Watanzania watakavyonufaika na mkopo wa TZS trilioni 2.4 kutoka IMF

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
Kabla sijaanza kueleza ni kwa namna gani Watanzania watanufaika na mkopo wa shilingi trilioni 2.4 kutoka Shirika la Fedha Duniani, kwanza ifahamike kwamba hakuna nchi duniani ambayo haikopi, nchi zinatofautiana kiwango na sababu za kukopa.

Baada ya hilo, nielekeza kwamba mkopo ambao Tanzania imepata, sio mkopo uliochukuliwa ili kuja kulipa mishahara, bali ni mkopo utakaowezesha utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo na huduma za kijamii.

Fedha hizo zitaleta unafuu kwenye mfumuko wa bei kwa kushusha bei ya mafuta na kuwezesha uchumi jumuishi, uchumi ambao utakugusa maisha ya Watanzania wote.

Pia, zitatumika kusisimua uchumi ambao umeathiriwa na janga la UVIKO19 na vita vya Urusi na Ukaine ambavyo vimeathiri uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo ngano na mafuta duniani.

Aidha, sekta binafsi ambayo imeajiri idadi kubwa sana ya Watanzania nayo itapata unafuu, zitatumika kuwezesha utoaji wa pembejeo za kilimo zenye ruzuku na zitasaidia vijana, wanawake na makundi mbalimbali.

Mkopo huo wa masharti nafuu utatolewa katika kipindi cha miezi 40 kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

FRRu2H1XEAAwbfN.jpg
 
Binafsi natamani kiasi kikubwa cha hizo hela zitumike kustimulate uchumi na kuongeza Ajira
Mf:
1. Hivi kwa nini serikali isilipie 70% ya uekezaji wa kiwanda cha general tyre pale arusha na Private sector iweke 30% kiwanda kianze? Soko lipo wazi kabisa, ni kutamka tuu na kuanza kukusanya kodi na kuongeza ajira

2. Kwa nini serikali isiangalia dawa za binadamu tunazo agiza zaidi; ikaweka hela kiwanda mojawapo kikatengeneza? Soko lipo waziwazi; ni kuambia tu Hospitali zinunue dawa huko. Yaani ni kukusanya tu kodi na kuongeza ajira nk
3. nk nki nki nk nk

Tunapenda miradi ila nafikiri sasa tujikite pia kwenye baadhi ya miradi inayo ongeza direct Kodi (inayo jilipa) na kuajiri. Bila kupanua idadi ya wazalishaji & middle class, Hata tukipanua uigo wa kukusanya hizi kodi ndogo ndogo sioni zikiwa na impact kubwa kwenye kufufua na kuendesha uchumi.....
 
Uitaji kutunga uongo matumizi ya huo mkopo yanapangwa na IMF. Waziri nae SAP za IMF anaita maono ya raisi na kumpongeza.

Sehemu za matumizi ya hela zinapoenda ni kwenye miradi ya umwagiliaji, ufugaji wa kisasa, uvuvi na ‘quantitative easing’ (japo hilo ajaliongelea) ya kushuka kwa makusanyo ili tulipe madeni.

Miradi ya mkakati inavyosua sua ingekuwa maamuzi ya matumizi ya hizo hela ni yao unadhani wangepeleka kwenye uvuvi na ufugaji kweli.

Umeshaambiwa ni ‘Extended Credit Facility’ ni mkopo wa masharti huo; zama kukopa na kuamua matumizi yake zimekufa na Magufuli.
 
