Watanzania wengi ni waoga au wanafiki?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Nakumbuka wakati wa Hayati Magufuli hata hapa mtandaoni kulikuwepo na watu ambao walikuwa wanapongeza hata mambo mabaya.

Wadau wengine walikuwa hata wakisema watu wanaopinga serikali wanajiteka, wengine walijiaminisha tu kipambe kwamba Corona itapiga nchi nyingine zote lakini haitaingia kwenye mipaka yetu ya kikoloni! kama vile Mungu ndiye aliweka mipaka. Lakini wengine hapa walikuwa wana support watesaji na wavunja sheria kama Sabaya na Makonda.

Kitu cha ajabu ni wale wale watu naowaona tena wamekuwa vinara wa haki za binadamu na sasa eti wanapenda demokrasia.

Swali Je tuna jamii ya watu wengi waoga au tuna jamii ya wanafiki wengi?
 
Sikuwahi kumuogopa JPM akiwa hai humu JF nilijua hawezi kunikamata.
 
Wwtaje kwa majina tuwafuatilie post zao kwa data.

Mimi siku zote nimekuwa nikisema "Magufuli is a country bumpkin" alivyokufa nikaendeleza "Magufuli was a country bumpkin".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom