Uchaguzi 2020 Watia nia CCM Mbeya wachimbwa mkwara

Halafu Msajili wa Vyama vya Siasa anashupalia Shaibu wa ACT kusema “kufa na kupona”. Nasubiri kusikia Msajili akikaripia vitisho vya kihalifu. Bila shaka mimi na wengine tutasubiri sana!!
 
Hakuna mtia nia wa CCM kukimbilia upinzani, ukishindwa kura za maoni. Ukitusaliti tutakufuata popote ulipo.

Mwaka huu huwezi kuharibu ushindi wa chama cha CCM ukabaki salama, tumepokea maagizo toka juu.
Hahahahaha demokrasia ya CCM tamu sana/ nasubiri wadau wa Lumumba waseme neno
 
5 Julai 2020
Mbeya, Tanzania

CCM NYANDA ZA JUU KUSINI : Walalama na kusema tumechoka kuongozwa na upinzani.


Sasa CCM lazima tuchukue hatua dhidi ya wasaliti walio ndani ya chama maana subira ya kungojea imekuwa ndefu na lazima tufanye hima tusikose kupata kura nyingi za wananchi 2020 hapa mkoani Mbeya.

Source : MbeyaYetuOnlineTV
 
Tutaona mengi sana mwaka huu, na matamko kutoka juu.
saivi inataka kuwa kama vile chama cha kijeshi vile (paramilitary CCM)
Kazi Kwenu watia nia sasa imekuwa kinyume ukikatwa jiajiri sasa
 
Tusinyimane uhuru wa kufunga.( freedom of association) kwani kuhamia chama kingine ni haki ya msingi. Vitisho si utamaduni wa Tanzania au ndo CCM mpya
Kuna vyama viwili tu ninavyovijua ambavyo vina sheria kama hii ya kwamba ukishaingia hurusiwi kutoka maana usije kutoa siri za chama. Ni chama cha wachawi na nyinyiemu
 
Mkuu ni mgeni kwenye Nchi hii? hujui tangu 2015 CCM ndio wameruhusiwa kufanya siasa peke yao? mara ngapi hata vikao vya ndani vya wapinzani vinavamiwa na Polisi....
Sikubaliani na hoja hii mkuu, hasa wakati huu kuelekea kwenye uchaguzi.

Hiki ni kisingizio kisichokubalika kabisa kwa wakati huu.

Sijaona popote July hii wapinzani wakifurumushwa kwa kufanya mipango yao ya kujiandaa na uchaguzi.
 
Mbona unafanya ujazaji fomu kama mtihani wa chuo kikuu vile? Yaliyotokea kwa madiwani, hayakuwa kwamba wapinzani hawakujua kujaza fomu, bali ulifanyika ujangiri fulani hivi! Najua unajua!
 
Nadhani ni kuweka mambo sawa! Hata kama wajumbe watamkataa Dk.Tulia,Kamati Kuu ya CCM itarudisha jina lake.Nawaza lakini.
 
Mbona unafanya ujazaji fomu kama mtihani wa chuo kikuu vile? Yaliyotokea kwa madiwani, hayakuwa kwamba wapinzani hawakujua kujaza fomu, bali ulifanyika ujangiri fulani hivi! Najua unajua!
Mkuu 'Karungikana', sijui, ndio maana nimeandika nilichosikia kwamba kimetokea: kwamba "wapinzani walikosea katika ujazaji wa fomu."

Sikusikia lolote zaidi ya hilo kutoka upinzani wakikanusha hilo na kuchukua hatua, kama za kisheria - kwenda mahakamani watu tujue kuwa walionewa.
Hata kama wasingepata haki zao toka huko huko mahakamani kwa kujua mahakama ni sehemu ya uonevu, sisi mahakama ya wananchi tungeelewa na kujiandaa kutoa hukumu ya mwisho katika uchaguzi huu wa October.

Wewe ulisikia wapinzani wakichukua hatua yoyote kupinga uonevu unaodai walifanyiwa?

Naomba unieleweshe mkuu kama unazo taarifa zaidi ya nilizonazo mimi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…