Unapokopa, the law of the thumb, kwanza ufikirie utaurudisha vipi huo mkopo..
Viongozi wetu yaelekea kwanza wanafikiri watautumia vipi au wapi. Matumizi mazuri ya mkopo kwa kweli ni kuanzisha mradi utakaojiendesha na kulipa kwa muda mfupi, yaani kuanzia baada ya kipindi cha grace. . Mradi huo baada ya kulipa ndipo unakuwa sasa rasilimali ya kufanya maendeleo. Kama tungefanya hivi Tangu Uhuru, tungeona faida ya mikopo.
Katika mazingira yetu, mkopo ungetumiwa tu katika kuboresha kilimo na yanayofungamana kwa karibu sana na kilimo (kama viwanda-kilimo, biashara-kilimo, zama na kilimo, umwagiliaji, barabara za mashambani nk) , viwanda, utalii na madini. Siyo hata kwa afya, au kujenga shule, maana maeneo haya huchukua muda mrefu kuleta tija. Haya yaachiwe serikali ipambane mayo kutokana na vyanzo vingine.
Lakini sisi ni wavivu wa fikra, twataka vya upesi upesi bila shida nyingi, na generally, viongozi wataka waonesha upesi upesi wamefanya nini, hasa hasa vitu vya kuonekana kwa macho (Barabara za juu, madaraja nk). Hakuna taswira ya kuwa mkopo utumiwe katika mambo ya long-term, ili mradi tu yatakidhi hadi miaka kumi ijayo (Kipindi cha mtawala). Baada ya mtawala kumaliza wakati wake, hayamhusu tena ni mzigo wa mtawala ajaye. Naye atakopa amwachie mtawala ajaye.....na ndiyo hapo tulipo! Hata imetokea kuomba mkopo kwa sababu ya kuwalipa wafanyakazi wa serikali!
Nafanya taswira: laiti tangu uhuru kama 60% tu ya mikopo ilichukuliwa kwa kuendeleza kilimo! Leo kusingekuwa na Mtanzania anayelima kwa kutumia jembe la mkono, wala kilimo chetu kisingetegemea mvua.... mazao yangefika masokoni siku hiyo hiyo.....kusingekuwa na tatizo la ukosefu wa ajira kamwe! Zaidi ya yote, tungekuwa tumelipa mikopo mingi.
 
hii ni mikopo ya kufurahisha wananchi wachache na wale walio karibu na "Mlezi wa Taifa"!

and of course, na kufurahisha waumini wa "Bretton Woods"!
 
Kabla sijaanza kueleza ni kwa namna gani Watanzania watanufaika na mkopo wa shilingi trilioni 2.4 kutoka Shirika la Fedha Duniani, kwanza ifahamike kwamba hakuna nchi duniani ambayo haikopi, nchi zinatofautiana kiwango na sababu za kukopa.

Baada ya hilo, nielekeza kwamba mkopo ambao Tanzania imepata, sio mkopo uliochukuliwa ili kuja kulipa mishahara, bali ni mkopo utakaowezesha utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo na huduma za kijamii.

Fedha hizo zitaleta unafuu kwenye mfumuko wa bei kwa kushusha bei ya mafuta na kuwezesha uchumi jumuishi, uchumi ambao utakugusa maisha ya Watanzania wote.

Pia, zitatumika kusisimua uchumi ambao umeathiriwa na janga la UVIKO19 na vita vya Urusi na Ukaine ambavyo vimeathiri uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo ngano na mafuta duniani.

Aidha, sekta binafsi ambayo imeajiri idadi kubwa sana ya Watanzania nayo itapata unafuu, zitatumika kuwezesha utoaji wa pembejeo za kilimo zenye ruzuku na zitasaidia vijana, wanawake na makundi mbalimbali.

Mkopo huo wa masharti nafuu utatolewa katika kipindi cha miezi 40 kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

View attachment 2297642

Kufaidika huko ndio huku kulikozaa hizi tozo.
 
Fedha hizo zitaleta unafuu kwenye mfumuko wa bei kwa kushusha bei ya mafuta na kuwezesha uchumi jumuishi, uchumi ambao utakugusa maisha ya Watanzania wote.

Pia, zitatumika kusisimua uchumi ambao umeathiriwa na janga la UVIKO19 na vita vya Urusi na Ukaine ambavyo vimeathiri uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo ngano na mafuta duniani.
Miaka nenda rudi ni misamiati ya kutupiga, kuna mkopo ulichukuliwa wa kupooza bei ya mafuta hata wiki tatu hazikwisha tukaanza kupigwa
 
Mtachekelea sasa hivi lakini baada ya miaka kadhaa mjiandae tena kulia.
Mikopo inakopwa bila ya njia na mipango ya uhakika ya jinsi ya kulipa matokeo yake deni linaenda kulipwa kwa kodi na hapo ndio msemo wa majuto ni mjukuu huanza kuwa uhalisia.
 
Back
Top Bottom