Watanzania Wote ni ndugu, anayeteka ndugu zako ni adui yako

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,711
47,204
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akitaka kuamsha ari ya kila mtanzania kupigania haki za Mtanzania mwenzake, alisema kuwa "WATANZANIA WOTE NI NDUGU" Sentensi hii moja, kivitendo ni majumuisho ya matendo mema msululu.

1) Ndugu yako huwezi kumwua. Hawa viongozi wa CCM wanaowaambia polisi kuwa eti watanzania wanaowakosoa watawala, wakipotea, polisi wasiwatafute, maana yake wanataka kutuambia kuwa wao siyo ndugu wa Watanzania.

2) Kwa vile kila mtanzania ni ndugu yako, kamwe huwezi kukubali ndugu yako auawe, na wewe ukae kimya. Watanzania lazima sote kwa pamoja, tujiulize tumefanya nini kwaajili ya ndugu zetu wanaotekwa na kuuawa au kupotezwa? Au na sisi tumekwishakuwa sehemu ya haya maharamia yanayoteka watu? Kwani kukaa kimya ni automatic submission kwa ushetani unaotendeka. Mwanadamu yeyote aliye kamili, huingiwa na hasira kali ndugu yake anapoonewa au anapouawa na maharamia. Watanzania tupo wapi kuonesha hasira zetu dhidi ya watekaji, tena ambao wametoka hadharani na kutamka wazi kuwa wao huwa wanawateka watu?

3) Ndugu yako, hata ungeshawishiwa kwa pesa, madaraka au kitu chochote, kamwe huwezi kukubali utende uovu dhidi yake. Tuwaulize Polisi ambao mara nyingi wanatumika kutenda uovu dhidi ya Watanzania, hivi kweli hawa wanawaona Watanzania wote ni ndugu zao? Na sisi wananchi ambao ndugu zetu wanatendewa uovu na polisi, kama matukio yale ya Mbeya, tunatambua kuwa mtanzania yeyote anapotendewa uovu, automatic huyo anayemtendea uovu ni adui yetu sote?

4) Undugu wetu unajengwa kwa utanzania wetu, siyo kwa vyama vyetu, makabila yetu, dini zetu au tutokako, je tunashikamana vipi kwa pamoja dhidi ya yeyote anayetenda ushetani dhidi ya ndugu yetu mmoja?

5) Hata siku moja, ndugu hawezi kuiba mali ya ndugu yake. Viongozi wa CCM kila mwaka, kwenye report ya CAG huonesha namna walivyofisadi pesa za Watanzania. Kama CCM wanaiba na kufanya ufisadi kwenye pesa ya watanzania wenzao, hawa kweli ni ndugu wa Watanzania? Ni ndugu gani anaweza kumwibia ndugu yake? Hawa wametuonesha wazi kuwa ni maadui wa Watanzania.

Sasa ni wakati wa kuacha uzamani, uzamani uliojaa unyonge, woga na unafiki, tubadilime tuuvae ukweli na kusimama imara dhidi ya maadui hawa wa Watanzania. Mtanzania mwenzetu, akitendewa uovu, ni ndugu yetu ametendewa uovu. Waovu wameshikamana dhidi yetu, ni muhimu sana nasi tushikamne dhidi yao.

Tujifunze:

Urusi ni Taifa kubwa, lenye watu wengi, lenye silaha nyingi na rasilimali kubwa ya mafuta, gas na madini mbalimbali. Lakini ilipoivamia Ukraine, ilikutana na nguvu kubwa ya wananchi waliogoma kuonewa, tena wengi hawakuwahi kuwaaskari. Misaada ya mataifa mengine iliwakuta wakiwa wamewagomea Warusi, kiasi cha kikosi maalum chenye ujuzi maalum cha Urusi kuikimbia Kiev, na kuelekea Mashariki. Adui yetu japo ana nyenzo nyingi lakini tusikubali aendelee kuwateka watu kama mtu anavyochagua kuku wa kitoweo. Ni wakati wa kukata ushetani wa kutekwa watu. Kukataa kwetu kuw kwa vitendo na kauli.

Kuwateka wanaharakati wanaoikosoa serikali na watawala, ni rungu tosha la kuwafurumisha CCM nje kabisa ya madaraka.
 
Nini kifanyike
 
Back
Top Bottom