Bishanga kungekuwa na option ya kuongeza like, ningekugongea mara 40.....madoctor pia wanahusika sana ktk kuhujumuSina tabia ya kufungua nyuzi jukwaa la siasa (JLS), anga zangu ni mmu na chi chat.
Lakini katika hili la hospitali ya muhimbili kwa kuwa naijua vyema naomba niseme haya yafuatayo:
1.MRI ( magetic resonance imaging):
Mashine hii muhimbili ipo,gharama za kipimo ni sh 120,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 540,000.- kwa kipimo....
Hahahaha BADILI TABIA mleta mada mwenyewe kashindwa kusimamia mada yake lol....chit chat imemuharibu!
Ha ha ha! Yaani sweetlady, chi chat inabidi waje kumsaidia huku, hili jukwaa shughuli, @Rejeo aliwahi kupewa humu za uso, pua, kichwa ikabidi akaugulie maumivu kwa Cantalisia.
Bishanga unajua mkuu, tunashadadia bure madai ya madaktari, lakini ukweli ni kwamba baadhi yao wana-sabotage huduma za hospitali za serikali. Inasemekana hivyo vifaa wanaviharibu makusudi ili patients waende kupata huduma hiyo private hospitals ambako wanafanya kazi. Lengo ni kuingiza kipato zaidi....Kila kukicha technians from Phillips company Uholanzi wanakuja TZ kurekekibisha mashine hizi muhimbili na zinakuwa ok,wakitoka tu zinakufilia mbali, patients wanaendelea wenda private hospitals,doctors wanalalamika vifaa duni.
Tutafika kweli?
Wasi wasi wangu ni nini hasa kinasababisha mashine za dialysis,ct scanner na MRI kila kukicha muhimbili zimekufa , opearators kwa maana ya technicians , wasoma majibu kwa maana ya doctors ambao wanasimamia mashine hizi za muhimbili ndo more or less unawakuta hao hao regency,agha khan na hindu mandal wanapiga mzigo?
Mkuu unataka tutajane kwa majina hapa? Twajuana ati.
I always wonder,hivi mhando na trupu lake la tanesco wakiamua kugoma na kuzima mitambo mtera itakuwaje? Dawasco nao wakigoma na kuzima mitambo ruvu chini itakuwaje? Na staff wa huduma za anga wakizima mitambo kisa haina quality itakuwaje? Na zima moto waki down tools kisa magari mazee je? For that matter hata wazoa taka darisalama waki down tools je?
This reminds me story ya Anus iliyogoma kupitisha choo eti inadharauliwa matokeo yake ikawa ni head ache na mwili mzima kuwa dysifunctional.
Ndugu zangu hakuna taaluma iliyo bora kuliko nyingine,hata Invisible na taaluma yake ya IT ana mchango mkubwa tu katika jamii.
Nawasilisha,
Bishanga Abashaija.
Kuwa makini na toa taarifa sahihi ct scan mnh ni lak 1.7 na ni mbovu mda mrefu , mashine moja inahudumia nchi nzima haifanyiwi service itadumu vipi???
ndo maana Kambarage wa Burito alijisemeaga..'argue don't shout',
Mazee hivi ili u drive in point lazima umdhalilishe mtoa mada?
Anyway enjoy your weekend.
Bishanga, umeongea point tupu mkuu..kama ilivyo sector nyingine..madaktari wa muhimbili na kote Tanzania huhujumu vifaa vya serikali kwa ajili ya kujifaidisha kiuchumi. Tangu serikali iruhusu hospitali binafsi na kuruhusu madrs wa serikali kufanya kazi kwenye hospitali hizo wakati wao wa ziada; madrs wamekuwa wakitumia vifaa vya hospitali ya taifa kufanya diagnosis hata kwa wagonjwa waliowahudumia kwenye private hospital
a. Diagnosis inakuwa bei mbaya (private) lakini inafanyika Muhimbili kwasababu drs wanatumia connection zao; hivyo hicho kifaa cha muhimbili hakiwezi kudumu..hata kama utanunua kila siku..
b. Madrs wanashiriki katika kuziharibu au kuchukua vifaa original na kuziuza kwa hospitali binafsi; mfano kuna kesi ya dr wa serikali mawenzi hospital aliiuzia kifaa cha diagnosis hospitali ya kanisa..na kule mawenzi akaweka vifaa feki..
