Uchaguzi 2020 Watia nia CCM Mbeya wachimbwa mkwara

CCM sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha kijeshi kilichojivika koti la chama cha siasa. Na bila tume hii ya uchaguzi, na vyombo vya dola, ccm haiwezi kushinda uchaguzi.
CCM inamiliki vyombo vyote vya dola
CCM inamiki haxina
Usicheze na CCM!
 
19 Julai 2020
Watia Nia CCM Mbeya Wachimbwa Mkwara

Mjiandae kisaikolojia, atakayesaliti kutimulia chama, Katibu Uenezi wa CCM Mpya ndugu Humphrey Polepole aongoza jopo kuwafunda




Hakuna mtia nia wa CCM kukimbilia upinzani, ukishindwa kura za maoni. Ukitusaliti tutakufuata popote ulipo.

Mwaka huu huwezi kuharibu ushindi wa chama cha CCM ukabaki salama, tumepokea maagizo toka juu.

Chanzo: MbeyaYetuOnlineTV

Haa wameshapiga ramli ya wapiga kura kwamba CCM itashinda
 
CCM Ni ileeileee ooooh Ni ileileee.

Captain komba alishaimba. Mnahangaika bure Ila umoja uliopo Kati ya rushwa, roho mbaya na CCM huwezi kuutenganisha hata kidogo.t
Nilishangaa saana maana kiukweli wapinzani Tanzania hawana pa kusemea;
eti mtangazaji wa DW ya Germany anahoji wana CCM wanasema wapinzani hawasemi chochote kazi ni kumsifia Magufuli!!
Kama vile hawajui wapinzani hawaruhusiwi kufanya mikutano kuongea na wananchi hata mikutano ya ndani Polisi wanawakamata!!
Wamezibwa ka kona, sasa hivi ni uchaguzi mpaka sasa hawajaruhusiwa kufanya kampeini, CCM kina Popole na Bashiru& Co kampeini wanafanya kila leo!!
Wapinzani kina Lema wanapitia mitihani migumu saana.
Vyombo vya habari visiwe biased vitoe nafasi ya kujieleza kwa vikundi vyote!!
 
Unaweza kufikiri kuwa vyama vya upinzani vimekufa kumbe CCM ndio imekufa kabisa na kuoza. Unaogopa watia nia kukimbilia upinzani???
 
CCM sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha kijeshi kilichojivika koti la chama cha siasa. Na bila tume hii ya uchaguzi, na vyombo vya dola, ccm haiwezi kushinda uchaguzi.
Hata wenyewe wanalijua hilo wazi.
Kilichobakia ni wananchi kuachana na uoga na kusimama pamoja na kusimamisha udhalimu na ukandamizaji wao.
Huu ni mwaka wetu.
We shall overcome.
 
Ni hivi hivi, mchana kweupe, upinzani unaanza kuchimbwa na wao wakishangilia kama inavyoonekana hapa.

Ukiachana na hivyo vitisho vya kipuuzi, angalia hawa mnaowasema kila siku akina Popole wanavyochakarika na kazi ndani ya chama wakifanya mikakati kila mahala, hata ile isiyokuwa halali na ambayo haitangazwa na kushangiliwa humu kwa sasa hivi.

Wapinzani kuja kustuka, too late, wamekwishafungwa goli! Mambo ni yale yale ya siku zote, lakini hakuna funzo linalosomeka.

Hawa, akina Popole, wapo sana huku vijijini, viongozi wa mashina wanatogota kimya kimya, wapinzani ndio kwanza wanajionyesha mijini.

Akina Popole wakiwafunda wagomea wao kila mahali, na kuwapa mbinu za kujaza fomu, wagombea wa upinzani watajaza fomu kama hawajawahi kaa darasani'
Halafu wanapokatwa kwa sababu za kipuuzi kabisa, upinzani ndio wanalilia wananchi wawaonee huruma!

Haya tunayaandika sio kwa furaha, lakini uzembe unapotokea hakuna sababu ya kuvungavunga ukweli ulivyo.

Sasa hivi wengi tunakaza roho, endapo uchaguzi utafanyika na ukaonyesha unafuu wa kutosha kwamba uvurugaji haukuwa mkubwa kiasi cha kutisha, na Magufuli akishinda katika hali hiyo tutashangilia, sasa tufanyeje kama waTanzania ndivyo walivyoamua kutokana na uzembe wa watu kufanya kazi zao kwa weledi.

Tunasubiri tu, uchaguzi ufanyike katika hali nzuri ya kuridhisha, tutameza vidonge vichungu na maisha yataendelea.

Na safari hii, baada ya kuipoteza nafasi hii, itabidi tusubiri muujiza uzuie kuwa kama Rwanda au Uganda kikamilifu kabisa.
Wanajisahau sanaa
 
19 Julai 2020
Watia Nia CCM Mbeya Wachimbwa Mkwara

Mjiandae kisaikolojia, atakayesaliti kutimulia chama, Katibu Uenezi wa CCM Mpya ndugu Humphrey Polepole aongoza jopo kuwafunda




Hakuna mtia nia wa CCM kukimbilia upinzani, ukishindwa kura za maoni. Ukitusaliti tutakufuata popote ulipo.

Mwaka huu huwezi kuharibu ushindi wa chama cha CCM ukabaki salama, tumepokea maagizo toka juu.

Chanzo: MbeyaYetuOnlineTV


Kwamba watawateka na kuwadhuru?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom