Watoa huduma Mitandao ya Simu na Internet wachukuliwe hatua!

jukaboy

New Member
Aug 13, 2015
4
7
Takribani siku nne sasa huduma ya mawasiliano ya Internet imekuwa inapatikana kwa shida sana na wakati mwingine inakulazimu utumie visaidizi kama VPN n.k cha ajabu mamlaka zinazohusika zimekuwa kimya kana kwamba hakuna tatizo lolote.

Watanzania wameendelea kupata hasara kwa maana ya vifurushi walivyonunua na wale wanaofanya biashara kwa njia ya mtandao. Ni wakati sasa wakuvichukulia hatua vyombo hivi. Je, kuna haki kwa mpewa huduma katika hili utakapofungua shauri mahakamani?

Embu tujadili.
 
Hicho chama cha mapinduzi kinahitaji kupinduliwa maana ni kioga,uongozi huu ni hasara kwa taifa wanatumia kila wawezacho kuhakikisha wanafanya vile watakavyo! Vyombo vyenyewe vioga tu vinamapengo lukuki nao hawawezi tetea wateja wao
 
Hawa vijana ndio tunawao watafuta...... Vipi shemeji yako kaamka ushambandikia maji ya kuoga?
😂😂😂
Shemeji yangu ameshinda kwa kishindo ni Gwaji boy!
Dr Magufuli hakika ni mbeba maono
Internet inaharibu kabisa uchumi wetu
Maaana vijana hawafanyi kazi wana kaa na kumuangalia diamond tu na zuchu na kiba na kutafuta ma flowers!
 
Aman ni muhimu kuliko hayo uyanenayo! Tatizo mitandao imevamiwa na wajinga, waongo, wazandiki, mawakala wa mabeberu nk! Kwa hiyo relax ufurahie Uhuru, chini ya serikakari ya CCM, chama chenye maono, kiongozi wa ukombozi nchi za Africa, na sasa ni chama cha ukombozi wa kiuchumi na Uhuru wa kweli kutoka kwa beberu! CCM inaongoza kwa kuwatangulia njia waafrika, tena kwa vitendo
 
This country is full of stupid people.

Nilitarajia wasomi wetu wa sheria kutoka school of law watatupa mwongozo ( hata basi kupitia mitandao ya kijamii) ya nini cha kufanya ili tufungue mashtaka katika mahakama za kimataifa kuyashtaki makampuni ya mitandao Tanzania yaliyoshiriki dhambi hii pamoja na tcra, au hata basi kuanzisha vuguvugu( movement) ya kuhamasisha watz wasusie mitandao ya simu, nalo limeshindikana.

Sijui ni nani aliyeturoga kwa kweli.
 
Aman ni muhimu kuliko hayo uyanenayo! Tatizo mitandao imevamiwa na wajinga, waongo, wazandiki, mawakala wa mabeberu nk! Kwa hiyo relax ufurahie Uhuru, chini ya serikakari ya ccm, chama chenye maono, kiongozi wa ukombozi nchi za Africa, na sasa ni chama cha ukombozi wa kiuchumi na Uhuru wa kweli kutoka kwa beberu! Ccm inaongoza kwa kuwatangulia njia waafrika, tena kwa vitendo

Akili hii takataka kabisa
 
Huduma za kifedha mabenki zimekuwa za shida mno, nadhani katika uchaguzi wa mwaka huu taifa limepata hasara mno
Mbona internet banking zinafanya kazi vizuri Mkuu...hebu acheni visa.

Hongera Mgufuli, Hongera Mwinyi ,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom