Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,844
- 39,577
Kuna dhana inazidi kushika kwenye akilil za watanzania kuwaona matajiri wote wa nchi yetu wamepata utajiri wao "kiujanjaujana". Kuna wakati watu wanatamani Salim Bakhressa afilisiwe, Mengi akione cha moto, Dewji asiwe tena na kitu na wengine wengi waliopo kwenye jamii yetu.
Marekani na Uchina ni mataifa makubwa duniani kwa uchumi, lakini wao huwa hawatamani matajiri wao wawe maskini bali wanatamani maskini wawe ni matajiri wa kati ili kulinufaisha zaidi taifa lao. Sisi tunatamani sana matajiri wetu wafilisike sijui ili kiwe nini?
Wakati wanasiasa wanatuaminisha kwamba Matajiri wetu wameupata utajiri kiujanja ujanja, wao hawataki utajiri wao huhojiwe. Mkapa wakati anaingia madarakani alikuwa na mali kiasia gani na wakati anatoka alikuwa na kazi gani. Mwinyi na Kikwete je. Wabunge wetu, wakuu wa mikoa na wilaya?. kwa nini wao hawasemi kuwa mali zao wanazipata kiujanjaujanja?