Kwa hivyo vifaa katika hospitali ya taifa havitadumu kwasababu zinatumika sana, zinaibiwa na hata kubadilihwa zile origini kwenda kwenye private hospitals??
Ufisadi huu upo kila mahali siyo kwa madrs tu..ni swala la kuangalia "Maadili katika nchi hii" kwenye sekta ya afya something is seriously wrong..
Mkuu sikusoma vizuri ebu fafanua.
Sina tabia ya kufungua nyuzi jukwaa la siasa (JLS), anga zangu ni mmu na chi chat.
Lakini katika hili la hospitali ya muhimbili kwa kuwa naijua vyema naomba niseme haya yafuatayo:
1.MRI ( magetic resonance imaging):
Mashine hii muhimbili ipo,gharama za kipimo ni sh 120,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 540,000.- kwa kipimo.
2.CT scanning:
Muhimbili tsh 80,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 360,000.-
3. Kidney dialysis:
Hiyo ndo usiseme.
In short,vipimo hivi day in day out ukienda muhimbili unaambiwa vimekufa, nenda agha khan,hindu mandal na regency,same doctors hao hao wa muhimbili wana handle vifaa hivi private hospitals na kutoa majibu kwa gharama kubwa,mnyonge inabidi augulie tu cant afford.
Kila kukicha technians from Phillips company Uholanzi wanakuja TZ kurekekibisha mashine hizi muhimbili na zinakuwa ok,wakitoka tu zinakufilia mbali, patients wanaendelea wenda private hospitals,doctors wanalalamika vifaa duni.
Tutafika kweli?????
Unafiki sio bure umetumwa. Vifaa unavyoongelea ni vichache haviwezi kumudu mahitaji ya wagonjwa kwa hiyo lazima viharibike mapema kwa kuzidiwa. Na kama vinasubiri watengenezaji kutoka nje ni kosa la serikali kwa sababu haijasomesha wataalamu.
Naamini hata ubora wa hivyo vifaa ni wa chini mno, vinginevyo tungeona viongozi wa CCM wakitibiwa navyo na sio kwenda nje ya nchi.
Madaktari unawaona hospitali binafsi kwa sababu wanatafuta hela ya kujikimu, au wameombwa na utawala wa hospitali husika, isitoshe bado hata huko wanayotoa ni tiba, tena kwa ubora zaidi kwani hospitali binafsi zina vifaa vya kisasa, usimamizi mzuri na mazingira yanayofaa kwa utoaji tiba. Nenda zako mmu kaongee mambo ya ngono, over!
Wewe unaonekana ni daktari ila huna exposure ya kutosha ya fani ya udaktari wa kisasa.
Vifaa kama CT scanner huwa vina number of images ambayo vinatakiwa kufanya bila kufanyiwa major service. Kutumiwa kwa mashine na nchi nzima hakupaswi kuwa sababu ya mashine kuhitaji service kabla ya kuhudumia idadi hiyo ya wagonjwa.
Kuhusu wataalam kutoka nje ndio unaonekana hujui kabisa unachoongea. Ndio maana kuna mtu humu JF alianzisha thread kuwa mitaala ya madaktari imekosewa. Unaponunua mashine inakuwa katika mkataba wa kufanyiwa service na kampuni iliyokuuzia kwa miaka fulani. Kama kampuni hiyo haina tawi nchini kwako basi watalaam hao watalazimika kutoka nje ya nchi, na hiyo huwa ni sehemu ya makubaliana ya awali juu ya nani atafidia gharama za usafiri etc. sasa unaposema kuwa serikali haijasomesha mafundi, unamaanisha kuwa mashine hiyo ingeweza kukarabatiwa na fundi yeyote. Jifunze kwanza mambo yanavyofanyika katika ulimwengu wa kisasa.
Bishanga unajua mkuu, tunashadadia bure madai ya madaktari, lakini ukweli ni kwamba baadhi yao wana-sabotage huduma za hospitali za serikali. Inasemekana hivyo vifaa wanaviharibu makusudi ili patients waende kupata huduma hiyo private hospitals ambako wanafanya kazi. Lengo ni kuingiza kipato zaidi.
Mara ngapi tumesikia tuhuma kwamba madaktari wanachua madawa hospitali za serikali na kupeleka kwenye maduka yao ya madawa au zahanati zao au kuziuza.
Tunashabikia tu madai yao lakini yanayofanyika nyuma ya pazia ni makubwa sana!