Watendaji katika Vituo vya Afya watakiwa kuacha kuwatoza fedha wajawazito, watoto walio chini ya miaka mitano na wazee

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa, amewataka watendaji katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za wilaya kuacha kuwatoza fedha wajawazito, watoto walio chini ya miaka mitano na wazee wanapohitaji huduma za afya

majaliwa.jpg



Alitoa onyo hilo alipozungumza na wananchi wa vijiji vya Ilungu na Kisamba vilivyopo wilayani Magu akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza.

"Tiba ya mama mjamzito, watoto, wazee, ni bure tumeleta fedha Sh. bilioni 10.8 kwanini watozwe hela wakati fedha zipo kama kuna mtendaji anayewatoza hao niliowataja wachukuliwe hatua kwa sababu ni wauaji pia tumewaboreshea vituo vya afya vyote ni vya kisasa, kuna sehemu ya kupima magonjwa yote, chumba cha upasuaji mdogo na mkubwa sambamba na chumba cha mama na mtoto," alisema Majaliwa.

Alisema, Magu bado kuna changamoto ya vituo vya afya, serikali itajenga vingine, ingawa imekamilisha vituo vya afya vya Kahangara, Lugeye na Kabila na kituo cha Kahangara.
"Endapo wananchi wa Magu wataichagua CCM, mkakati wa serikali ni kuhakikisha wilaya hiyo inapata maji ya uhakika.

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga, alisema wananchi wa eneo hilo wamepata mafanikio mengi kwa kutatuliwa changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.


IPPMedia
 
Hiyo kitu ilishashindikana, ukitaka mjamzito, mtoto au mzee apate tiba sahihi, zama tu mfukoni, ukienda NHIF, baadhi ya huduma dawa labda uwe waziri au mbunge, ndiyo utazipata!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Hiyo ni rushwa waziwazi..haya madaraka ya mawaziri yana margin wakati huu wa Campaigns!
 
Back
Top Bottom