakati wa sherehe za kuzima mwenge... hawajalipwa posho zao hadi leo ndio wakaja juu baada ya Mongela (mkuu wa wilaya ya Kigoma) kuwaeleza kuwa suala lao litashughulkikiwa Jumanne wakati viongozi watakapokutana na kufanya tathmini ya shughuli nzima
 
Suala la kuhudhuria shughuli ya kitaifa kwa nchi unayoipenda kwa moyo sidhani inahitaji posho. Ila kama watu wamezoewa kuhongwa hongwa kwenye kila kitu haya ndo matokeo yake.
 
si walikula pilau ya ccm?.......dawa ni wqazazi wa watoto hao kutowapa kura kikwete na ccm
 
ccm haiwatambui hao hata hawajaingia mkataba na ccm kuhusu shuguli hiyo ni wao wenyewe walijipeleka ---- wananchi wasiwe wavivu hiyo
 
maskini,kumbe wanalipwa??????
Kazi kweli kweli,watadai hadi wazeeke kama wazee wetu wa EAC
 
Back
Top Bottom