Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

Na huwa njiuliza sana hawa mabinti wanapata wapi milion 13 ya kumlipia mtu kama faini kirahisi rahisi tu. Ok naanza kupata majibu ya maswal niliokuwa nikijiuliza.

Sio mchezo aisee yaani huoni mtu akijishughulisha lakini mwisho wa siku fujo zake ni balaa... Ku mwaga milioni kadhaa kwenye kumbi za starehe ni kawaida kabisa....
 
Na huu unga sikuizi naona.unawahusu wadada zaidi kuliko wakaka na wababa. Short cut.................
 
Tatizo ni kubwa sana,Dada zangu hebu jitambueni,tamaa haitawasadia chochote,hao waliowaagiza mzigo wala hawatawasaidia chochote mtakufa peke yenu,
 
Mhhh!kilo 150 zinakaa kwenye rectum ya mtu au begi?mh hawa mabinti wana mapango!
 
Na huwa njiuliza sana hawa mabinti wanapata wapi milion 13 ya kumlipia mtu kama faini kirahisi rahisi tu. Ok naanza kupata majibu ya maswal niliokuwa nikijiuliza.
kweli mkuu hata mimi nawazaga sana ukiunganisha biashara zetu hizi na misele ya mtu no advertisement ya biashara yake , nachoka kabisa
 
Bado ni jambo la kushangaza na kujiuliza hivi kweli walitokea Tanzania na walipitia viwanja vya ndege vya Tanzania??? kama ndio basi hatuna kweli watenda kazi pale kiwanjani kweli wasione mzigo mkubwa hivyo? Mie mwanakijiji nikija Dar huwanajiuliza magari mazuri haya yote ni hela halali na Serkali inaangalia tu Enzi za Mwalimu tayari wote hawa wangekiona. Naomba Serkali iwashughulikie MAPAPA wa madawa ya kulevy kuokoa watoto wetu jamani!!!!1

Ukaguzi airport zetu bado uko loose sana kama ni deal limesukwa ni rahisi sana hizo drugs kupitishwa!! Siku moja nilishangaa dada mmoja alivyotukagua mizigo yetu pale airport ya Mwanza!! She was so careless and alone!! So mie sishangai hizo drugs kupenya kwenye hizo airports zetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii ni aibu kwa wale waliopewa jukumu la kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya. Wanakula kodi zetu bure huku madawa yakipita kwenye viwanja vyetu vya ndege bila kizuizi chochote. Haiwezekani kg 150 zipite bila kuonekana au wenyewe ndio ninyi mnaopambana na hayo madawa?

Huwa sin imani na kamanda Nzowa! Nakumbuka aliwahi kutuhumiwa kutaka kumbambika mtoto wa Mengi drugs lakini hiyo issue ilipotezewa kiaina hebu tukumbushane iliishaje??
 
Ukaguzi airport zetu bado uko loose sana kama ni deal limesukwa ni rahisi sana hizo drugs kupitishwa!! Siku moja nilishangaa dada mmoja alivyotukagua mizigo yetu pale airport ya Mwanza!! She was so careless and alone!! So mie sishangai hizo drugs kupenya kwenye hizo airports zetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ilikuaje ukakaguliwa mizigo kwenye local airport,, kusema kweli sijawai kukaguliwa mizigo mwanza hata mara moja,,

Sehemu wanayokagua mizigo ni JKIA tena ukiwa unaenda nje ya nchi.. But kwa safari za ndani sijawai kusachiwa
 
Mpaka muda huu maafisa wote waliokuwa uwanjani cku hiyo walitwkiwa wawe nje ya kazi
 
Huku afrika kusini Wabongo wengi wapo mitaani wakiuza madawa. Jamani watu msikimbilie afrika kusini hata nchi yeyote kama hauna complete plan of what you will do ukiwa huku. Haya si mambo mazuri. madawa yanaua watu yanavunja familia etc.

Hii kesi ya hawa mabinti utagundua kwamba kuna drug barons wako nyuma yao, na watu hawa wana nguvu kubwa sana (UNTOUCHABLES) ambayo hata Nzoa anaifahamu. Haiwezekani 150kg zivushwe hapo JNIA bila kutambulika and yet huyu Nzoa hawajibiki. Ukifuatilia kwa undani hasa ile kesi waliyotaka kumbambikiza yule mtoto wa mnene wa ai pi pi utaona kuwa huyu Nzoa anahusika. Sasa mbona yupo tu kwenye kitengo ambacho kinakamata dagaa wakati papa wanatesa? Au tuamini kuwa kuna agenda ya siri ambayo watawala wanaijua? 150kg kwa watu 2 from Tz to South? No way usitilie mashaka. Hapa kuna mchezo bana!
 
Back
Top Bottom