Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

kipochi

Member
Jul 2, 2013
35
25
Waliokamatwa na 'unga' wa mabilioni ni mabinti

- Wote ni Watanzania, walianzia safari Dar, washikiliwa Afrika Kusini

NA THOBIAS MWANAKATWE | 9th July 2013


Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni
Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita NIPASHE ilipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik' zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.

Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.

Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.


CHANZO: NIPASHE Home

###########
Kwa wasomaji

Agnes Gerald, maarufu kama Agnes Masogange Alizaliwa Aprili 23, 1988 kwenye hospitali ya Mkoa wa Mbeya na akasoma Shule ya Msingi na Sekondari ya Sangu.​
 
duh kama ni uyo balaa wamekamatwa na kilo 150 za madawa zenye thamani ya bilioni 6 za kitanzania kweli walijiamini kupita na mzigo mkubwa kama huo haijawaitokea kukamatwa mzigo mkubwa kama huo huko
 
kipochi 09:11 Today
Wanawake hao ambao hawakutajwa
majina wala uraia wameshikiliwa na polisi
nchini Afrika Kusini.

Title inasema ni watanzania.
 
[video=youtube_share;EUANDIek-24]http://youtu.be/EUANDIek-24[/video]




JUL082013


WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANIA







Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.


Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.


"When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.

Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa." Alisema Muller.


Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.

Tazama video yenye habari hiyo










 
nami nashangaa title yake
huku kilichomo kikikanusa uhalisia wa uraia wao
cha kujiuliza hayo madawa yalipenyaje JKN airport?
jana tumeambiwa wamewakamata tena wawili wakielekea bangkong
nadhani wahusika wataanikwa,, Bil 6 sio mchezo
kipochi 09:11 Today
Wanawake hao ambao hawakutajwa
majina wala uraia wameshikiliwa na polisi
nchini Afrika Kusini.

Title inasema ni watanzania.
 
nami nashangaa title yake
huku kilichomo kikikanusa uhalisia wa uraia wao
cha kujiuliza hayo madawa yalipenyaje JKN airport?
jana tumeambiwa wamewakamata tena wawili wakielekea bangkong
nadhani wahusika wataanikwa,, Bil 6 sio mchezo

Kwa hali halisi ya mtandao wa madawa ya kulevya wahusika hawawezi kupatikana kitakachofanyika kama sio kuwaokoa hao waliokamatwa basi ni kuhakikisha hawafikii hatua ya kutaja nikimaanisha watauliwa kabla.
 
Back
Top Bottom